Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Wakati Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega aking’aka hatua ya makandarasi wanaojenga miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, kutokamilisha kwa wakati, Bunge nalo limeiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuwasimamia kikamilifu makandarasi.
Limeagiza mradi wa barabara ya Kabingo-Kasulu hadi Manyovu kukamilishwa kwa wakati uliopangwa ili wananchi waondokane na adha ya usafiri na usafirishaji.
Machi 5, 2025 Waziri Ulega alionyesha kukasirishwa na makandarasi wanaotekeleza mradi wa mabasi yaendayo haraka kuanzia Posta-Mwenge -Daraja la Kijazi, Mwenge hadi Tegeta, Ubungo hadi Kimara na kuwataka kufika nchini kabla ya mwisho wa mwezi huu, kutokana na miradi waliyopewa kuwa nje ya muda.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Leo Jumatano Machi 19,2025 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imetoka agizo kwa Wizara ya Ujenzi na Tanroads kuhakikisha inawasimamia vyema makandarasi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustine Vuma Holle amesema mradi huo mkubwa uliogharimu Sh400 bilioni ni mkombozi kwa wananchi wa Kigoma na maeneo jirani.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dk Charles Msonde ameahidi kuwa Serikali itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kama ulivyopangwa.
Ujenzi wa mradi huo unafanyika katika sehemu nne ambapo kipande cha Kasulu - Manyovu chenye urefu wa kilomita 68.25 utakamilika Mei 31, 2025.
Kipande cha Kanyani Junction - Mvugwe chenye urefu wa kilomita 70.5 utakamilika Oktoba 30, 2025. Huku sehemu ya Mvugwe - Nduta Junction yenye kilomita 59.35 kitakamilika Mei 7, 2025 na Nduta Junction - Kabingo yenye urefu wa kilomita 62.50 ipo kwenye uangalizi.