DAR: Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na RC Makonda yatinga Clouds Media kutoa pole kwa ajali ya moto

je wewe ungeweza kama mtu kakufitisha na bosi umeachishwa kazi .kama kapata ajali na yuko moi je unaweza kwenda kumjulia hali
 
Wanatengeneza matukio halafu wanawahi kwenda kutoa pole...

Mwaka 1932 Adolf Hitler alichoma moto jengo la Bunge la Ujerumani halafu akawahi kutoa pole na kuwatuhumu wapinzani, hivyo hivyo mwaka 1976 Idi Amini alimwua Jaji Mkuu wa nchi hiyo halafu akajitokeza haraka kulaani tukio hilo na kuahidi kuwa wahusika wote watakamatwa na watakiona cha mtema kuni, maskini kumbe alishamla nyama na baadhi ya viungo vya mwili wa huyo Jaji alivihifadhi kwenye jokofu kwenye moja ya vyumba za Ikulu ya nchi hiyo!
Hvi na ww bado una ule propaganda za mwalmu kama idd amini anakula nyama za watu duuhh
 
Kaka Chupayamaji usitake watu tubadili jina lako na liwe kichwamaji sasa manake unapotea...Kwa akili ya kawaida tu ulitegemea nini baada ya Bashite kutapatapa kwa njia zoote za kuwamaliza Clouds kushindikina nini kingefuatia...Tokea zamani amekuwa akidanganywa na ma 'ZB' wanaomzunguka 'of the likes' za akina Lemubabes, Jerry Muro, Naibu waziri wa Michezo (Shonza I think so) na wengine kibao kwamba ukizuia FIESTA umewamaliza Clouds...sasa pamoja na kutishia isifanyike kwa kuweke vikwazo kibao lukuki...jana kapewa taarifa kuwa jamaa wameshauza ticket za kutosha kama hawana akili so ata kama akizuia itakula kwa washabiki na sio Clouds....Hakuishia hapo alienda mpaka TCRA akitaka wafungiwe kutokana uropokaji wa Kibonde na yule Bacherlor Gadner lakini alichopewa sicho...wazungu walisema njia bora ya kummaliza adui yako ni kuwa karibu nae..Naona amejaribu kufuata hiyo njia.Ila ninavyomfahamu Ruge the guy he is very smart than Kusaga.
watz 2na vituko sana
 
Hongera sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Makonda kwauchapa kazi uliotukuka, wenzako huku mikoani tunawaona kwenye kukabidhi zawadi za washindi wa karata tatu aka Biko, nk.
 
hongera sana Rc wangu makonda na kamati yako kwenda kuwapa pole Clouds media group, hii inaonyesha upendo wako kwa watu wako wa d'salaam kwa kuonyesha uzalendo weka mbali maneno ya mitandaoni ya kuwa una chuki nao wakati wewe ni RC wa wote.keep it up
 
Nimepishana na msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar ukiongozwa na Mwenyekiti wake RC Makonda muda huu..!

Nadhani ni kwenda kutoa pole kwa tukio la moto lililotokea jana.
----------

Saa 2 baadaye..

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amefika Ofisi za Clouds Media akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama kutoa pole kwa ajali ya moto uliounguza sehemu ya jengo hilo..

View attachment 635547 View attachment 635548

Video..

Poleni Clouds Fm kwa janga hili la moto. Hii ni mara ya pili baada ya lile la Kitega Uchumi. Tunaamini uchunguzi utafanyika kubaini chanzo cha moto huu na kuwekwa wazi.
 
Poleni Clouds Fm kwa janga hili la moto. Hii ni mara ya pili baada ya lile la Kitega Uchumi. Tunaamini uchunguzi utafanyika kubaini chanzo cha moto huu na kuwekwa wazi.

Kama mlipuko wa office za IMMMA Advocates ulijulikana chanzo chake basi na huu wa jengo la Clouds FM utajulikana.

Na ule wizi uliotokea ofisi za Prime Attorneys kama wezi walishapatikana hapo na moto wa jengo la Clouds FM bila wasiwasi chanzo kitajulikana.

Ila kama matukio ya nyuma yamepotezewa basi na huu moto wa jengo la Clouds FM wasahau tu itawasaidia kuendelea mbele na kuwa makini na wanaokuja kutoa pole siku moja baada ya tukio.
 
Back
Top Bottom