Kamati ya Siasa Songwe yatembelea walioathirika na mvua Ilasilo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Songwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda imetembelea na kufanya ukaguzi wa athari zilizosababishwa na mvua na upepo katika Kijiji cha Ilasilo Kata ya Galula.

Katika ukaguzi huo kamati hiyo imebaini nyumba saba zimebomolewa huku 11 zikiwa zimeezuliwa mapaa baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha Novemba 13, 2023 usiku katika Kijiji cha Ilasilo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya Kamati hiyo ya Usalama ambayo pia iliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Songwe, CPA. Cecilia Kavishe kutembelea eneo hilo, Mhe, Itunda amesema kuwa Kamati hiyo imeona athari huku akiiagiza kamati ya maafa ya Kata ya Galula kufanya tathmini ili kujua athari na kuwasilisha ripoti kwa kamati ya Usalama ya Wilaya ndani ya siku tatu.

Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wananchi ambao nyumba zao zimebomoka kuwa watulivu wakati zoezi hilo la tathmini likiendeleo ili Serikali kupata uhalisia wa athari hiyo.

Mhe. Itunda ameuagiza uongozi wa kijiji kuhakikisha kuwa wale ambao nyumba zao zimebomoka kuhakikisha kuwa hawapati changamoto ya malazi wakati Serikali inashughulikia tatizo hilo.

"Kwa Pamoja Tunaijenga Songwe."

#SongweImara
#KaziIendelee
#TusongeMbelePamoja
 
Attachments

  • IMG-20231117-WA0010.jpg
    IMG-20231117-WA0010.jpg
    212.7 KB · Views: 3
  • IMG-20231117-WA0011.jpg
    IMG-20231117-WA0011.jpg
    218.6 KB · Views: 3
  • IMG-20231117-WA0012.jpg
    IMG-20231117-WA0012.jpg
    205.3 KB · Views: 3
  • IMG-20231117-WA0013.jpg
    IMG-20231117-WA0013.jpg
    217.3 KB · Views: 3
  • IMG-20231117-WA0009.jpg
    IMG-20231117-WA0009.jpg
    186 KB · Views: 4
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Songwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda imetembelea na kufanya ukaguzi wa athari zilizosababishwa na mvua na upepo katika Kijiji cha Ilasilo Kata ya Galula.

Katika ukaguzi huo kamati hiyo imebaini nyumba saba zimebomolewa huku 11 zikiwa zimeezuliwa mapaa baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kunyesha Novemba 13, 2023 usiku katika Kijiji cha Ilasilo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya Kamati hiyo ya Usalama ambayo pia iliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Songwe, CPA. Cecilia Kavishe kutembelea eneo hilo, Mhe, Itunda amesema kuwa Kamati hiyo imeona athari huku akiiagiza kamati ya maafa ya Kata ya Galula kufanya tathmini ili kujua athari na kuwasilisha ripoti kwa kamati ya Usalama ya Wilaya ndani ya siku tatu.

Mkuu wa Wilaya huyo amewataka wananchi ambao nyumba zao zimebomoka kuwa watulivu wakati zoezi hilo la tathmini likiendeleo ili Serikali kupata uhalisia wa athari hiyo.

Mhe. Itunda ameuagiza uongozi wa kijiji kuhakikisha kuwa wale ambao nyumba zao zimebomoka kuhakikisha kuwa hawapati changamoto ya malazi wakati Serikali inashughulikia tatizo hilo.

"Kwa Pamoja Tunaijenga Songwe."

#SongweImara
#KaziIendelee
#TusongeMbelePamoja
This is administration and politics we want
 
Back
Top Bottom