Kamati ya Maadili yamsimamisha Stephen Masele kutohudhuria vikao vitatu vya Bunge. Spika Ndugai apendekeza asamehewe

Hivi ni Masele aliliweka wazi kwa umma ama ni spika?
Angalia sasa hivi toka aitwe kamati ya maadili nyuzi za masele zimepunguwa humu JamiiForums nk .Zilikuwa nyingi na kwenye forum zake binafsi akijimwaga kuponda wito nk yeye ndie alianza kuzimwaga mitandaoni ndio maana nasema muulizeni Masele na kumuulize eti kosa lako nini lililokufanya hadi ukaomba msamaha bungeni.Huu wakati muafaka wa waandishi kwenda kumhoji mhusika mwenyewe hamna haja kuandika vitu vya kutunga au kufikirika mfuateni awaambie.BBC nk nendeni mkamhoji
 
Hivi kosa la Maselle ni lipi mbona halisemwi?

(Jamaa anahofu kupoteza uspika kwa Masele ... Sasa anaanza zengwe kumchafua Jamaa)

Isitoshe ndugai hapendi kupewa changamoto.....

1. Lisu alikuwa tishio ndani na nje ya bunge kashughulikuwa kotekote

2. CAG Prof Assad ni bora Kabisa, ndugai kaona hapana..... anapambana Usiku na Mchana kumuondoa CAG Prof Assad

3. Akina Bashe, Nape, Lema, Mnyika, Msigwa, Mdee Nk ni vichwa, wanaonekana kuijadili bajeti vema na kuihoji serikali vilivyo..... ndio maaduwi kwa ndugaI

Kifupi nidhaifu saaana
 
1. Kulidharau bunge
2. Kudharau mamlaka ya spika
3. Kulidhalilisha bunge
4. Na kugonganisha mihili ya dola

Chengachenga hizo zote

Aliyafanya hayo kupitia bunge gani?

La Tanzania au PAP, ndugai na kamati yake wanajidhalilisha sana
 
Kwa taarifa za uhakika leo hii Mei, 23 , Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inategemewa kuwasilisha ripoti yake Bungeni kuhusu suala la Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika Ndugu Masele. Taarifa za ndani zinadai Kamati iligawanyika kutokana na mashtaka ya Masele kuonekana kama yana shinikizo la Spika Ndugai.

Tutegemee leo mjadala mali ndani ya Bunge kutokana na ukweli kuwa Wabunge wameagawanyika sana kuhusu suala hilo na wengi wao wameanza kuwa na shaka na mwenendo wa Spika Job katika masuala ya muhimu.

Tusubiri tuone. TT.

======

UPDATES:
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani katika makosa manne Mbunge wa Shinyanga Mjini ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele na kuazimia asihudhurie mikutano ya Bunge

"Kwa niaba ya Mwenyekiti Kamati ya Maadili ya Bunge, naomba kuwasilisha mezani taarifa kuhusu Julius Masele ya kulidharau Bunge, mamlaka ya spika, kulifedhesha Bunge na kuchonganisha mihimili ya dola", amesema Maige.

Mbunge huyo Masele amehukumiwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kufuatia kosa lake hilo alilofanya, kuanzia Mei 23, 2019.

------
Spika Ndugai apendekeza Mh. Masele asamehewe

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amependekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini, na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele asamehewe kwa tuhuma na makosa aliyokuwa akituhumiwa baada ya Mbunge huyo kuomba msamaha bungeni.

Awali Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza mbunge huyo (Stephen Masele) asimamishwe kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23,
Watu siku hizi wamekuwa walemavu wa fikra, sasa huu uzi unamantiki gani wakati haujabeba maudhui yote? Soma gazeti la mwananchi kwenye mtandao utapata vyooooote alivyosema Mh. Masele?. Mbioo zooote hizi za nini, uzi kwa kijinga kabisaa huu ufutwee
 
Moderators naomba msiunganishe hii thread. Kuna mambo ya msingi sana hapa kwa nchi yetu.

Kamati inatoa taarifa juu ya hitimisho kuhojiwa kwa Masele dhidi ya tuhuma zilizomkabili. Ghafla Ndugai anapata simu urgent. Akimaliza kuongea na simu, anatoa tamko, kabla hata kamati haijamaliza kusoma matokeo ya kikao chake, kwamba Bunge limsamehe Masele. Ndivyo tunaambiwa ilikuwa.

Kama ni kweli, maana yake nini?

Nadhani wote tunakumbuka mhemuko aliokuwa nao Ndugai dhidi ya Masele. Hasira na kuonyesha kama angekuwa na uwezo angefutilia mbali Ubunge wa Masele. Ghafla Ndugai kabadilika?

Kumbukeni adhabu dhidi ya Nassari. Dhidi ya Lema. Hakuna msalie mtume - you are out! So why Masele ni tofauti ukichukulia hasira iliyoonyeshwa na Ndugai? Je ni kwa kuwa Masele anatoka kanda ya ziwa - na ni handle with care? Wengine wanasema hivyo. Au labda ni kwa kuwa ni mbunge wa CCM - adhabu ni kwa ajili ya wabunge wa upinzani tu!

Labda la msingi, nani alimpigia simu Ndugai na kutoa amri "Masele asemehewe?" Waziri Mkuu? Raisi? Na kama ndio, nani basi yuko nyuma ya kelele nyingi za Ndugai? Nani hasa ndio nguvu ya Bunge la Tanzania? Je tuna Bunge lililo huru au Bunge letu sio tu ni dhaifu, bali ni ki- puppet (kikaragosi) kinachocheza kulingana na mtu fulani nyuma ya pazia anaekichezesha kwa kamba?

Watazania wote wenye akili tunapaswa kujiuliza sana.
 
Kwa taarifa za uhakika leo hii Mei, 23 , Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inategemewa kuwasilisha ripoti yake Bungeni kuhusu suala la Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika Ndugu Masele. Taarifa za ndani zinadai Kamati iligawanyika kutokana na mashtaka ya Masele kuonekana kama yana shinikizo la Spika Ndugai.

Tutegemee leo mjadala mali ndani ya Bunge kutokana na ukweli kuwa Wabunge wameagawanyika sana kuhusu suala hilo na wengi wao wameanza kuwa na shaka na mwenendo wa Spika Job katika masuala ya muhimu.

Tusubiri tuone. TT.

======

UPDATES:
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani katika makosa manne Mbunge wa Shinyanga Mjini ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele na kuazimia asihudhurie mikutano ya Bunge

"Kwa niaba ya Mwenyekiti Kamati ya Maadili ya Bunge, naomba kuwasilisha mezani taarifa kuhusu Julius Masele ya kulidharau Bunge, mamlaka ya spika, kulifedhesha Bunge na kuchonganisha mihimili ya dola", amesema Maige.

Mbunge huyo Masele amehukumiwa kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kufuatia kosa lake hilo alilofanya, kuanzia Mei 23, 2019.

------
Spika Ndugai apendekeza Mh. Masele asamehewe

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amependekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini, na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele asamehewe kwa tuhuma na makosa aliyokuwa akituhumiwa baada ya Mbunge huyo kuomba msamaha bungeni.

Awali Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza mbunge huyo (Stephen Masele) asimamishwe kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23,

Zaidi soma:

Dodoma. Bunge la Tanzania limeridhia kumpuuza mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele ambaye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilimkuta na hatia ya kugonganisha mihimili na utovu wa nidhamu.

Kamati hiyo ilipendekeza Masele ambaye pia ni makamu wa rais wa Bunge la Afrika (PAP) kusimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge la Tanzania.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 23, 2019 bungeni jijini Dodoma baada ya kamati hiyo kuwasilisha taarifa yake hiyo.

Kabla ya wabunge kuanza kuchangia maoni ya kamati hiyo, Ndugai alihitimisha jambo hilo kwa kutaka Bunge kumpuuza Masele.

Mbali na kutaka kupuuzwa, Ndugai amesema amepokea ujumbe wa Masele kwamba anataka kuomba radhi.

Masele aliposimama alitoa tuhuma mbalimbali akidai Ndugai amewasiliana na Rais wa PAP ili amng’oe nafasi yake ya makamu wa Rais na ubunge wa Bunge hilo. Masele pia ameikataa taarifa ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomkuta na hatia.

Masele alihojiwa na kamati hiyo Jumatatu Mei 20, 2019 akituhumiwa na Ndugai kwamba amekuwa utovu wa nidhamu pamoja na kutoa maneno ya kugonganisha mihimili.

Ndugai alilieleza Bunge Mei 16, 2019 kwamba kutokana na utovu huo wa nidhamu amesimamisha uwakilishi wa Masele PAP ambako mkutano wa Bunge hilo ulikuwa ukiendelea nchini Afrika Kusini na kuagiza mbunge huyo kurejea nchini.

Alisema mara baada ya kurejea nchini, Masele atahojiwa na kamati hiyo pamoja na kamati ya maadili ya wabunge wa CCM.

Chanzo: Mwananchi
Happa sawa, acha mbio mazee
 
Ndugu zangu, kwa unyenyekevu kabisa tunaomba Spika aonyeshe kwa vitendo na kwa adhabu atoazo kuwa upinzani sio wanaokosea tu hata ndani ya ccm wapo wanaokosea. Adhabu kwa MH.Masele kuomba mwenyewe asamehewe ni ishara ya mhimili huo kukosa double standard katika kutoa adhabu. Tumeshuhudia Mahakamani Wapinzani wakipewa haki yao bila upendeleo lakini mbona bungechini ya spika ndugai halijawahi fanya hivyo?. Tupaze sauti zetu Bungeni watende haki pia.
 
Sijui kama unafahamu kwamba maselle ni mbunge wa shinyanga mjini?
Hiyo tiketi ya PAP kaipata kupitia bunge la JMT,kama kuna tuhuma za utovu wa nidhamu ni lazima waliomtuma wamuhoji.
Kwa Bhanji watu waliongea na viongozi wa chama chake,wakamfyekelea mbali
Haya majina yanayoshabihiana na alcohol ni shida tupu. Namfahamu pombe, chapombe, kapombe, mapombe, lupombe, mwapombe .... wote hawa shida tupu. Mkuu kapombe heshima kwako maana pumba unazotemaga sio za nchi hii. Ila unalitendea haki jina good keep it upper.
 
Masele aliposimama alitoa tuhuma mbalimbali akidai Ndugai amewasiliana na Rais wa PAP ili amng’oe nafasi yake ya makamu wa Rais na ubunge wa Bunge hilo. Masele pia ameikataa taarifa ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomkuta na hatia.
Naomba ufafanuzi kuhusu hii sentensi.
 
Back
Top Bottom