Kamati ya Maadili yamsimamisha Stephen Masele kutohudhuria vikao vitatu vya Bunge. Spika Ndugai apendekeza asamehewe

Kwanza ndio vizuri ili apate nafasi ya kuhudhuria kuapishwa kwa rais wa nigeria
 
Masele hakutumwa kupeleka vurugu kwenye bunge la AU.
Masele anatamani kiti cha bosi wake tu
Huyu ni kumsimamusha mwaka mzima mpa bunge liishe atafutwe muwakilishi mwingine
Hana tofauti na na Bhanji aliekua analeta vurugu EALA,Bhanji kang'olewa EALA sasa kumetulia
Yaani we jamaa comments zako zote huwa ni uharo tu, sometimes ni bora uwe unapita kimya tu.
 
Habari za uhakika, Mamlaka za juu zimemuelekeza SPIKA kuondoa hoja ya Kamati ya maadili haraka iwezekanavyo. Kumejitokeza sintofahamu Bungeni baada ya SPIKA kusema Bunge limsamehe Masele kinyume na mapendekezo ya Kamati. La kuchekesha zaidi Bunge limefikia uamuzi bila kuondoa hoja ya awali ya Kamati.
Spika kala za uso jamani, Pole sana Ndugai. Ndo umjue Magufuli.

Sasa hilo la kumfungia mikutano ni uamuzi wa nani?
 
Kwa mujibu wa ndugai NI kwamba anamekuwa akifanya mambo ya hovyo hovyo na kuichonganisha serikali na bunge. That is why alipoitwa kurudi aliwasiliana na PM badala ya spika.

Vizuri mkuu, hapa ndo alipokua anakosea Sele Boy.

Watanzania wengi hawapendi kufuata protocal na kuruka ngazi jambo ambalo si busara. Mfano kesi zilizoko mahakamani zinaendelea wanataka azishughulikie rais wakati ziko kwenye mhimili mwingine.

Masele alitakiwa kuitikia wito wa spika kwa kua waziri mkuu ni mtu mdogo kwenye mhimili wa Bunge.

Waziri mkuu hana mamlaka ya kumzuia masele asirudi. Hilo liwe fundisho kwa viongozi hasa wabunge wenye viburi.
 
Wanaohojiwa wanakua wamekamilisha tu utaratibu ila makosa yanakuepo hata kabla ya kuhojiwa wanakamati wanafanya kazi ya kuelekezwa nini wafanye na nini wasifanye...
 
Wa Tz bana yani wanaona kama Masele kaonewa vile liacheni bunge lifanye kazi yake,Bunge lina taratibu zake kama umekosa adhabu muhumu
 
Sasa hilo la kumfungia mikutano ni uamuzi wa nani?
Taarifa ya Kamati iliyosomwa ilipendekeza afungiwe mikutano 3. Wakati Mwenyekiti anamaliza kusoma, SPIKA akapata ujumbe wa SIMU toka kwa Mwenye Mamlaka ya juu, basi ikabidi awaambie Wabunge eti wampuuze na kumsamehe Masele. Hivyo Taarifa haikujadiliwa tena na wala utaratibu wa kuondoa hoja haukufanyika. SPIKA ametishwa Ndugu, kajichanganya.
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amependekeza Mbunge wa Shinyanga Mjini, na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele asamehewe kwa tuhuma na makosa aliyokuwa akituhumiwa baada ya Mbunge huyo kuomba msamaha bungeni.

Awali Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza mbunge huyo (Stephen Masele) asimamishwe kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo Alhamisi Mei 23,
 
Habari za uhakika, Mamlaka za juu zimemuelekeza SPIKA kuondoa hoja ya Kamati ya maadili haraka iwezekanavyo. Kumejitokeza sintofahamu Bungeni baada ya SPIKA kusema Bunge limsamehe Masele kinyume na mapendekezo ya Kamati. La kuchekesha zaidi Bunge limefikia uamuzi bila kuondoa hoja ya awali ya Kamati.

Spika kala za uso jamani, Pole sana Ndugai. Ndo umjue Magufuli.

Huyu mtu ni very low, u-speaker alipataje?
CCM wana kazi yakusafisha kiti cha speaker

Hizi aibu mpa lini.... Ndugai....why?

Masele kaonekana shujaa sana huko PAP na amesifiwa kwelikweli na wenzake

Huku nyumbani tunamchafuwa ..... watatuonaje wale jamaa!!!

Charity begins at home
 
Taarifa ya Kamati iliyosomwa ilipendekeza afungiwe mikutano 3. Wakati Mwenyekiti anamaliza kusoma, SPIKA akapata ujumbe wa SIMU toka kwa Mwenye Mamlaka ya juu, basi ikabidi awaambie Wabunge eti wampuuze na kumsamehe Masele. Hivyo Taarifa haikujadiliwa tena na wala utaratibu wa kuondoa hoja haukufanyika. SPIKA ametishwa Ndugu, kajichanganya.
Hiyo ndio maana ya amri toka juu...huyo Ndio Magufuli hakuna cha mhimili wala bunge huru wote wanaburizwa tu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom