VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Kamati ya Maadili ya CCM iliyokutana leo kuwahoji wanachama kadhaa wanaoonekana kama 'waleta fujo' chamani imekwama kutoa uamuzi juu ya jambo hilo leo.Chanzo cha kuaminika kutoka Kikaoni humo kinadai kuwa uamuzi umeshindikana kutokana na mambo mawili.Kwanza, waliohojiwa wote walitumia muda mwingi kulalamika,kutupiana lawama na kuzalisha tuhuma mpya ambazo Kamati inapaswa kujiridhisha nazo.
Chanzo husika kinaongeza kuwa sababu nyingine ni kuwa Mh.Benard Camilius Membe hakuwepo katika mahojiano hayo ambayo angepaswa kuwepo. Taarifa za kichama zinaonesha kuwa Mh.Membe ana ruhusa rasmi na ameambatana na Rais nje ya nchi.
'Jamaa walijipanga sana.Ni kama walijadiliana kabla.Walitupiana tuhuma waziwazi na kuzaa maswali ambayo Kamati lazima iyafuatilie kabla ya kutoa uamuzi. Lakini Kamati inaonekana kupendekeza kutoa ushauri zaidi yauamuzi mkali' kilisema chanzo hicho kilichohudhuria kikao hicho.
'Pia, uamuzi usingeweza kutolewa kwa wachache na mmoja kuachwa.Hadi naye ahojiwe na ndipo uamuzi ufikiwe. Mimi sioni kama kutakuwa na jipya' kiliongeza chanzo hicho. Waliohojiwa leo ni pamoja na Edward Lowassa,Fredrick Sumaye na William Ngeleja.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam