Kamati ya Maadili CCM yakwama kutoa uamuzi

Kamati ya Maadili CCM yakwama kutoa uamuzi

Kamati ya Maadili ya CCM iliyokutana leo kuwahoji wanachama kadhaa wanaoonekana kama 'waleta fujo' chamani imekwama kutoa uamuzi juu ya jambo hilo leo.Chanzo cha kuaminika kutoka Kikaoni humo kinadai kuwa uamuzi umeshindikana kutokana na mambo mawili.Kwanza, waliohojiwa wote walitumia muda mwingi kulalamika,kutupiana lawama na kuzalisha tuhuma mpya ambazo Kamati inapaswa kujiridhisha nazo.

Chanzo husika kinaongeza kuwa sababu nyingine ni kuwa Mh.Benard Camilius Membe hakuwepo katika mahojiano hayo ambayo angepaswa kuwepo. Taarifa za kichama zinaonesha kuwa Mh.Membe ana ruhusa rasmi na ameambatana na Rais nje ya nchi.

'Jamaa walijipanga sana.Ni kama walijadiliana kabla.Walitupiana tuhuma waziwazi na kuzaa maswali ambayo Kamati lazima iyafuatilie kabla ya kutoa uamuzi. Lakini Kamati inaonekana kupendekeza kutoa ushauri zaidi yauamuzi mkali' kilisema chanzo hicho kilichohudhuria kikao hicho.

'Pia, uamuzi usingeweza kutolewa kwa wachache na mmoja kuachwa.Hadi naye ahojiwe na ndipo uamuzi ufikiwe. Mimi sioni kama kutakuwa na jipya' kiliongeza chanzo hicho. Waliohojiwa leo ni pamoja na Edward Lowassa,Fredrick Sumaye na William Ngeleja.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

umekurupuka kupost kwa kujifanya una chanzo,.tulia kuhojiwa sio lazima tuhuma ziwe za kweli,,ulitaka maamuz gani watoe
 
Hata mi nilishangaa, maana waliohojiwa wengine wana nguvu kuliko CCM yenyewe, sipati picha Mangula akimhoji Lowasa
 
Mleta mada unatokea chama cha demokrasia na maendeleo ,hakina msemaji,utasikia kauli ya mnyika,lema,msigwa,slaa,mbowe na vifaranga wengine,ccm ina utaratibu wake,wakimaliza mahojiano watatoa taarifa yao rasmi,wewe unawashwa tu kujikimbiza hapa jamvini na taarifa zako zisizokuwa na kichwa wala miguu
 
hiyo kamati ina watu wepesi sana halafu MASIKINI WATUPU ! Haiwezi kuwakabili MAFISADI WA CCM , kinachofanyika ni kupotezeana muda tu .
Nasikia kikao kimefadhiliwa na Rostam akisaidiwa na Raja
 
mimi nafikiri tumezoea kupoteza muda sana nchi hii
 
Kamati ya Maadili ya CCM iliyokutana leo kuwahoji wanachama kadhaa wanaoonekana kama 'waleta fujo' chamani imekwama kutoa uamuzi juu ya jambo hilo leo.Chanzo cha kuaminika kutoka Kikaoni humo kinadai kuwa uamuzi umeshindikana kutokana na mambo mawili.Kwanza, waliohojiwa wote walitumia muda mwingi kulalamika,kutupiana lawama na kuzalisha tuhuma mpya ambazo Kamati inapaswa kujiridhisha nazo.

Chanzo husika kinaongeza kuwa sababu nyingine ni kuwa Mh.Benard Camilius Membe hakuwepo katika mahojiano hayo ambayo angepaswa kuwepo. Taarifa za kichama zinaonesha kuwa Mh.Membe ana ruhusa rasmi na ameambatana na Rais nje ya nchi.

'Jamaa walijipanga sana.Ni kama walijadiliana kabla.Walitupiana tuhuma waziwazi na kuzaa maswali ambayo Kamati lazima iyafuatilie kabla ya kutoa uamuzi. Lakini Kamati inaonekana kupendekeza kutoa ushauri zaidi yauamuzi mkali' kilisema chanzo hicho kilichohudhuria kikao hicho.

'Pia, uamuzi usingeweza kutolewa kwa wachache na mmoja kuachwa.Hadi naye ahojiwe na ndipo uamuzi ufikiwe. Mimi sioni kama kutakuwa na jipya' kiliongeza chanzo hicho. Waliohojiwa leo ni pamoja na Edward Lowassa,Fredrick Sumaye na William Ngeleja.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kwani wewe ni msemaji wa CCM? TUSUBIRI muda ukifika CCM kupitia msemaji wake watatupa habari juu ya kile kilichojiri. Huu udaku Peleka BAVICHA.
 
....naona mzee Mangula,anataka kuionyesha jamii kwamba anatekeleza maagizo ya M/kiti wake,ila kwa ufupi hizi ni bla bla bla za siku zote za magamba!
 
CCM ni Chama cha Kidemokrasia, watayamaliza kwa Busara hakutakuwa na Ngumi wala watu kuporwa Laptop na kUSHUSHIWA vitofa vya Kichwa.Mbowe ana mzidi Mwenyekiti wetu vitu vitatu.

1) Makengeza
2)Uwezo wa Kusugua Santuri kwenye kumbi ya Muziki.
3) Uongo wa Kipropaganda e.g

Chadema yaibuka Kidedea kwa kujizolea Ushindi wa Kishindo wa Kata TATU huku CCM ikigaragazwa VIBAYA SANA kwa kuambulia Viti Ishirini na Nne tu katika Uchaguzi wa Madiwani hivi karibuni. Source Gazeti la Mbowe Tanzania Daima.

Wewe ka.h.a.ba vp tena Mbowe kaingiaje hapa? Tumia akili katka kuwazua mambo.
 
Mleta mada unatokea chama cha demokrasia na maendeleo ,hakina msemaji,utasikia kauli ya mnyika,lema,msigwa,slaa,mbowe na vifaranga wengine,ccm ina utaratibu wake,wakimaliza mahojiano watatoa taarifa yao rasmi,wewe unawashwa tu kujikimbiza hapa jamvini na taarifa zako zisizokuwa na kichwa wala miguu

Wewe mwanadada tulia,CHADEMA inathubutu kuchukua hatua hilo liko wazi.Vp ccma na kujivua gamba na mawaziri mizigo imetekeleza?
 
Ngojeni muone mwendelezo wa hii filamu.
Mimi nadhani Ccm wanataka kujiosha kwenye jamii kuhusu kushughulikia wanachama wake. Ila pia inataka iwaaminishe watanzania kuwa huhitaji kutimua wasaliti bali kuwaonya tu na hivyo kuleta suala la Zzk kuonewa kwa upya na kukifanya Cdm kionekane kilifanya maamuzi kwa kukurupuka.
 
Ndani ya hicho chama simwoni mtu yoyote anayeweza ku-disclipe mamvi, huyu ameisha jibinafsishia chama na kipo mfukoni mwake, kinachofanyika ni hofu tu ya baadhi ya vigogo wakijua siku akichukua nchi huyu Masai atawalipizia kisasi, kwa jinsi ambavyo Watanzania tulivyo wasahaulifu, nina mashaka sana kama Mmonduri huyu hata kua Ikulu next year, ni suala la kusubiri! Nina tazama Bungeni, siku akisema kitu tu, wabunge robo 3 toka ccm humshangilia, hivi hiyo inaonesha nini kama sio mahaba kwake, siku ile alipomnywesha pilipili mwenyekiti wake pale Dodoma juu ya tuhuma za Richmond, hadi wajumbe wa magambas inaonekana walikua upande wake, namwone sana huruma nepi Nnauye kwenye hili!
 
Huko ni kupoteza muda na pesa. Toka lini kutaka kugombea urais ikawa ni kosa mpaka watu wahojiwe? Kwanza hawa wanaonesha nia ndio wazuri kwasababu wanatupa muda wa kuwatathmini kuliko hao watakao kuja ghafla. Ukweli ni kuwa uchaguzi ukiisha ni wakati mwafaka kujipanga kwa uchaguzi mwingine. Hao wanaohojiwa wameonesha nia ya kutaka kugombea urais na hakuna aliyetangaza rasmi kuwa atagombea urais. Kosa lingekuwa kama wanataka kumwondoa rais aliyepo kabla ya muda wake. Sasa kama ni kweli rais aliyepo ana maliza muda wake na hatoruhusiwa kugombea tena kwa mujibu wa katiba kuna kosa gani kwa wengine kujiandaa kuchukua nafasi yake?
 
CCM YA Aliyoiacha Mwl nyerere na hii ya Leo ni Tofauti ! Ama kweli moto hauzai moto huzaa jivu !!
kipindi hicho hakukuwa na uchaguzi bali justification tu - we uliona wapi unapigia kura kati ya mtu na kivuli?

attachment.php
 
Iwe kweli isiwe kweli
Uwezo wa kumuondoa lowasa hawana
huu ndiyo ukweli - unless aamue mwenyewe kuachana na urais na hiyo ndiyo itakuwa pona ya CCM, vinginevyo ni balaa maana jama ana siri lukuki kiasi hakuna mtu ndani ya CCM ya leo atamweka kitimoto.
 
Back
Top Bottom