Kamati ya Maadili CCM yakwama kutoa uamuzi

Kamati ya Maadili CCM yakwama kutoa uamuzi

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kamati ya Maadili ya CCM iliyokutana leo kuwahoji wanachama kadhaa wanaoonekana kama 'waleta fujo' chamani imekwama kutoa uamuzi juu ya jambo hilo leo.Chanzo cha kuaminika kutoka Kikaoni humo kinadai kuwa uamuzi umeshindikana kutokana na mambo mawili.Kwanza, waliohojiwa wote walitumia muda mwingi kulalamika,kutupiana lawama na kuzalisha tuhuma mpya ambazo Kamati inapaswa kujiridhisha nazo.

Chanzo husika kinaongeza kuwa sababu nyingine ni kuwa Mh.Benard Camilius Membe hakuwepo katika mahojiano hayo ambayo angepaswa kuwepo. Taarifa za kichama zinaonesha kuwa Mh.Membe ana ruhusa rasmi na ameambatana na Rais nje ya nchi.

'Jamaa walijipanga sana.Ni kama walijadiliana kabla.Walitupiana tuhuma waziwazi na kuzaa maswali ambayo Kamati lazima iyafuatilie kabla ya kutoa uamuzi. Lakini Kamati inaonekana kupendekeza kutoa ushauri zaidi yauamuzi mkali' kilisema chanzo hicho kilichohudhuria kikao hicho.

'Pia, uamuzi usingeweza kutolewa kwa wachache na mmoja kuachwa.Hadi naye ahojiwe na ndipo uamuzi ufikiwe. Mimi sioni kama kutakuwa na jipya' kiliongeza chanzo hicho. Waliohojiwa leo ni pamoja na Edward Lowassa,Fredrick Sumaye na William Ngeleja.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Hiyo ilikuwa danganya toto tu, utakuja kusikia hawa jamaa wakila matapishi yao kwa ridhaa zao. Kwani wale Mawaziri MIZIGO si walihojiwa, hatimaye mh. Rais aliwarudisha kwenye nafasi zao kwa KISHINDO.
 
Hamna kitu hapo pheeeeeeeeeeew,kutupotezea muda tu.
 
CCM ina utaratibu wake wa kutoa Habari kwa Umma. Vuta subira..

Wataichakachua hiyo TAARIFA na kuifanya as if nothing happened...

CCM ni CULT -- Haitaweza kufanya kama CUF na CHADEMA wanavyofanya kwa Wanachama NONGWA...
 
hiyo kamati ina watu wepesi sana halafu MASIKINI WATUPU ! Haiwezi kuwakabili MAFISADI WA CCM , kinachofanyika ni kupotezeana muda tu .
 
hawana ubavu wa kuwatimua wasaliti kama chadema
hawana ubavu wa kuchukua maamuzi magumu
kwa vyoyote mmoja wao ndie atachukua kijiti cha urais,sio mwingine ni Lowassa ingawa hatashinda
wasipompa chama kitapasuka vipande vitatu.
 
Vua gamba i wapi??? Magamba yalivuka,pamoja na mbwembwe zooooo........te? Mangula ameshughulikia waliongia kwa madarakani kwa rushwa,au miezi sita alikuwa na maana miaka sita??Labda mimi sikumsikia vizuri! Leo tuna uhakika gani wa utekelezaji wa hayo wanayotueleza??
 
Tutolee umbea hapa. Wewe ni msemaji wa chadema unajidai kujifanya ccm. Huu ni upuuzi mwili mzima
 
Nasoma habari hii kwakuwa nimekosa usingizi tu,lakini si matarajio eti ccm wanajipya tofauti na maneno yakwenye kahawa
 
CCM ni Chama cha Kidemokrasia, watayamaliza kwa Busara hakutakuwa na Ngumi wala watu kuporwa Laptop na kUSHUSHIWA vitofa vya Kichwa.Mbowe ana mzidi Mwenyekiti wetu vitu vitatu.

1) Makengeza
2)Uwezo wa Kusugua Santuri kwenye kumbi ya Muziki.
3) Uongo wa Kipropaganda e.g

Chadema yaibuka Kidedea kwa kujizolea Ushindi wa Kishindo wa Kata TATU huku CCM ikigaragazwa VIBAYA SANA kwa kuambulia Viti Ishirini na Nne tu katika Uchaguzi wa Madiwani hivi karibuni. Source Gazeti la Mbowe Tanzania Daima.
 
CCM ni Chama cha Kidemokrasia, watayamaliza kwa Busara hakutakuwa na Ngumi wala watu kuporwa Laptop na kUSHUSHIWA vitofa vya Kichwa.Mbowe ana mzidi Mwenyekiti wetu vitu vitatu.

1) Makengeza
2)Uwezo wa Kusugua Santuri kwenye kumbi ya Muziki.
3) Uongo wa Kipropaganda e.g

Chadema yaibuka Kidedea kwa kujizolea Ushindi wa Kishindo wa Kata TATU huku CCM ikigaragazwa VIBAYA SANA kwa kuambulia Viti Ishirini na Nne tu katika Uchaguzi wa Madiwani hivi karibuni. Source Gazeti la Mbowe Tanzania Daima.

daha kuna watu ni wa kuwa hurumia tu hapa duniani!!
 
CCM YA Aliyoiacha Mwl nyerere na hii ya Leo ni Tofauti ! Ama kweli moto hauzai moto huzaa jivu !!
 

Attachments

  • 1392325427755.jpg
    1392325427755.jpg
    45.5 KB · Views: 304
Back
Top Bottom