Kamati ya hamasa ya Taifa Stars ipo wapi? Hao akina Joti na Mwijaku wamehamasisha nini?

Yaani hii nchi Ina vitu vinachekesha kweli kweli!

Mwanzoni mwa mwezi huu wa January wizara ya michezo na ilitangaza kamati ya hamasa Kwa ajili ya kuhamasisha mashabiki kuishangilia taifa stars.

Watu mbalimbali akiwemo Joti, Mwijaku, Baba levo, Eng Hersi n.k waliteuliwa lakini Cha kushangaza haieleweki hii kamati hizo hamasa inafanyia wapi!

Hivi Sasa taifa stars ipo Ivory coast inashiriki mashindano ya kumtafuta bingwa wa Africa ila haieleweki Hersi na wenzake akina Mwijaku hamasa wanafanyia wapi, maana hata kusikia wakizungumzia timu ya taifa hicho kitu hakionekana wala kusikika!

Hebu wizara na wadau wengine wanajua hii kamati ilipo watuambie!
Tz hatujawahi kuwa na akili
 
Back
Top Bottom