Kamati Kuu ya CHADEMA yaahirishwa kufanyika Zanzibar

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
KUFUATIA kifo cha Mbunge Jeremiah Sumari, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeamua mkutano wa kawaida wa Kamati Kuu ya chama uliokuwa ufanyike Zanzibar kuanzia Januari 21, 2012 mpaka Januari 22, 2012, sasa utafanyika Dar es Salaam.

CHADEMA imefikia uamuzi huo ili kuwezesha viongozi wake wakuu wa chama, wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbrod Slaa kuwa karibu ili kujumuika na kuifariji familia ya marehemu pamoja na kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Sumari.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Jeremia Sumari, mahali pema peponi, Amina.

Imetolewa leo Januari 20, 2012
John Mnyika (Mb),
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Ahsante kwa taariifa ila uwakilishi wa Uzini tutashiriki uchaguzi?

Bila shaka, bila shaka kamanda. Kwa nguvu zote kabisa mkuu. CHADEMA kinajiandaa kuwa sauti ya watu wa Zanzibar, kwa maana ya kushika hatamu za chama mbadala (upinzani?). Hii ni baada ya wananchi wa Zanzibar kukosa msemaji wa kuwasemea dhidi ya madhira ya watawala/serikali. Utakuwa ni muda mwafaka wa CHADEMA kufanya siasa za Zanzibar kadri ya mahitaji ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, wapenda demokrasia na maendeleo.
 
Walikua wanatafuta tu sababu hao wasepe, wanajua fika Zanzibar hawatakiwi hata kwa kutupiwa mbwa.
 
Bila shaka, bila shaka kamanda. Kwa nguvu zote kabisa mkuu. CHADEMA kinajiandaa kuwa sauti ya watu wa Zanzibar, kwa maana ya kushika hatamu za chama mbadala (upinzani?). Hii ni baada ya wananchi wa Zanzibar kukosa msemaji wa kuwasemea dhidi ya madhira ya watawala/serikali. Utakuwa ni muda mwafaka wa CHADEMA kufanya siasa za Zanzibar kadri ya mahitaji ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, wapenda demokrasia na maendeleo.

Hilo Kani likubalike Zanzibar? Wewe unachonga sana na Wana wa Zanzibar kumbeeeee!!!
 
Bila shaka, bila shaka kamanda. Kwa nguvu zote kabisa mkuu. CHADEMA kinajiandaa kuwa sauti ya watu wa Zanzibar, kwa maana ya kushika hatamu za chama mbadala (upinzani?). Hii ni baada ya wananchi wa Zanzibar kukosa msemaji wa kuwasemea dhidi ya madhira ya watawala/serikali. Utakuwa ni muda mwafaka wa CHADEMA kufanya siasa za Zanzibar kadri ya mahitaji ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, wapenda demokrasia na maendeleo.

Hilo KANISA likubalike Zanzibar? Wewe unachonga sana na Wana wa Zanzibar kumbeeeee!!!
 
Asante kamanda Makene.CDM wameona mbali kukupa nafasi uliyonayo .....maana ingawa una umri mdogo mambo uyafanyayo yanastahili pongezi.Kule tu kuwahi kuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la The Hill Observer la UDSM ni CV nzito sana, ukijumlisha na na enzi zile tuko wote High School tunachangishana mia mia ili kupata 500 ya kununua gazeti la Rai la miaka hiyo
 
....................Kule tu kuwahi kuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la The Hill Observer la UDSM ni CV nzito sana, ukijumlisha na na enzi zile tuko wote High School tunachangishana mia mia ili kupata 500 ya kununua gazeti la Rai la miaka hiyo
Mkuu ingependeza kama ungem-pm tu, haya ukiyoyaeleza yako nje ya topic
 
Asante kwa taarifa makamanda! Hicho ndo chama makini, na chenye watu makini...,
keep it up CDM!!
 
........... enzi zile tuko wote High School tunachangishana mia mia ili kupata 500 ya kununua gazeti la Rai la miaka hiyo
Mbali na kwenda out of topic lakini unataka kutuambia kuwa wewe bado ni mtoto mdogo. Maana bei ya Rai kufika sh 500 ilikuwa mwaka 2011 mwaka ambao ulikuwa High school
 
Back
Top Bottom