Kamati Kuu kukata jina la Lowassa

Kamati Kuu kukata jina la Lowassa

Kufuatia kikao cha Kamati Kuu ya CCM kinachofanyika huko Zanzibar, kuna uwezekano mkubwa jina la Lowassa likakatwa kutoka kwenye orodha ya wanaCCM watakaopeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015. Hii ni kwa sababu baada ya yeye na makada wengine kufungiwa kwa muda wa mwaka mmoja kwa sababu ya kuanza "mbio" mapema, bado aliendelea kujifanyia kampeni kama kawaida.

Chanzo: RFA

:israel:
Sasa umefaidika mini na huo uzushi wako wewe na RFA yako maana CC imemalizika na Ngayai hajakatwa Jina na anazidi kuchanja mbuga
 
KATIKA MIAKA YOTE HIYO ALIYOKUWA KIONGOZI NDUGU LOWASA , AMEFANYA NINI CHA KUPIGIWA MFANO ? AU UmEAMUA KUJIDHALILISHA TU ?

Aliyofanya yako Wazi! Wala siyahitaji kuyaorodhesha hapa. Hata nyimbo zimesha tungwa kuhusu alofanya ndugu Lowassa. Kwa vile wewe ni mvivu wakusoma naomba utafute zile nyimbo usikilize!
 
Waimbaji wa Tanzania hata masikini kama wewe unaweza kuwanunua tu , bei yao iko chini mno , aliyofanya lowasa wayaone waimbaji tu !
 
lowassa ni fisadi km mafisadi wengine kina slaa na mbowe ktk saccos yao na mfano wa hawa watu hawawezi kupata madaraka nchi hii,wakatawale somalia
membe for 2015 hana mpinzani
 
atang'oka tu ccm hatuwezi kumsimamisha fisadi,aende huko ukawa kwa wakaskazini wenzake na mapadri,halafu hao wasijisumbue ccm tuna historia ya kusimamisha wagombea wasio na kashfa ya ufisadi na wenye uzoefu kwenye international relation nadhani wenye akili wamenielewa
Kama ufisadi watanzania wote ni mafisadi. Tunazidiana viwango tu. Mwenye ufisadi usiolipa sana anamwonea wivu mwenye ufisadi wenye tija. Kwani Mtanzania inakuwaje anaweza kuishi kwa mshahara chini ya laki Tano kwa mwezi, yeye na familia ya watu SITA tu ya kisheria, katika bei juu kwa kila unachokigusa,nauli za daladala zilizopo, decently ukapeleka watoto shuleni msingi, sekondari na vyuo wakati huo unalisha waliomo ndani ya nyumba yako wajomba na shangazi na uwapelekee wazazi wenu wa kikke na kiume mahitaji ya lazima, usisahau bili za kila mwezi za maji na umeme na mawasiliano mpaka whatsapp? kama wewe sio fisadi sema sasa, unaishije na kwa mshahara huo unaweza kulipa pango la nyumba kila mwezi na pia nakuona uko nadhifu sana unaogea sabuni na kupaka mafuta nywele zako? Sema sasa....Ammmah! Si useme tu? Lowasa....Lowasa....kila kukicha, Lowasa.....Kumbe kweli nyani haoni masaburi yake. Na huyo nyumba ndogo yako unaranda bure hata soda au maji uhai humpi?

Acha ushororo wewe, Lowasa kama alivyo binadamu yeyote anazo kasoro zake lakini uzalendo anao. Leo hii sema kama Shinyanga wangepata maji kutoka ziwa Victoria kwa hofu ya mikataba ya kikoloni kuzuia Tanzania iniwape watu wake maji ili Farao amwagilie maua yake? Kwa hiyo unataka nani agombee uraisi wakati wewe umedwarf?
 
Kipofu hata ukimwonyesha nyumba iliyojengwa hataiona ng'o! Ubishi tu kukalia kwa sababu mazoea ni kama tabia. Hata huo muda wa kufanya kazi wewe umeinamia key board kumwandika Lowasa ati fisadi, mbona unaiibia serikali muda wake halafu unalalamika mshahara hautoshi wakati hufanyi kazi? Wewe umeponaje ufisadi hapo?
 
Aliyofanya yako Wazi! Wala siyahitaji kuyaorodhesha hapa. Hata nyimbo zimesha tungwa kuhusu alofanya ndugu Lowassa. Kwa vile wewe ni mvivu wakusoma naomba utafute zile nyimbo usikilize!

Hivi wewe unajitambua kweli? Kwanza shule zimefunguliwa tangu jana, kwanini hujaenda shule leo? Ngoja nikamwambie mwalimu wako wa shule ya Kata unayosoma.
 
Aliyofanya yako Wazi! Wala siyahitaji kuyaorodhesha hapa. Hata nyimbo zimesha tungwa kuhusu alofanya ndugu Lowassa. Kwa vile wewe ni mvivu wakusoma naomba utafute zile nyimbo usikilize!

mkuu wewe ni ke au me? mbona kama vile unaandika mipasho? taarabu na rusha roho za kike zimekuharibu kichwa!
 
Kama ufisadi watanzania wote ni mafisadi. Tunazidiana viwango tu. Mwenye ufisadi usiolipa sana anamwonea wivu mwenye ufisadi wenye tija. Kwani Mtanzania inakuwaje anaweza kuishi kwa mshahara chini ya laki Tano kwa mwezi, yeye na familia ya watu SITA tu ya kisheria, katika bei juu kwa kila unachokigusa,nauli za daladala zilizopo, decently ukapeleka watoto shuleni msingi, sekondari na vyuo wakati huo unalisha waliomo ndani ya nyumba yako wajomba na shangazi na uwapelekee wazazi wenu wa kikke na kiume mahitaji ya lazima, usisahau bili za kila mwezi za maji na umeme na mawasiliano mpaka whatsapp? kama wewe sio fisadi sema sasa, unaishije na kwa mshahara huo unaweza kulipa pango la nyumba kila mwezi na pia nakuona uko nadhifu sana unaogea sabuni na kupaka mafuta nywele zako? Sema sasa....Ammmah! Si useme tu? Lowasa....Lowasa....kila kukicha, Lowasa.....Kumbe kweli nyani haoni masaburi yake. Na huyo nyumba ndogo yako unaranda bure hata soda au maji uhai humpi?

Acha ushororo wewe, Lowasa kama alivyo binadamu yeyote anazo kasoro zake lakini uzalendo anao. Leo hii sema kama Shinyanga wangepata maji kutoka ziwa Victoria kwa hofu ya mikataba ya kikoloni kuzuia Tanzania iniwape watu wake maji ili Farao amwagilie maua yake? Kwa hiyo unataka nani agombee uraisi wakati wewe umedwarf?

kwa hiyo unatutangazia kwamba wewe ni FISADI? ngoja niwatonye TAKUKURU waje kukubeba. halafu unavyoandika utadhani unatunga mashairi ya rusharoho!
 
Kama umekubali kuwa mimi name ni mtanzania basi tayari umekubali kwamba mimi name ni fisadi. By definition hata hao TAKUKURU kama ni watanzania pia ni MAFISADI TU! Hajapona hata mmoja. Tusinyoosheane kidole bali tuangalie vidole vitatu vinaaelekewa kwa nani. Wakija kwangu hao maana yake tutakuwa tunachunguzana levels of corruption each one of us has. KWISHA? Viwango vya ufisadi wa Mtanzania vinazidiana lakini wote wote wote ni mafisadi tu! Ukitaka kupona ukane utanzania wako.
 
kwa hiyo wewe unashuri nini kifanyike ili kuondoa janga la UFISADI katika taifa hili masikini na ombaomba? au unataka wale wenye ufisadi mogo wajitume kufanya ufisadi kwa bidii ili wapunguze malalamiko na waache kuwasakama mafisadi papa? maana naona kama bado sijakuelewa vile.
 
Huyu jamaa EL wanamzuia lkn wp?anakuja kama nvua atawanyeshea tu, hakuna mbwa anayefukuza simba.
 
Lowassa Ana mvuto mdogo sana ndani ya ccm na nivigumu sana lowassa kupata ridhaa ya kupeperusha bendera hiyo ya kijani kuelekea ikulu, miongoni mwa wafuasi wakubwa wa lowassa ni wananchi wa kipato cha chino tena easily na weledi juu ya siasa bora kwa maendeleo ya Tanzania,
 
kwa hiyo unatutangazia kwamba wewe ni FISADI? ngoja niwatonye TAKUKURU waje kukubeba. halafu unavyoandika utadhani unatunga mashairi ya rusharoho!

Umeungana nami! Lowasa ni President ajaye!
 
Kama ufisadi watanzania wote ni mafisadi. Tunazidiana viwango tu. Mwenye ufisadi usiolipa sana anamwonea wivu mwenye ufisadi wenye tija. Kwani Mtanzania inakuwaje anaweza kuishi kwa mshahara chini ya laki Tano kwa mwezi, yeye na familia ya watu SITA tu ya kisheria, katika bei juu kwa kila unachokigusa,nauli za daladala zilizopo, decently ukapeleka watoto shuleni msingi, sekondari na vyuo wakati huo unalisha waliomo ndani ya nyumba yako wajomba na shangazi na uwapelekee wazazi wenu wa kikke na kiume mahitaji ya lazima, usisahau bili za kila mwezi za maji na umeme na mawasiliano mpaka whatsapp? kama wewe sio fisadi sema sasa, unaishije na kwa mshahara huo unaweza kulipa pango la nyumba kila mwezi na pia nakuona uko nadhifu sana unaogea sabuni na kupaka mafuta nywele zako? Sema sasa....Ammmah! Si useme tu? Lowasa....Lowasa....kila kukicha, Lowasa.....Kumbe kweli nyani haoni masaburi yake. Na huyo nyumba ndogo yako unaranda bure hata soda au maji uhai humpi?

Acha ushororo wewe, Lowasa kama alivyo binadamu yeyote anazo kasoro zake lakini uzalendo anao. Leo hii sema kama Shinyanga wangepata maji kutoka ziwa Victoria kwa hofu ya mikataba ya kikoloni kuzuia Tanzania iniwape watu wake maji ili Farao amwagilie maua yake? Kwa hiyo unataka nani agombee uraisi wakati wewe umedwarf?

UNATIA HASIRA WANA WA INNJI HII.... unashanga anaepokea 500,000/= na anasavive!!
me napokea 120,000/ watoto 3 + mke, chumba kimoja, naishi kongowe kazi Tegeta na siku zinaenda
hiyo 500,000= sijawahi kuisikia kuiona. unatiana machungu tu. aghhhhhhrrrrrrrr!!!!!!!
 
kwa mtazamo wangu nionavyo mimi kiongozi ambae naona angalao amewajibika kwa kujaribu kuwatendea haki wana wa nchi hii ni MH. MWAKYEMBE. nathubutu kusema huyu ameafanya yale yasiyowezekana kufanywa na viongozi weengi ndani ya serikali ya CCM waliopewa majukumu na wana wa nchi ili kuwatumikia.
AMETHUBUTU KUFANYA YUALIYOSHINDIKANA NDANI YA MIAKA 20 YA SHIRIKA LA RELI KWA KULETA USAFIRI MPYA WA TRENI na pia kupunguza kero ya usafiri hapo mjini DAR kwa treni yake ile maarufu kama YA MWAKYEMBE.
angalao huyu naona anadhamira ya kweli ya kuwatendea haki wana wa nchi hii yenye utajiri lukuki na wana wa nchi walio maskini kupindukia.
ANAWEZA KUPOKEA KIJITI CHA RAIS DHAIFU TULIYE NAYE.. na kututoa katika dhahama ya umasikini uliokithiri.
kama atajitokeza kuchukua jukumu la kuendesha innji hii nashauri kiupole kabisa TUMKUBALI NA KUMSAPOTI ili atutoe katika janga hili la umaskini.
ANGALIZO:
Ikumbukwe huyu jamaa msidhani amesahau madhila aliyofanyiwa na FISADI NGOYAI. tena si mara moja ni zaidi ya mara mbili katika harakati za kutaka kumuondoa duniani kisa ni huyu bwana MWAKYEMBE kukomalia ufisadi wa RICHMONDEEEE uliyokuwa umesimamiwa na na huyu fisadi EL!!

na akitemwa huyu MWAKYEMBE!! Patachimbika endapo FISADI ATAPEWA NAFASI ya kupeperusha rangi ya kijani.
yatatolewa yoote yanayomhusu fisadi ambayo tusiyo yajua.
STAY TUNE!!!!!!!!!!!![/
B]
 
kwa hiyo wewe unashuri nini kifanyike ili kuondoa janga la UFISADI katika taifa hili masikini na ombaomba? au unataka wale wenye ufisadi mogo wajitume kufanya ufisadi kwa bidii ili wapunguze malalamiko na waache kuwasakama mafisadi papa? maana naona kama bado sijakuelewa vile.
Safi sana. Nini kifanyike ndilo swali muhimu hapa kama tunataka kujikomboa. Tunaenda kwenye uchaguzi wa viongozi. Kwanza watanzania tujitambue kwamba ufisadi sio sera ya kuwaendeleza watu wengi na sio sera ya Mwalimu Nyerere, imezaliwa Zanzibar baada ya kuua kabisa miiko ya uongozi ambapo aliyenacho anajiongezea wakati asiyenacho hata kidogo alichonacho ananyang'anywa. Tukijitambua tunajipanga kujikomboa. Msingi bora wa uongozi wa viongozi wetu uwe wananchi wenyewe ndo washike hatamu. Tufike mahali kwamba tunawaambia wanaotaka kutuongoza, kwamba tunataka 1,2,3,4,5.....yafanyike ndani ya miaka mitano kwa kuanzia na 1, kasha 2, kasha 3....wanapewa na muda wa kutimiza vipaumbele vyetu. Kwamba atakayeona hawezi anapigwa chini wakati wowote. Tukatae kuhongwa khanga na kofia na t-shirts na sigara. Msingi huo upo kwenye KATIBA iliyo wazi na iliyotungwa na sisi wenyewe kwa mtiririko tuutakao sisi kwa kuamini kwamba itatuongoza vizuri.

Sasa mafisadi walio na mitaji mikubwa ya kifisadi wametuzidi kete, wamesoma unyonge wetu na wana-maximize, wanajua sisi tutalalamika na kusahau. Wamefuta mawazo yote tuliyowaambia yawepo kwenye katiba mpya na wakajiwekea maneno laini yanayowakinga wao ili sisi tuendelee kuwa wanyonge lakini uzao wao uendelee kutanua kiuchumi kwa kututumia sisi. halafu wanakuja na lugha laghai iliyo tamu kama nyoka alivyomdanganya mama yetu Hawa mkewe Adam. madhara yake ni kama kilichoukuta uzao wa Adam na Hawa. Wanatuambia katiba pendekezwa ni nzuri kupita uzuri wa kawaida, wanatubembeleza tuseme NDIYO kuikubali. Sasa wale wanaotuambia mitego iliyomo tunaambiwa tuwapuze. Kumbe ukiona mtu anabembeleza sana akikuambia mazuri tu asikuambie na ubaya wa kitu hicho, ujue nyoka huyo anataka kukuangamiza kijanja kwa kuwa yeye amebahatika kushika mpini na wewe umeandamwa na makali ya upanga.

TUKATAE mpaka warudishe yale waliyofuta kwenye asimu ya pili. Kama vipi tukae upya na kuandika upya kwa utaratibu mwingine ambao hautawapa nafasi wapigadebe wa ufisadi,dilute all of them by simple calculation of representation. sio kujaza wanasiasa uchwara ambao bongo zao ni stereotyped kwa kutetea vyama badala ya uhalisia wa mambo. Tuwaunge mkono wanaokataa kamchezo ka kuangamiza nchi kwa kutumia nyadhifa zao, tutengeneze sera ya kitaifa (sio ya chama) ambayo chama kitakachoweza kuitekeleza kwa mafaniko kiseme kitafanyaje, tukikielewa tukipe nafasi, kikizubaa kipigwe chini based on the outcome sio kwa utaalam wa kuongea tu, hata nusu ya muhula tutakaowapa nafasi. Wajue kabisa havipendwi vyama au makundi bali watu mmoja mmoja kutegemeana na uwezo wake binafsi hata kama hana chama.

hayo ni machache sana labda utaweza kunielewa japo kidogo.
 
UNATIA HASIRA WANA WA INNJI HII.... unashanga anaepokea 500,000/= na anasavive!!
me napokea 120,000/ watoto 3 + mke, chumba kimoja, naishi kongowe kazi Tegeta na siku zinaenda
hiyo 500,000= sijawahi kuisikia kuiona. unatiana machungu tu. aghhhhhhrrrrrrrr!!!!!!!
teh teh teh teh teeeeeeh Nilikuwa namsemea mtu anayedaiwa analipwa vizuri zaidi mkuu, pole kwa hasira hiyo, najua kuna walio wengi ambao hata hiyo 120,000/- hawajawahi kuishika, hawajui hata 20,000 waipateje kupeleka watoto shule na wanapoomba huruma wanaambiwa BORA WASIZAE. Nilitarajia swali lako litakuja tu kwa namna Fulani. Asante kunisaidia. Wafanyakazi weng wanaopata 500,000 ni wale waliosoma sana kwa muda mrefu na vikwazo kupitiliza, wengine ndio wenye vyeo maofisini ambako wanayo dhamana juu ya vitu vyenye thamani ya mabilioni ya shilingi kama sio mamilioni lakin ati waendelee kuwa waaminifu tu. Nani anaweza kuwa mwaminifu kutunza ugali ilhali ana njaa kali na hajui familia itakula nini leo? Wanaojilipa sana ndio hao wanaotuambia tungejee kulipwa mbinguni, nadhani wenyewe wameshajua kwamba mbinguni hawatakiwi.
 
Back
Top Bottom