Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,289
Kamati
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA.
Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kuwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) itakutana katika kikao maalum cha dharura, kitakachofanyika kwa siku moja, Alhamisi, Novemba, 2019.
Kikao hicho kitakachojadili agenda maalum ya Taarifa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wa Mwaka 2019, kitaketi chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.15 ya Katiba ya Chama ya Mwaka 2006, Toleo la Mwaka 2016.
Baada ya kikao, Kamati Kuu ya Chama itakutana na Wabunge wote wa Chadema.
Imetolewa leo Jumatano, Novemba 6, 2019 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema.
=========Updates.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Chama leo Jijini Dodoma kujadili mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajika kufanyika tarehe Novemba 20, 2019.
Maamuzi ya Chadema Leo 07/11/2019,Chama kimejitoa kushiriki Uchaguzi huu wa Serekali za Mitaa,
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza chama hicho kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili.