Kamata kamata ya wabunge wa upinzani inatupeleka kubaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamata kamata ya wabunge wa upinzani inatupeleka kubaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jun 3, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  UBUNGE: ni nafasi ya kisiasa ya uwakilishi wa wananchi. Wabunge hupatikana kwa njia ya kupigiwa kura na wananchi katika majimbo yao kwa ajili ya kuwawakilisha katika vyombo vya kutunga sheria kama vile mabunge na mabaraza ya wawakilishi.
  Pia wabunge wana wajibu mwingine mkubwa wa kuisimamia serikali ili iiongoze nchi kadri ya matarajio yao.
  Hata hivyo, kutokana na kupanuka kwa demokrasia ya uwakilishi, siku hizi kuna wabunge wanaopatikana bila kuchaguliwa na wananchi katika majimbo yao. Wabunge wa aina hii ni wale wanaoyawakilisha makundi kadhaa ya jamii.
  Kundi la pili la wabunge wanaopatikana bila kuchaguliwa na wananchi linapatikana katika nchi za Kiafrika na limekuwa likipingwa hususani wabunge wa kuteuliwa na Rais kwa hoja kwamba hawana wanayemtetea bali aliyewateua, chama chake na serikali yake.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwaka jana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, wabunge kadhaa wa upinzani waliokuwa wakitetea nafasi zao walijikuta wakipata wakati mgumu katika mikutano yao ya kuomba kura. Mosi, baadhi yao, mikutano yao ya kampeni ilikuwa ikivurugwa na makundi ya wakereketwa bila polisi kuchukua hatua!
  Moja ya mkutano uliovurugwa ni wa John Shibuda wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika vurugu zilizosababisha kuuawa kwa mmoja wa wafuasi wa CCM. Shibuda alishikiliwa katika kituo cha polisi kwa takribani siku nzima kabla ya kuachiwa baada ya kubainika kuwa vurugu hizo zilisababishwa na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Cha kushangaza ni kuwa polisi walimkamata Shibuda, mgombea ambaye katika mkutano wake wa kampeni alitumia busara kuwatuliza na kuwsihi wafuasi wake wasiwashambulie vijana wa CCM ambao wanadaiwa kuwa waliuvamia mkutano wake!
  Na baada ya kubainika kuwa vurugu hizo hazikusababishwa na Shibuda, polisi hawakuchukua hatua yoyote ya kumuomba radhi kutokana na usumbufu alioupata.
  Mapema mwaka huu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), alikamatwa na polisi na kuachiliwa baadaye. Mbunge huyo alifunguliwa shitaka la kudaiwa kufanya vurugu katika kituo cha polisi na kumtorosha mfuasi wake aliyekuwa anashikiliwa katika kituo hicho mjini kigoma kwa tuhuma za kutoa matusi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
   
 3. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama wanavunja sheria za nchi hamna budi sheria ikachukua mkondo wake ipasavyo.pia jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama vinapasya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na taaluma yao ya kimsingi
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wiki iliyopita zilipatikana habari kwamba wajumbe sita wa baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), akiwemo mbunge wa Viti Maalum, Mangdalena Sakaya, walikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora, kwa madai ya kufanya mkutano na wananchi bila kibali.
  Viongozi hao walikamatwa wakati wakifuatilia mauaji ya rai ayaliyofanywa na polisi mkoa wa Tabora kutokana na mgogoro baina ya wananchi na hifadhi. Uongozi wa Jeshi la Polisi unadai kuwa viongozi hao na mbunge huyo waliingia na kukutana na wananchi bila mamlaka za serikali kujulishwa.
  Mara nyingi haki inapochelewa kutolewa kwa wanaoitafuta, waathirika hutumia njia nyingine. Kama wananchi wa Tabora wangesikilizwa na mamlaka husika katika kufikia mwafaka wa mgogoro wa kulisha mifugo katika eneo la hifadhi, wasingetoa taarifa hizo kwa CUF ili viongozi wake wawasaidie kupata suluhu.

  Sioni dhambi kwa viongozi wa CUF kuzungumza na wananchi wanaomiliki mifugo iliyochukuliwa na polisi kwa nguvu. Vyombo vya dola vilitakiwa kumshauri mbunge huyo wa CUF na viongozi wengine kutumia njia ambayo vingeona inafaa badala ya kukimbilia kuwakamata na kuwafungulia mashitaka huku wakinyimwa dhamana kwa sababu za hali tete!
   
 5. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Isipokuwa wabunge wa CCM, wengine wote hawana kinga ya kutokamatwa na polisi.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanaokamatwa si wabungw bali wavunja sheria. Ukitoa hao unaowaita wabunge ni wananchi wangapi wanaokamatwa kwa siku halafu hao wenye vivuli vya ubunge waichiwe tu hata kama wanamakosa. Labda cha kujadili hapa ni je waTz (wote bila kujali cheo chake) wanaokamatwa wanamakosa? we sijui ni great thinker wa wapi. labda chooni.
   
 7. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Red:rekebisha.
  Blue:nakuheshimu sana.
  Hakuna sehemu hata moja ambayo nimeongea maneno ya ovyo ovyo kama hayo ya blue,sasa sijui kati ya mimi na wewe ni nani ambaye yupo chooni///
   
 8. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tabia ya kuwakamata na kuwafungulia mashitaka wabunge wa upinzani ni kuwadhalilisha mbele ya jamii na wananchi wao wanaowawakilisha. Lakini Jeshi hilo likumbuke kuwa wananchi pia wana akili, na ninaona kama mara nyingi hawaridhiki na hivyo kuwa sababu ya kuichukia serikali yao.
  Jeshi la Polisi linapaswa kufuatilia historia ya mtukio yaliyopita na kutazama mbele. Bila shaka Jeshi letu la Polisi linakumbuka aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi la Kenya alivyoshiriki katika mauaji ya maelfu ya raia wa kushirikiana na Chama cha PNU cha Rais Mwai Kibaki baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
  Ofisa huyo leo hii ni mmoja wa watuhumiwa wa mauaji hayo wanaoshitakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini The Hague, nchini Uholanzi. Polisi wakae wakijua kuwa leo CCM iko madarakani lakini kesho chama cha upinzani kinaweza kutawala.
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  crap.....
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  ANNA MAKINDA, MIZENGO PINDA, LUKUVI, JANUARI.........na wavua magamba wengine kibao walichaguliwa na nani? mbona walipitishwa kibabe bila kupingwa?
   
 11. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Pia inachochewa na mfumo wa utawala tunaotumia sasahivi.
  Mbunge ambaye ndiye muwakilishi wa umma wa jimbo lake,
  Anakosa nguvu ya dola na mamlaka za kiutendaji wa moja kwa moja,
  Ndio maana inakuwa rahisi kudharaulika na viaskari ambavyo hata havina makazi
   
 12. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  inavyoonekana mbunge ni wa ccm, kwa sehemu wale wa tanzu za ccm, ila wa CDM ni wahalifu
   
Loading...