Kamanda Sirro: Bado tunamshikilia Vanessa Mdee

Kamanda Sirro: Bado tunamshikilia Vanessa Mdee

Yaani unamkamata mtu ukitegemea akwambie kama anatumia, anasambaza au vyote kwa pamoja?!!!
Huna intelligence ya kum-track umkamate ni ushahidi!!!!!!!
Huko CCP na KURASINI huwa wanafundishwa nini?
SIRO UNAKERA.
Kazi yao ni kukimbizana na wapinzani tu ndio wanaweza
 
Hili li dada linapepo juzi tu limedajwa alafu limerudia tena??
 
View attachment 479272

Kamanda Sirro: "Tunamshikilia msanii Vanessa Mdee toka jumatano ambaye taarifa zinaonyesha kuwa ni mtumiaji lakini pia ni msambazaji wa dawa za kulevya, tunaendelea na uchunguzi wetu na tukikamilisha uchunguzi wetu na ikathibitika kama ana kosa la kujibu basi, tutamfikisha mahakamani".

Chanzo: EATV

Huyu yuko na Jux hawezi kuwa salama hata siku moja, jamaa (Jux) atamteketeza muda si mrefu, si mliona alivyomsambaratisha demu wake kule China?. Ndugu wa Vanessa msaidieni ndugu yenu anapotea, madushe mbona yako mengi tu hapa mjini?
 
View attachment 479272

Kamanda Sirro: "Tunamshikilia msanii Vanessa Mdee toka jumatano ambaye taarifa zinaonyesha kuwa ni mtumiaji lakini pia ni msambazaji wa dawa za kulevya, tunaendelea na uchunguzi wetu na tukikamilisha uchunguzi wetu na ikathibitika kama ana kosa la kujibu basi, tutamfikisha mahakamani".

Chanzo: EATV
Na akikutwa hana hatia je?
 
Ni Taarifa isiyo na mashiko kwa umma kutoka Chombo cha juu cha usalama. Ni ujinga kusema tumemkamata kwa kutumia na kusambaza dawa za kulevya halafu unasema "lakini tunachunguza"!!!! Ni vema ungekaa kimya uitoe Taarifa baada ya uchunguzi.
Hii biashara ipo kwenye network.....wanaendelea kuchunguza ili wawatie wengine kambani
 
Na akikutwa hana hatia je?
Mie nilidhani busara ingekuwa kumhoji........ kumpima na kujiridhisha kama anatumia anauza anasambaza au la kisha kutangaza tumemshika anajihusisha na so and so............... au kwa sasa hatujathibitisha so and so.....
 
Nilishangaa sana huyu binti kujiita 'cash madame'...
 
Eti tunamshiikilia kwa kosa la kutumia na kusambaza madawa ya kulevya na ikidhibitika tutamfikisha mahakamani!
 
Hivi wanatumia Intelijensia ipi?! Kutaka sifa kwenye media tu.
 
Lakini kamishna si alipiga marufuku kukamata watu bila ushahidi?
Naona hapo kamanda Sirro anasema uchunguzi haujakamilika na kwamba wakithibitisha kuwa anajihusisha na madawa then ndo atapelekwa mahakamani!!
Swali linakuja, je wamemkamata na kumtangaza kwenye media kabla hawajathibitisha kwa nini?

Naona approach kama ile ile iliyotumika kipindi cha Makonda kabla kamishna hajateuliwa imeendelea tena leo!
Uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za watu.
Sidhani kama yeye alifurahi kutuhumiwa hadharani kupokea rushwa ya shisha.
 
Mie nilidhani busara ingekuwa kumhoji........ kumpima na kujiridhisha kama anatumia anauza anasambaza au la kisha kutangaza tumemshika anajihusisha na so and so............... au kwa sasa hatujathibitisha so and so.....
Udhaifu wa sheria na umbumbumbu wa wananchi juu ya haki zao vimeleta haya yote
 
Mtu kakamatwa tangu Jumatano na hii huenda ikaendelea hadi Monday na hapelekwi kokote ati uchunguzi unaendelea. Hivi kwani uchunguzi hauwezi kuendelea wakati mtu akiwa nje?

Kuna imposters wapo nje na kwa hali ilivyo inaonekana yanayosemwa ni kweli lakini hawaguswi. Culture of impunity slowly creeping in.
 
Yaani unamkamata mtu ukitegemea akwambie kama anatumia, anasambaza au vyote kwa pamoja?!!!
Huna intelligence ya kum-track umkamate ni ushahidi!!!!!!!
Huko CCP na KURASINI huwa wanafundishwa nini?
SIRO UNAKERA.
Na utakereka sana.Tanzania bila madawa inawezakana
 
View attachment 479272

Kamanda Sirro: "Tunamshikilia msanii Vanessa Mdee toka jumatano ambaye taarifa zinaonyesha kuwa ni mtumiaji lakini pia ni msambazaji wa dawa za kulevya, tunaendelea na uchunguzi wetu na tukikamilisha uchunguzi wetu na ikathibitika kama ana kosa la kujibu basi, tutamfikisha mahakamani".

Chanzo: EATV
Ikithibitika hana kosa je watamuomba msamaha au
 
Hivi Kamishna wa Madawa ya Kulevya amelichukuliaje hili suala?

Nakumbuka Waziri Mkuu alipiga marufuku kutangaza watu kwenye media mpaka ithibitike na ushahidi

Kamishna wa Kuzuia madawa pia akazungumza hivyohivyo

Sasa hii ya Vanessa je Kamanda Sirro amethibitisha na wana ushahidi wa kwamba ni Msambazaji?, au wametangaza kabla ya uchunguzi kukamilika?
 
Wanamakalisha mtu lumande zaidi ya masaa 24 kinyume cha sheria hivi sheria zetu zilitungwa kwa ajili ya nani?
 
Back
Top Bottom