Mamlaka yatangaza kutaifisha mali za watuhumiwa wa dawa za kulevya Zanzibar

Thabit Madai

Member
Oct 8, 2024
52
138
images (1).jpeg

MAMLAKA ya Kudhubiti na Kupambana na dawa za kulevya (ZDCE), imetangaza kutaifisha mali za watuhumiwa watatu wa dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 976 na kuwa na mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hatua imefikiwa baada ya Mamlaka hiyo kuendelea na operation maalum ya kuwakamata watuhumiwa wa mtandao haramu wa biashara haramu ya dawa za kulevya.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Migombani, Mkoa wa mini magharib Unguja,Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Kanal Burhan Zubeir Nassor amesema hatua hiyo imefanyika kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mwaka 2021 ya Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na Dawa ya kulevya Zanzibar.

3.jpg


Amesema, mali hizo zilizotaifishwa ni pamoja na Kiwanja kilichopo Matemwe na Honda ya aina ya Click, vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 422,126, Saleh Khamis Basmani Mkaazi wa Chukwani Wilaya ya Magharibi ‘B’ na Mke wake Dawari Abas Fakih ambapo Mamlaka inaendelea kuchunguza mali nyengine zilizomo ndani na nje ya Nchi.

Aidha amemtaja Mtuhumiwa mwengine kuwa ni Mohamed Abdalla Juma Mkaazi wa Michenzani Wilaya ya Mjini ambae ni Mtumishi wa Serikali katika Kada ya Sheria ambapo ametaifishwa Kiwanja kilichopo Bweleo Wilaya ya Magharibi B, chenye thamani ya Sh. Milioni 35 baada ya kubainika anashirikiana na Saleh Khamis Basmani katika utakatishaji wa fedha na kuingiza Simu zinazotumika kufanya uhalifu kutoka Nchini Afghanistan.
2.jpg


Hata hivyo amesema Mamlaka imetaifisha Gari aina ya Toyota na Nyumba zilizopo Paje Wilaya ya Kusini, zinazomilikiwa na Andrea Scoph Fres, Raia wa Ujerumani, zenye thamani ya Sh. Milioni 518,926 mara baada ya kukamatwa na Mashine ya kisasa ya kuoteshea Bangi, Polo moja la Bangi pamoja na Shamba la Bangi huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

1.jpg


Mbali na hayo Kanal Burhan amesema Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na Dawa za kulevya inaendelea kuwatafuta wanaojishughulisha na Dawa hizo ili kunusuru Vijana na utumiaji wa Dawa hizo.
3.jpg


Itakumbukwa mnamo Aprili 22, 2024 Mamlaka hiyo ilitangaza kutaifisha mali haramu ya Dawa ya kulevya ya Saleh Khamis Basman, Mkaazi wa Chukwani na Mke wake Dawari Fakih zenye thamani ya Tsh Bilion 15.3.

6.jpg

7.jpg
 
Back
Top Bottom