Kamanda mawazo kuongoza moto wa m4c igoma-mwanza 2/1/2013 .

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
227
Ndiyo Wakuu , heshima kwenu ! Baada ya Kamanda Mawazo kuichakaza CCM Kwimba , wiki hii 2/1/2013 ata ongozana na Makamanda wa M4C kanda ya Ziwa kuwasha moto Igoma Jijini Mwanza. Ikumbukwe kuwa kata ya Igoma imekuwa kwenye sintofahamu kubwa baada ya Diwani wa kata hiyo Ndgu Adam Chagulani kuvuliwa uanachama na kamati kuu kwa tuhuma za kukihujumu chama cha CDM hapa Mwanza. Baada ya kuvuliwa udiwani yeye na Henry Matata walikwenda kupinga uamzi huo Mahakamani. Kwa hiyo mkutano huo ni mwendelezo wa kufikisha dhima pana ya vuguvugu la mabadiliko i.e M4C kwa Wananchi wote . Pia Mkutano huo umelenga kukemea na kulaani hujuma zinazo ratibiwa na kuendeshwa na CCM za kuwanunua vijana Wa Cdm ambao ki msingi wameonekana kuwa ni wachumia tumbo na Wapiga dili tofauti na wao wanavyo jitangaza kwenye vyombo vya Uchwara kwamba wao ni Wazalendo na Wana uchungu na nchi hii. Nape na Mwigulu chini ya ccm wanatakiwa wanunue dawa na vitanda hospitalini, madawati na vitabu, wajenge madarasa, waongeze mishahara ya walimu, madaktari na polisi, watoe mikopo kwa dada zetu wanaojiuza vyuo vikuu kwa sababu ya njaa, wapeleke misaada wa chakula ngorongoro watu wanakufa njaa na wala si kuhangaika na vijana hawa ambao serikali ya ccm imewanyima ajira. MY TAKE :- SISI SOTE NI NDUGU, ADUI YETU NI CCM.
 
hao waliokihujumu cdm wasipewe nafasi kabisa tunataka ukombozi na sio wachache wachumia tumbo
 
Ndiyo Wakuu, Heshima kwenu!

Kama nilivyo post thread hii jana ni kuwa kesho tarehe 2/1/2013 , Kamanda Mawazo kwa kushirikiana na Makamanda viongozi na Waratibu wa M4C kanda ya Ziwa watapiga mkutano wa hadhara kata ya Igoma-jijini Mwanza utakao anza kuanzia saa 9 mchana .

Kwa taarifa nilizo pata toka kwa Kamanda NICKY mpiganaji wa ukweli toka Igoma ni kuwa Mkutano huo umeandaliwa na wananchi wenyewe wa Igoma baada ya kuchangishana wao kwa wao kwa shilingi mia,miambili,miatatu na kuendelea kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo.

Vile vile kamanda NICKY akadokeza kuwa mbali na makamanda hao wa M4C, atakuwepo na Kamanda Adrian Tizeba ,diwani kata ya Lugata -Sengerema alie vua gamba na kuvaa gwanda tangu mwaka jana.

MY TAKE :- SISI SOTE NI NDUGU, LAKINI ADUI YETU NI CCM. TUSIPO CHUKUA HATUA DHIDI YAKE, BASI NI WAZI KUWA SISI TUTAKUWA SEHEMU YA TATIZO. M4C NEVER STOP,TWANGA KOTE KOTE MPAKA KIELEWEKE.
 
kama kawaida tutakuwepo pale kuanzia saa 7 mwajiri wangu Jiji mtanisamehe sana maana ntaenda kupata hoja za makamanda wenye uchungu na nchi yao siyo hii yakina Kabwe na wenzake anatunyanyasa tu hapa jiji hatupumui ila anaiba ile mbaya.
 
Umesomeka sana mkuu...huyo NICKY nimemsika sana wana Igoma wanamwitaji nasikia ni kijana wa hapo hapo igoma...babu yake alishawahi kuwa diwani wa CCM miaka ya nyuma....mama yake nae alikiua diwani wa CCM viti maalum badae akagombea kata ya Buswelu..pia Mzee wake alikua Mwenyekiti wa CCM Kata ya Igoma CCM 2007-2012...

DOGO NASIKIA NI MFANYAKAZI WA Serikali....pia ni msomi wa mambo ya Utawala na Uongozi...Chagulani amewazalau sana wana igoma kwa kujiitamsomi na kuwapora mali zao wananchi mchana mchana...jembe hili ndo mkombozi mya wa igoma na uzuri liko CHADEMA
 
Tunahitaji vijana kama hao wenye moyo na dhamira ya dhati ya kupigania mabadiliko ya kweli kama ni kweli kijana katoka katika familia yote CCM ila akaamua kuchagua chama makini kinachowapigania watanzania CDM hii ndio spirit tuitakayo na sio vijana wanaoweza kununulika virahisi na kutumika kama kondom bravo guys aluta continua
 
MAWAZO alikuwa diwani ccm kata ya Sombetini Arusha, alivua gamba na kuvaa gwanda tangu mwaka jana. Kwa takribani miezi 7 ameji hidhirisha kuwa kamanda mpiganaji wa ukweli kwani kazi yake na nguvu zake vime onekana dhahiri katika ujenzi wa chama na vugu vugu la mabadiliko (M4C) maeneo mbalimbali ya Tanzani.

WATANZANIA TUSHIRIKIANE KUUSAMBARATISHA MTAMBO WA ANALOGIA (CCM ) NA KUUIMARISHA MTAMBO WA DIGITALI (CDM) KWA NGUVU ZETU,AKILI ZETU NA MIOYO YETU.
 
Kwa antiM4C hapo (chagulani) jiandaen kukabiliana na hujuma.

Igoma tunaijua wana Igoma kamanda Chagulani mwenyewe anakaa Mahina kama km 5 kutoka Igoma ila upepo mdogo wetu aliuchezea vibaya. Hapa ni AMANI tu Karibu kamanda Mawazo kwa Makamanda kama kina GEORGE KAYEGO huyu jamaa anafanya shughuli za Bodaboda hapa Igoma ila ni mwanaharakati mzuri sana na ndo makamanda wetu.
 
Ndiyo Wakuu , heshima kwenu!

Juzi kamanda Mawazo na Makamanda wengine wa M4C walifanya mkutano Wilayani Nyang'wale, Geita katika kijiji cha Ibambila. Lakini katika hali isiyo kuwa ya kawaida, mamia ya waombolezaji kijijini hapo walimzuia Mawazo na msafara wake asiendelee na safari yake kuelekea eneo ambalo mkutano ulikuwa ume endaliwa.

Hali ilijitokeza baada ya Mawazo na Makamanda kushiriki kutoa rambirambi katika msiba huo huku akilaani udhaifu wa serikali ya CCM katika utoaji wa huduma mbovu kwa wananchi masikini watanzania wakati vigogo wakiugua mafua na magonjwa ya zinaa wanapanda ndege kwenda kutibiwa India na Afrika ya kusini.

Pia aliwaambia waombolezaji hao kuwa vifo vingi vya watanzania katu si mipango ya Mungu ,bali ni mipango ya CCM ( MWENYEZI MUNGU ANATOA ,CCM WANATWAA ). Hivyo wakati waombolezaji hao wakiendelea kumzinga, ali wasihi warejee msibani na akawa ahidi kwamba atapanga siku nyingine rasmi kuja kusalimia. J

ana Mawazo aliongoza amsha amsha katika mji wa Kisesa nje kidogo jijini Mwanza na kesho ataongozana na Makamanda wa M4C Kanda ya Ziwa katika mkutano wa hadhara Kata ya Igoma kwenye viwanja vya stand ambapo mkutano huu unavuta hisia nyingi sana kwa wakazi wa jiji la Mwanza kutokana na sintofahamu ya madiwani wa CHADEMA-Mwanza.

MY TAKE :- WAUNGWANA WANASEMA " SIKU MJINGA AKIJITAMBUA, MWELEVU YUPO MATATANI ." Watanzani wengi wa vijijini ambao zamani walikuwa mtaji wa CCM leo wanajua fika kuwa adui yao mkubwa aliewafikisha hapa ni CCM.
 
Nimeipenda hii ya Mungu anatoa CCM wanatwaa!!!!Nawakubali makamanda maana wapo makini kama beki ya italy katika kuwakabili masalia!
 
Back
Top Bottom