Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kwanza mnajifanya kuguswa na kifo cha Mawazo wakati mlikuwa mkimhisia kauza chama kule Geita. Inawezekana nyinyi wenyewe ndio mmemshughulikia kwa hasira za kushindwa kwenye uchaguzi ili mpate sympathy kutoka kwa wananchi. Acheni uhuni wenu. Chacha Wangwe alikufa hivihivi mpaka leo kifo chake kina utata? Hakuna majibu, ni Kwa hisia kuwa viongozi wa chadema walishughulikia hili. Tupeni majibu kwanza ya kifo chake then turukie hili la Mawazo. Mungu amrehemu., R.I.P
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.

Kwa hiyo mwananchi akitenda kosa anapigwa na kuuawa kwa mashoka na watu kukimbia au?!
 
Baada ya kusikia ama kuona taarifa za tukio hili jana niliumia sana. Ila taarifa hii yako Lema imenisononesa sana zaid kwa kweli!

Watu wana hubiri amani kwenye vyombo vya habari, ofisini, makaisani, misikini, majukwaani lakini baadhi yao wakitoka hapo wanaenda kupanga minu ovu dhidi ya yale wanayo yahubiri!

Hali hii ya kutoa uhai wa mtu itakoma lini? Nani wa kutusaidia Tanzania kukomesha tabia na mipango hii? USA? France? ???

Nani wa kuwasemea watanzania jamani? Nani wa kutetea na kulinda haki ya Mtanzania??????
 
Ndo zake huyo ! Redio za Arusha zote zinaogopa kumpa 'live air time' maana anaweza kukutia kwenye matatizo usiyoyategemea !
Hachagui maneno, hana busara, hana subira na ni mpenda uchochezi.
Lema ana dalili zote za uhalifu !
Lema sio mchochezi, anaongea ukweli, ila nadhani kwenye kipindi hiki anatakiwa kuwa careful kwasababu some of his words may need justification, na uchaguzi wake bado

Mauaji ya Mawazo ni choreographed
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.
......Wewe unaishi nje ya nchi Mkuu?Kwani hukuona visa vingi ktk uchaguzi ulioisha hivi majuzi?Huu ni muendelezo tu..
 
Kamanda Mawazo kauawa na Polisi na inajulikana,najiuliza hivi hawa Polisi wetu ni Watanzania?na kama ni Watanzania wanapigania nini?nasema wazi watatumaliza wote ili wabaki wenyewe,lakini kabla hawajatumaliza haki itachukua mkondo wake na ndipo Taifa langu Tanzania litainuka kutoka kwenye mavumbi,Mungu M;laze pema Kaka yangu Kamanda Mawazo!

Unakurupukaga sana wewe yaani wewe ni bendera fuata upepo, Jana ulisema kapigwa na wana CCM leo umesikia lema kasema ni polisi wamehusika na wewe umedandia!....nakushauri fanya tafiti jizoeshe kusoma ili uje na misimamo yako
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.

So, kulingana na fikra zako, mwananchi akitenda kosa anapaswa kutekwa, kupigwa na kuuawa???
 
Kaka ushawahi kuhudhuria mikutano ya Kamanda Mawazo?
Geita hakukuwa na CHADEMA yenye nguvu hadi alipokuja Kamanda Mawazo. Alitumia hadi usafiri wa baiskeli kueneza elimu ya uanachama. Hotuba zake ukihudhuria huwezi kuwa mwana CCM tena. Kifo chake ni sherehe kubwa kwa wanyonyaji wa Taifa hili. Kaka nashangaa sana pamoja na kuiamini zaidi CHADEMA baada ya ujio wa Lowassa lakini imekuwa bubu kwa mambo nyeti sana kama haya.

Chadema ni chama cha siasa na hakuna watakatifu huko wengine ni wazinifu na majambazi. Ndio maana walimuingiza Lowassa kundini bila ya aibu
 
Godbless J Lema natambua kama ilivyo kwa wengi wewe pia umeguswa sana na kifo cha Alphonce Mawazo hivyo naomba nitoe pole kwako na kwa wengine wote. Lakini, kwako Lema, unapaswa kuwa makini sana mwanangu na matamko uyatoayo kwani ghalama yake unaweza ukashindwa kuilipa.

Kama madai yako yatakua na ukweli basi elewa kuwa hapo mlengwa hakuwa Mawazo nali wewe. Mawazo ilikua ni kete tu ambayo wataalam wa saikolojia ya mwanadam walijua ikichezwa ile kete tu, basi wewe utakuwa triggered na kulipuka. Ni kama draft unapewa kete, unakulwa watu wanakupiga double mpaka King (tamka kingi).

Ulihitaji sana msaada wa kusheria kabla ya kutoa madai yako. Kama siyi msimamo wa wana Arusha basi leo hii ungekua umekighalimu cha chako ila kwasababu ya msimamo wao basi wasiwasi wangu ni sijui kama utarudi bungeni, maana kauli zako ndiyo zitatumika dhidi yako katika kipindi hiki na na kama ujuavyo Arusha inahitajika kwa namna yoyote ile 'dead or alive'. Msipuuze sana nguvu ya wapinzani wenu maana wapo tayari kutumia ushauri wowote ule ili mradi ushindi upatikane.

Mbatia alimtaka mgombea wa CUF ajitoe, mimi ninashauri asijitoe, abaki kama backup. Nikirudi kwa Lema jaribu sana kuepuka kuwa too emotional ingawa kwa uliyoyaandika yamesomeka na sidhani kama yatafutika
 
Kuna siku inakuja tujipe moyo wakuu tutauupigania uhuru wetu kwa namna yoyote pole lema na familia ya Alfonse Mawazo
 
Watoe tamko gani? Viongozi hawa wana busara na hawakurupuki kama unavyotaka.

Kutokea kifo cha Mwangosi,Chacha wangwe, Dr Mvungi ,mauaji soweto na wao wakisema wana mkanda mzima jinsi polisi walivyohusika lakini mpaka sasa hakuna walilolifanya na hiki kifo cha Alphonce pia ni polisi hao hao wanahusishwa ,ni busara ipi unayo iongelea ?????
 
Back
Top Bottom