Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

uzuni na simanzi kwa wanaarusha na wana chadema wote kwa uumla, aliyoyasema Lema ni maneno yenye Ekima na Busara,najua wapo watu wanaofuraia yaliyotendeka lakini muda si mrefu nao watasikitika kitachoelekea baadae ni kila wakati kundi moja kusikitika na kundi la pili kufurai kama mambo haya hayatakemewa na viongozi wa nchi na waliousika kuchukuliwa hatua kali, lakini ukimya wa tukio hili itapelekea kuwa na misiba kila wakati kwa pande zote mbili zilizojengwa na polisi
 
Mawazo alitaka kukata rufaa kupinga matokeo, nafikiri kuna aliyemkwamisha, na amefanikiwa, tungeanzia hapa
 
Ni masikitiko sana kupoteza binadamu ambaye nchi bado inahitaji mchango wake.

Mungu akuweke pema peponi Kamanda Mawazo.

Nashangaa umeanza kutoa tuhuma mapema kabla hata ya uchunguzi haujafanyika. Nadhani Mtu ambaye aliwahi kuwa Mbunge atakuwa anafahamu maana ya sheria.


Na wewe Lema ni kati ya wanasiasa wanaosaidia wauwaji wasifahamike na waendelee kuwepo mitaani!

Kama mmoja wa viongozi wa CHADEMA walivyoueleza ulimwengu, kwa sasa una mkanda ambao unaonyesha watu waliofanya mauwaji katika mkutano Arusha kwenye viwanja vya Soweto! Kinachoshangaza na kusikitisha ni kuendelea kukaa na mkanda wa video badala ya kuvipa vyombo vya habari ili vihabarishe dunia kuhusu wauwaji hao kwa sababu kuna uwezekano wanaendelea kufanya maovu wakati una mkanda unaonyesha sura zao.

Inaeleweka Vyombo vya habari ni muhimili mwingine wa nchi na taasisi zake zinafanya kazi kubwa ya kuelimisha na kupasha habari. Nchi kama Uingereza wananchi wanatumia vyombo vya habari kama BBC kuhabarisha jamii kuhusu watenda maovu walionaswa kwenye video (Crimewatch).

Kama hamuwezi kuwapa polisi/serikali huo mkanda, vipeni vyombo vya habari ili viwafichue watenda maovu.

Kuna familia mpaka sasa hazifahamu kilichotokea mpaka kupotelewa na ndugu, jamaa na marafiki. Kwa familia hizi kufahamu nani aliyetenda maovu ni njia ya kuponya makovu ya masikitiko.

Maisha ya binadamu ni zaidi ya siasa. Hata kuwafahamu kwa sura wauwaji ni moja ya justice kwa familia. Wapeni haki ndugu, jamaa na marafiki.

Ulichoandika ni kama umekatwa kichwa vile....hiv tangu lini ikawa kaz ya lema kukamata wahalifu ...na wakati huohuo jeshi la polisiblina watuvwanaolipwa kwajili hiyo...?? Mwisho kabisa masharti ya kutoa mkanada ni iundwe tumehuru yabkijaji ...serekali haitaki...je nan apelekewe....huo mkanda...???
 
una ushahidi gani kuwa kauwawa na polisi?
Mihemko ya kisiasa isiwajae mpaka kufikia kukosa uelewa. Huyo lema hajawahi wala hatokuja kuwa kitu kimoja na polisi kwasababu tangu zaman inajulikana alikuwa jambaz sugu
wewe si unaushaidi wa Lema kuwa jambazi? kwanini asishitakiwe akafungwa? mkubwa ebu elimika kidogo!, nafikiri hata shule ya kata umefika!
 
Uhai wa mtu ni thamani kubwa sana maishani na hakuna mwenye haki ya kuuondoa zaidi ya Mwenyezi Mungu. Kamanda mawazo ameondoka akiwa kwenye harakati za kutafuta haki ya msingi. Mungu akulaze mahali pema peponi. Amin

Lakini kwa jicho la pili, kuna watanzania wenzetu kila siku wanauliwa kwa namna moja au nyingine na ni jamii tulizomo ndizo zimekuwa zikifanya hivyo tunaona, tunapuuzia bila kuchukua hatua kisheria. Mwisho wa siku mazoea huzaa tabia, na tabia ikikolea huzaa mazoea na mazoea huzaa kawaida hicho ndicho kilichopo leo watu wameshaona mauaji ni kitu cha kawaida.

Haijalishi ni nani ameuawa iwe awe ni mtu mwenye umaarufu ktk jamii au asiye na umaarufu wowote yote kwa yote mbele za Mungu binadamu wote ni sawa.

Yanayotokea leo ni dalili ya mazoea. Najua kila msiba ni maumivu ktk familia au jamii husika lakini nitoe wito kwa wanasiasa, wanaharakati na wananchi kwa ujumla turudi kwenye misingi ya kuthamini utu na ubinadamu.

Wanasiasa chungeni sana kauli zenu mnapokuwa kwenye majukwaa ya kisiasa kwani kwa kiasi kikubwa ndiyo chanzo kikuu cha matukio mbalimbali tunayoshuhudia leo. Haijalishi ni chama gani iwe CCM, CDM,TLP, CUF, nk wote mnatakiwa kujitathmini juu ya siasa chafu mnazofanya ambazo ndizo zinapelekea watu kujenga hisia za mihemko.

Wenye uwezo wa kufanya tathmini bila kuingiza unazi wa kisiasa mtakuwa mmenielewa.

Binadamu wote ni sawa, tupige vite ukatili baina yetu

Kundi lako ni moja na baadhi ya maaskofu wanafiki. Wakitendwa ccm mara moja mnaibuka kukemea kwa kutaja majina ya vyama. wakitendwa wapinzani mnajificha kwenye suala la Amani. unafiki mtupu! sema waziwazi nani anahusika na kifanyike nini...suala la siasa za majukwaani na kuchunga ndimi ndiyo matokeo yake haya
 
atakuwa kauawa na wahalifu,halafu watu wanaingiza siasa,ndo maana hawataki kueleza hasa kimetokea nini

Hivi lumumba fc...mmesahau kunasheria ya mitandao..ya kukandamiza watu...polis ndo wanao paswa kutoa maelezo ya nn kilitokea
 
Alikuwa kijana aliyeamini katika Mabadiliko , alitembea Nchi nzima kwa shida kujenga ufahamu kuhusu Ukweli ,Haki na Usawa . Ameuwawa akiwa akitoka kwenye kazi za Chama chake ,akavamiwa , akapigwa na baadae kufariki . Ni nani amefanya kitendo hiki ?

Watu wengi mnalaumu Wanachama wa ccm kwani ndio waliofanya kazi hiyo , hapana, mnakosea . Mawazo ameuwawa na mfumo wa Serikali na Jeshi la polisi unaojali ukatili na uovu . Mauaji yataendelea sana , kwani wengi wamekishauwawa na kuumizwa bila Serikali kuchukua hatua .

Polisi wanaowajibika kwa utawala unaojali ukatili ,ubaya,na uovu ni lazima watamsaidia Shetani kufanya kazi . Polisi wanaoshindwa kukamata wahalifu na na kuwajibisha wahalifu , wao ndio wanaosaidia Taifa hili kuingia Vitani, Matukio ya Green guard kuvamia na kujeruhi na hata kuua ni mengi katika Taifa hili, Wahalifu wanalindwa na sasa wana ujasiri wa kufanya wanavyotaka . Sioni siku nyingi za Amani Tanzania , magari ya kuwasha na silaha za moto zitashindwa kupambana na Umma uliojawa hasira na Uchungu, propaganda pia zitashidwa kutengeneza hali ya usalama , masikitiko yangu ni kuwa hali hii itamkuta kila Mtu aidha ni mwenye haki au ni asiye na haki. Usalama wa Nchi haujengwi na wingi wa silaha wala wingi wa Askari , Isipokuwa utawala unaojali Haki na Usawa .

Uhalifu wa namna hii katika Taifa hili unajengwa na Polisi walioshindwa kazi zao kwa kuzingatia Uadilifu na Sheria za kazi , Kamati za Siasa za Chama Tawala ndio zinatoa maelekezo ya utendaji wa Jeshi la Polisi . Kwa mfano hapa Arusha Rpc ni mdau namba moja wa ccm na hivi karibuni katika vikao vyake vya kampeni ya kumsaidia mgombea Ubunge wa ccm alichokaa na Viongozi wa boda boda alitoa maelekezo mabaya na ya uharibifu dhidi yangu , unafikiri nini ? Ni lazima Vijana hawa kama watakosa Utu , wanaweza kufanya uhalifu mbaya sana kwangu , kwani anayepaswa kulinda amani ndiye anayesimamia Mipango mibaya ya uhalifu .

Mambo haya ni lazima yafike mwisho . Polisi mnapaswa kuwa na hekima sasa na mtambue kuwa hali ya Usalama Nchini haiko salama , Watoto wenu ,Wazazi wenu , Wake zenu , na Familia zenu ziko Mitaani , Ukatili na Uonevu unapoongezeka kwa Watu wanyonge , ndivyo hivyo Watu hawa wanaanza kufikiria njia mbadala ya kujitetea , naona Binadamu wa Tanzania anaanza kuelekea huko .

Ni nani anafuata baada ya Mawazo ? Ni vita ya kujilinda au kukubali kuwa Maiti kwa njia ya mapanga na vipigo ? Tulitafakari jambo hili wote , kwani Utulivu huu tulionao hauna muda mrefu kutoweka na ndipo Nchi yetu itakuwa Nchi ya Ukiwa.

Moyo wangu umeumia na kuchoka sana nahitaji msaada zaidi , Ni Kijana rafiki mzuri niliyemuingiza kwenye Siasa , nilimpa Suruali , Mkanda, na Koti wakati ninampleka kumtambulisha kwa ajili ya kura za maoni kwenye Chama cha Tlp wakati huo , tuliishi wote na familia zetu zikapendana sana , hakuwahi kuwa mnafiki juu ya anachokipigania .

Mawazo umeuwawa ? Kosa lako ni kuwa Chadema na kufanya Siasa ? Mkuu wa Wilaya ya Geita atafurahi sasa , kwani alishawahi kutamani kuona maiti yako na leo ameshuhudia ,Rafiki zako tunatafakari kwa kina na Uchungu mkubwa .

Ni heri Vita inayotafuta Haki na Usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha Utu wa Binadamu.

Nilikuwa nakupenda sana Mawazo .

Godbless Jonathan Lema

binafsi nimeumia sana nanimekuwa nikiumizwa mno na aina ya matukio ya kinyama nawapo watu viongoz wa ccm mfano mabina,katibu mwenez kahama , kule nzega wakati fulan aliuawa kiongoz wa ccm leo mkiti mkoa wa geita chadema mie natofautina kidogo nawewe kuwa polis ndo chanzo hapana bali ninyi viongoz mnaosimama majukwaani na kutia hamasa na kuwafanya watu wajiamin nakuona polis silolote hasa wewe huwa unakauli fulan za mlengo wa hamasa ya vulugu kwa vijana ninakumbukumbu nyingi sana za kauli zako ambazo nadhan zinaweza kuwa mchango wa haya yanayotokea leo unakumbuka ulivyokuwa uwanja wa furahisha ukimshambulia mlugo na hamasa ulizotoa lakin kesho yake bariadi ulivyokuwa ukiwapa hamasa vijana juu ya kubeba visu mawe na fimbo wakati wa kwenda kupiga kura na kulinda kura kumbuka ulivyokuwa ukisema haya upande wapili nao walichukua hatua dhidi ya kile ulichokimwaga pale
naomba nihitimishe kwa kusema hivi ninyi viongoz wa juu na wenye mvuto wa siasa nchi hii please badiriken vingine Taifa letu mtaliingiza kwenye vita nimeumia sana kwa kifo cha huyu kiongoz nilimsikiliza mara kadhas kwenye mikutano alikuwa akijenga hoja vizur zikileta hisia kubwa mno na kuwasisimua watu kwani alikuwa anaeleza historia yatulikotoka na sasa alikuwa rafiki wa mdogo wangu katibu wa baraza lavijana geita wa chadema inauma mno lakin naonya kauli zako na za pinda na za akina nape mziache zinagharimu maisha ya watu wengi sana
 
Tatizo mnapenda kulialia ili muonewe huruma ilhali na nyie ni wale wale tu.Mbona vijana wa Red Brigade walivyomtesa Kagenzi na yule mwandishi wa habari tena kwenye ofisi za makao makuu ya chama hamkuandika hizi hekaya za kulaumu jeshi la polisi?Acheni unafiki karma afanye kazi yake barabara.Huo uzi mliwapongeza sana hao RB,leo yako wapi sasa?CALM DOWN,KARMA IS AT WORK.
 
Pamoja na kwamba nimesikitishwa na kifo cha kikatili cha ndugu Mawazo lakini sikubaliani na hii tabia ya kupeana tuhuma. Wananchi wengi tunahisi huenda kifo cha mawazo kimesababishwa na mgogoro wa dhulma humo humo ndani ya CHADEMA; Wengine wanasema huenda ni migogoro binafsi kati yake na jamaa zake. CHADEMA mnasema kifo chake kimepelekewa na green guard kumvamia marehemu na wengine mnasema polisi ndio wamemuua. Sasa tushike lipi!?

Aidha, mbona kifo cha Chacha Wangwe hatukuona watu kuguswa hivi!? Wakati kilijaa giza zito na hadi leo haieleweki nini kimemuua Chacha Wangwe. Ndugu Lema kama unajua kuhusu Wangwe tugusie kidogo. Huenda ikatoa mwanga wa kujua kuhusu kifo cha Mawazo. Natazama kwa jicho la tatu tu.

RIP Mawazo

naona unajitahidi kuizima mada kuleta nyingine, tunalijadili hili kwanzaaa
 
mkoa wa geita unaijumuisha chato anakotokea Magufuli, Mawazo aliwapeperusha sana kwenye kampeni kiasi kilichowapoteza kwenye msitari, nafikiri mjadala ungeebdelea hapo
 
Polisi wepi unaozungumzia kufanya kazi kwa weledi? Hivi Lema katamka hayo wanamsagia meno wanatamani na yeye... Wako wapi watu mbalimbali waliouawa siku za nyuma? polisi haikuwepo? unategemea hapakazi tu atajali jambo hilo ili mradi si "mwenzetu" aliyeguswa? Kama kweli hapa kazi tu anataka ajitanabaishe mbali na utawala mbovu aanze na hilo na aunde tume huru ya uchunguzi wa masuala yote hayo tangu akina Mwangosi, Kibanda na wengine...vinginevyo tutaamini "hapa kazi tu kufanya vyote tuvitakavyo kwani hakuna atakayethubutu kutugusa"

Ni bahati mbaya sana kuwa na mtazamo kama wako juu ya jeshi la police,
najua hata wewe Leo hii ikitokea ukadhulumiwa haki yako kituo chako cha kwanza ni jeshi la police ili kudai haki yako.

Kwa nini ktkt hili unatutaka tushindwe kuliamini jeshi la police?

NAAMINI JESHI LA POLICE LITAFANYA KAZI YAKE VIZULI NA KWA WERED ULIOTUKUKA
NA KUWAZIBA MIDOMO WOTE WENYE MTAZAMO KAMA WAKO.
 
Laiti kama mods wangekua wanafanya kazi zao hapa jukwaani bila ya kuwa biased, kuna mambo yangejulikana na kufumuliwa mapema kupitia JF.
Kuna thread niliwahi kuileta humu ndani kipindi kile cha kampeni nikielezea namna nilivyojitokeza kumuokoa kijana mmoja pale Mwanza ambaye alishambuliwa na 'Vijana wa CCM'. Nilieleza kuwa kwa jinsi walivyomshambulia yule jamaa na na kumdhibiti, wale watu walionekana hawakua raia wakawaida, hata kwa muonekano wao ingawa walivaa mavazi ya CCM. Lakini nilipoipandisha hapa JF Mods waliinyofoa haraka sana habari ile.
 
Dah...vifo vya maalbino navyo vingewauma watu kiasi kama hiki ningeelewa kweli watu wanauchungu na wanachukia uonevu,lakini ajabu vifo vya kisiasa ndiyo vimekuwa na nguvu hadi kuamua nao kulipiza.

Kweli siasa na dini vimefanywa kuwa vitu ndiyo vyenye kuleta matatizo ulimwenguni.
 
Wamempora ushindi wa Ubunge, hawakuridhika Jana wakamua kumkatisha maisha yake kikatili sana.

Pumzika kwa amani kamanda mpambanaji Mawazo.
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.

Naamini katika utawala wa haki na sheria. Hata kama alitenda kosa, Je kuna kosa gani, uhalali gani wa kuweza kumuadhibu mtu yeyote mkosaji kwa njia hii?
Kama alitenda kosa wauaji walipaswa kuchukua hatua za kumpeleka kwenye vyombo vya sheria. Siku zote tunshimizwa kutokujichukulia sheria mkononi.
So waliofanikisha mauaji haya watabaki kuwa wauaji tu. Hawana haki ya kutoa uhai wa mtu.
 
Kundi lako ni moja na baadhi ya maaskofu wanafiki. Wakitendwa ccm mara moja mnaibuka kukemea kwa kutaja majina ya vyama. wakitendwa wapinzani mnajificha kwenye suala la Amani. unafiki mtupu! sema waziwazi nani anahusika na kifanyike nini...suala la siasa za majukwaani na kuchunga ndimi ndiyo matokeo yake haya

Hata NZI japo anakula kinyesi lakini ana akili ndo maana akikuona anakimbia
 
Mbona wachaga hawauawi? Kaeni mbali na Kundi hili la CHADEMA! Yatawamaliza yana hasira za kushindwa uchaguzi!
 
Kamanda Mawazo kauawa na Polisi na inajulikana,najiuliza hivi hawa Polisi wetu ni Watanzania?na kama ni Watanzania wanapigania nini?nasema wazi watatumaliza wote ili wabaki wenyewe,lakini kabla hawajatumaliza haki itachukua mkondo wake na ndipo Taifa langu Tanzania litainuka kutoka kwenye mavumbi,Mungu M;laze pema Kaka yangu Kamanda Mawazo!

Umeshuhudia ameuwawa na polisi?
 
Back
Top Bottom