Kamanda Kamuhunda awageuka wakubwa...

Kamanda Kamuhunda awageuka wakubwa...

Napita tu, lakini Mungu mwenye uweza wote atayadhihirisha yote yalinyuma ya pazia, siku yaja.
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, akiojiwa kamanda kamuhunda kuhusu kifo cha mwangosi alisema “Kazi yetu ni kutekeleza majukumu na maagizo tu na mimi niliyafanya hayo yote.”.

Kamhanda! Hivi unataka kuniambia mtu akikutuma nenda kamtukane mama yako matusi ya nguoni utakwenda na kumwambia ........."Mama fulani kanituma eti nikutukane Ku.............! Je, sio kwamba utakuwa umemtukana wewe mwenyewe?? Hebu jaribu kutoa majibu kama KAMANDA WA POLISI.
 
Utaumia kichwa ukiuliza elimu za maaskari, hata matendo yao yameshakupa picha ya elimu na uwezo wao.
Hata mauaji ya kupewa maagizo wameshindwa kuyafanya kuvuruga ushahidi!! Sikiliza kauli za makamanda wengi utagundua wengi ni zero brain
Nilishapewa siri ya Makamanda wa mikoa(RPCs} kuwa ni rejected officers. Kwa sababu hiyo wamekuwa maroboti ya JK. Ukifuatilia kwa makini utagundua hilo, ndiyo maana hakuna TAMKO la serikali juu ya mauaji yote yaliyokwisha tokea. Muulize Vincent Nyerere kwa nini alikatazwa kusoma kipengele cha mauaji haya kwenye hotuba yake pale mjengoni kwenye kikao cha bajeti!
 
Hivi ni sahihi kwa mtu kuvunja sheria za nchi kwa madai kuwa anatekeleza maagizo toka kwa kiongozi mwingine?

Atakapofika kule ICC atajitetea nani alimtuma na kwanini alitumwa kufanya mauwaji wakati akijuwa kuishi ni haki

yalazima
kwa kila kiumbe anayeitwa mwanadamu anaeishi kwa amani na kufuata sheria.


Kamuhanda aache kuchachawa na wenzie akina andengenye na shilogile wajiandae.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kamuhanda haendi kwene vikao vya harusi hadi saa saba usiku jamani???
 
Kamuhanda haendi kwene vikao vya harusi hadi saa saba usiku jamani???
nakuapia huyu jamaa atakufa kifo kibaya kuliko kile cha Barlow na Mwangosi... Na mwili wake hautaonekana... Nipe muda, kuwa na subira.
 
nakuapia huyu jamaa atakufa kifo kibaya kuliko kile cha Barlow na Mwangosi... Na mwili wake hautaonekana... Nipe muda, kuwa na subira.
Na asipo tubu laana itaendelea mpaka kwa vizazi vinavyofuata katika uzao wake
 
Utatumikaje kama robot au ndio kutaka maendeleo kusiko kuwa na elimu? ina maana akili yake hakujua alichokuwa anakifanya?
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, akiojiwa kamanda kamuhunda kuhusu kifo cha mwangosi alisema “Kazi yetu ni kutekeleza majukumu na maagizo tu na mimi niliyafanya hayo yote.”

Unaona, ngoma hiyo ameshaanza kuwatumia salamu waliomtuma ki aina kwamba alikuwa anatekeleza maagizo yao waliomtuma, hii inaweza kutoa jawabu la kwanini JK amekaa mbali sana na issue Mwangosi hasa kuhusiana na kitendo chake cha kukataakatakata kuunda tume huru ya uchunguzi.

Kkuhusu mengine amezungumzia kuwa gari lake lilikuwa mbali na eneo la tukio na kwamba polisi ilibidi watumie nguvu kujitetea kwani walirushiwa mawe na raia.

Yaani sijui Kamuhanda kama anajua kuwa kuna kitu kinaitwa video ambayo haisemi uongo pengine hajui kuwa tukio zima liko kwny youtube hata kipofu anaona kuwa hakuna jiwe lilorushwa na raia.

Katika kumbukumbu zangu mikutano aliyofanya na waandishi wa habari siku hiyo kabla ya tukio na kauli kadhaa baada ya tukio alieleza kuwa anatekeleza maagizo kutoka kwa wakubwa wake, jaribu kuwa na kumbukumbu, kuna wakati nilikusudia kuanzisha uzi wa kauli hiyo ya Kamuhanda hapa.

Si jambo la kawaida RPC awepo kwenda tukio dogo kama lile la kufungua tawi kijijini, kuna sughuli nzito iliyokusudiwa kufanywa siku hiyo. Wenye kusoma hali hiyo waliishaiona mapema na ndio maana walitoa tahadhari kwa Dr. Slaa asiende huko kwenye tukio kwani aliyekudiwa wa siku hiyo huenda si Mwangosi, pale walimalizia hasira baada ya kumkosa waliyemdhamilia.

Hata polisi waliokuwepo pale hata Mkuu wa kituo cha Mafinga huenda alikuwa gizani, na polisi wa kuchomekewa walioandaliwa kwa shughuli maalum kufanya mauaji hayo. Niwape dondoo moja hapa chini:

Katika riporti ya uchunguzi iliyotolewa na Baraza la habari na Jukwaa la wahariri Tanzania, imeeleza kwa kina tukio hilo na kwamba polisi walipomzingira Mwangosi huku wakiendelea kumteremshia kipigo, OCD Mwampamba akifanya jitihada za kumwokoa, Kamanda Chamuhanda alipiga honi ya gari lake na mara kishondo cha bomu kikasikika kilichomwua Daud Mwangosi.


Kwa tukio hilo ni kwamba Kamuhanda ndiye aliyeamrisha bomu lipigwe, kuna aliyeandaliwa kwa kazi hiyo ndiyo maana honi ile ilikuwa amri ya kuashiria kufanya kilichokusudiwa.
 
Kamuhanda, Kamuhanda!!! Damu ya Mwangosi itakusuta wewe na kizazi chako chote!!
 
ni AIBU kwa askari kama wewe kusema hadharani kwamba ulikuwa unafuata amri zawakubwa ni dhahiri askarimkokama MBWA kazi ni kufuata amri zamabwana wenu
 
Hii ndio shida ya kupanda cheo kutokana na UKADA wa CCM pamoja na UTII wa Amri za WAKUU. Huyu kamanda hana elimu, hajui sheria na ni mkereketwa. Damu ya mwanadamu haimwagiki bure
 
Excuse ya 'kutii sheria' walitumia maaskari wa Third Reich ya Hitler Ujerumani baada ya vita, lkn haukukubalika...
 
Kamuhanda...will not forget him.. hata Ocampo sasa anamfahamu huyu jamaa
 
Kuna maswali ningependa kujua kuhusu Kamuhanga,
1.0 Hivi anafanya kazi kwa mkataba au bado yupo under 60yrs ndani ya Jeshi la Polisi.
2.0 Elimu yake au CV yake general kwa mwenye kumjua zaidi????
Kazi hizi hazihitaji elimu kubwa saana hapa Tz tofauti na ulaya! Kwanza hapa ukiwa msomi ni adui kwa wenzio,
Cha msingi uwe na psychomoter damain njema umefuzu!
 
Back
Top Bottom