Kamanda Kamuhunda awageuka wakubwa...

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, akiojiwa kamanda kamuhunda kuhusu kifo cha mwangosi alisema "Kazi yetu ni kutekeleza majukumu na maagizo tu na mimi niliyafanya hayo yote."

Unaona, ngoma hiyo ameshaanza kuwatumia salamu waliomtuma ki aina kwamba alikuwa anatekeleza maagizo yao waliomtuma, hii inaweza kutoa jawabu la kwanini JK amekaa mbali sana na issue Mwangosi hasa kuhusiana na kitendo chake cha kukataakatakata kuunda tume huru ya uchunguzi.

Kkuhusu mengine amezungumzia kuwa gari lake lilikuwa mbali na eneo la tukio na kwamba polisi ilibidi watumie nguvu kujitetea kwani walirushiwa mawe na raia.

Yaani sijui Kamuhanda kama anajua kuwa kuna kitu kinaitwa video ambayo haisemi uongo pengine hajui kuwa tukio zima liko kwny youtube hata kipofu anaona kuwa hakuna jiwe lilorushwa na raia.
 
Acha wageukane. Kamuhanda kila anapotembea roho inamuuma sema hamjui tu. Ata aliyemtuma anamuona mjinga maana asingefanya kwa sataili ile. Na yeye tunamtumia wa kutoka Mwanza kwa Barrow wakamshughulikie
 
Damu isiyokuwa na hatia inapomwagika, itamuumiza mmwagaji daima. Ni vigumu sana kila aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika mauaji ya Mwangozi kupata amani moyoni. Itafika mahali yote yatawekwa peupe.
 
Mkuu wala usipate shida kuwaza ya kamhanda kwa sababu akili za magamba haziamini hata kama watanzania wana uelewa wa kuchambua mambo,hawaamini hata kama watu wana uwezo wa kuangalia matukio kwenye tv na mitandao kwa sababu falsafa yao ni "wanyime elimu ili uwatawale" wameshashindwa siku nyingi hakika.
 
Kamuhanda ameshachanganyikiwa naamini mzimu wa mwangosi unamtokea usiku na hapati usingizi, kwa wataalamu wa saikolojia wanelewa Muda si mrefu mzee Huyu ataanza kutembea bila viatu, Nguo na mwisho atawehuka kabisa, malipo ni hapa hapa duniani, wapi Liberatus .
 
Kama angekuwa amefanya kwa utashi wake siku nyingi angekuwa hana kazi, ila jamaa alikuwa anatekeleza maagizo ya mabosi wake tu..
 
Kuna maswali ningependa kujua kuhusu Kamuhanga,
1.0 Hivi anafanya kazi kwa mkataba au bado yupo under 60yrs ndani ya Jeshi la Polisi.
2.0 Elimu yake au CV yake general kwa mwenye kumjua zaidi????
 
Kuna maswali ningependa kujua kuhusu Kamuhanga,
1.0 Hivi anafanya kazi kwa mkataba au bado yupo under 60yrs ndani ya Jeshi la Polisi.
2.0 Elimu yake au CV yake general kwa mwenye kumjua zaidi????

Utaumia kichwa ukiuliza elimu za maaskari, hata matendo yao yameshakupa picha ya elimu na uwezo wao.
Hata mauaji ya kupewa maagizo wameshindwa kuyafanya kuvuruga ushahidi!! Sikiliza kauli za makamanda wengi utagundua wengi ni zero brain
 
Kuna maswali ningependa kujua kuhusu Kamuhanga,
1.0 Hivi anafanya kazi kwa mkataba au bado yupo under 60yrs ndani ya Jeshi la Polisi.
2.0 Elimu yake au CV yake general kwa mwenye kumjua zaidi????

bahati mbaya sana polisi hawafanyi kazi kwa kutumia elimu bali ni amri hata kama kitu aki make sense lazima
utekeleze agizo la mkubwa wako no matter wapi ni kazi moja ya ajabu sana.
 
Ukitaka kujua kasoro ya askari wa Bongo hebu safiri nje ya nchi uende kwa mfano Uingereza au Marekani. Nilishangaa sana, kumbe askari kumshika maungoni mhalifu ni kwa procedure maalumu. Approach ya askari wa Marekani kweli ni ya askari, hawana papara na wako very reasonable, nadhani mafunzo wanayopitia ni special haswa. Hawa wa hapa kwetu yaani kabla hajajua hata wewe ni nani anaweza akakutia kirungu halafu akaomba samahani kumbe sio wewe.
 
Wamemuua wakadhani wanamkomoa, mwenzao sasa amelala usingizi wa milele,hasikii maumivu wala uchungu wa maisha wao wapo macho wanahangaika na shida za dunia siku si nyingi nao watatamani wafe, damu ya Mwangosi haiwezi kukauka pale ilpomwagika bila haki kutendeka ni kiasi cha muda tu hata kama wanaichelewesha, taratibu wanaanza kuropoka na kunyoosheana vidole mwisho watararuana wenyewe kwa wenyewe.......Pumzika kwa amani Mwangosi raha ya milele Mungu akuangazie.
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, akiojiwa kamanda kamuhunda kuhusu kifo cha mwangosi alisema "Kazi yetu ni kutekeleza majukumu na maagizo tu na mimi niliyafanya hayo yote."

Unaona, ngoma hiyo ameshaanza kuwatumia salamu waliomtuma ki aina kwamba alikuwa anatekeleza maagizo yao waliomtuma, hii inaweza kutoa jawabu la kwanini JK amekaa mbali sana na issue Mwangosi hasa kuhusiana na kitendo chake cha kukataakatakata kuunda tume huru ya uchunguzi.

Kkuhusu mengine amezungumzia kuwa gari lake lilikuwa mbali na eneo la tukio na kwamba polisi ilibidi watumie nguvu kujitetea kwani walirushiwa mawe na raia.

Yaani sijui Kamuhanda kama anajua kuwa kuna kitu kinaitwa video ambayo haisemi uongo pengine hajui kuwa tukio zima liko kwny youtube hata kipofu anaona kuwa hakuna jiwe lilorushwa na raia.
Anatafuta huruma kwa watu,amefanya kazi kizembe na kwa sifa,ingekuwa ni mtoto wake angeweza kumlipua kiasi kile?Ni mnafiki tu huyu Mzee!
 
Hivi ni sahihi kwa mtu kuvunja sheria za nchi kwa madai kuwa anatekeleza maagizo toka kwa kiongozi mwingine?
 
Kamuhanda ameshachanganyikiwa naamini mzimu wa mwangosi unamtokea usiku na hapati usingizi, kwa wataalamu wa saikolojia wanelewa Muda si mrefu mzee Huyu ataanza kutembea bila viatu, Nguo na mwisho atawehuka kabisa, malipo ni hapa hapa duniani, wapi Liberatus .
Sijui huyu Kamuhanda ana roho ya namna gani? Alivyoshuhudia Mwangosi akichanwa chanwa na kulundikwa mithili ya mbwa aliyegongwa na gari barabarani na bado anabisha kilichotokea!!! IDDI AMIN Dada alikuwa bora kuliko Huyu KAMUHANDA
 
hakika wakuu wake wanahusika masimulizi ya huko nyuma yanasema askari wengine walitoka dodoma.kama hilo ni kweli basi kamanda wa iringa hawezi kukusanya askari mikoa mingine bila makao makuu kushiriki
 
Naona kapata hofu baada ya kuskia ishu imeenda hadi kwa Ocampo so anajua warrant inadondoka wakati wowote akamatwe
 
Back
Top Bottom