Kama wewe ni programmer wa aina yoyote ingia hapa

Kama wewe ni programmer wa aina yoyote ingia hapa

Sidhani kama hio ni approach nzuri kujifunza programming cause programming naina very logical Na sidhani kama kuna Language inaisha hasa hizi C/C++ inabidi tufanye utafiti why most institute hapa kwetu zinaavoid C++ kama introductory language, but naona nje wamechagua Python(Practically can do almost everything).., my opinion
 
Kama alivyokushauri mdao hapo juu, wewe hujasoma na kumaliza C++, aisei kaka C++ ni mnyama mkubwa, ni jitu. Hauwezi kuimaliza, komaa nayo kabisa utengeneze system ya nguvu. Unachofaa kufanya, tumia muda wako kusoma principles za systems development, fanya mazoezi na hiyo C++ hadi kieleweke.

Usirudie makosa niliyoyafanya ya kusoma lugha nyingi nikitapa tapa, yaani baada ye kuelewa syntax halafu najiamiisha kwamba nimeimaliza na kuruka kwa nyingine. Nilizipitia lugha zaidi ya ishirini na hatimaye nikajikuta sina chochote, na wala sina uwezo wa kuandika software yoyote kuanzia mwanzo hadi mwisho. Ilinichukua miaka kujirekebisha kwa kuanza upya.

Unafaa utafakari ni system ipi unafaa kutengeneza, angalia kwenye jamii baadhi ya changamoto zilizopo, halafu anza na system analysis, fuatia design, halafu piga codes ukitumia hiyo hiyo C++ yaani komaa nayo kabisa, hakikisha umeelewa mambo ya ndani tena kwa kina. Tumia muda wako mwingi humo hadi watu wakuone chizi fulani vile, na hatimaye ibuka na system, ikiwezekana shirikiana na wadau katika kufanya tests, pitia online forums.

Baada ya hapo itakua rahisi kujifunza lugha zingine.

Lakini narudia kusema, ni muhimu sana kuhakikisha umeelewa programming principles, ingia kabisa kwenye basics, elewa data type kwa undani. Hii ni mojwapo wa kile huwa kinanitamausha na vijana wengi wanoingia kwenye taasisi hii. Unakuta jamaa kweli yupo anaweza kutengeza software maana zipo tools nyingi zinazorahisisha kazi, lakini hawana uelewa wa ndani wa nini kinachofanyika.
 
Back
Top Bottom