Mkuu ukiwa unafikiria language ni vizuri kujua language ipi ina fanya vizuri wapi, language nyingi unaweza kuajiriwa kama umezimaster vizuri. Ukiongelea popularity hakuna language inayoshinda Javascript since inatumika kwenye websites client side na toka 2006 inatumika server side kwa framework inaitwa Node.js ambayo ni very powerful. Ila pamoja na huo u-popular, haimaanishi ni language nzuri kwa kila kitu, mfano kutengeneza app kama ya google maps vile, naongelea calculations zinazofanyika backend, achana na unachokiona kwenye website juu juu, huwezi enda na Javascript kabisa kwa kua mbali na kua slow ina some limitations ambazo zinafanya kazi hiyo kua ngumu, ndio maana wanabaki kutumia language kama C++, C au Java kwa kua zina very high performance.
Cha muhimu ni kujua language ipi itumike kwenye nini, kujua language unaweza jua nyingi tu very quick, tatizo ni kujua programming, programming its not about language, its about mastering the logic, ukipewa tatizo uweze kuligawanya na kuhakikisha unali-solve efficiently and very fast. Ndio maana mtu anayesoma mfano Computer science chuoni hatokutana na language miaka yote minne, atakutana na Algorithms, datastructures, data mining techniques, hardware design, computer vision, artificial intelligence, zote hizi ni courses zinazofundisha techniques zinazotumika ambazo ukizijua unaweza kaa ukaanza kutengeneza AI kwa kutumia language yoyote unayojisikia na ikafanya kazi.
Kuanza na java sio mbaya, unaweza endelea nayo, hata hivyo kama utapenda mobile development Java ndio inatumika kwenye android so una uwanja mpana, ila usijilimit language moja, soma angalau languages tatu nne, Javascript iwekemo. Ila cha muhimu kuliko vyote ni master programming and not programming languages.