Kama wewe ni mwanaume hii itakusaidia

Kama wewe ni mwanaume hii itakusaidia

Lotus 123

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
3,151
Reaction score
5,534
Kwenye mchezo wa kandanda kinachohitajika na kupata pointi tatu muhimu, hii ni muhimu Sana, haitajilishi unashinda hyo mechi Kwa goli 1, 2, 3au goli 4 muhimu ni kupata point tatu haijalishi utachezea uwanja wa nyumbani au ugenini.

Jambo muhimu ni kupata alama tatu. Ni vizuri uwe na mikakati imara itakayokuwezesha kupata alama tatu muhimu, usije kusema ndani ya dakika tisini nilimiliki mpiga na kupiga chenga lakini sikushinda, kinachotakiwa na alama tatu, visingizio vya uwanja ulikuwa na maji haifai kitu, hakikisha umefanya mazoezi ya kutosha, na beki zinakaba vizuri, pia hakikisha unafahamu vizuri counter attack na offside trick.

Ushindi ni ushindi hata kama ni wa goli moja.
 
Sawa ila ushindi unapendeza zikiwa goli tatu na kuendelea mbili mara mojamoja bao moja ni hatari sana utaambiwa umebahatisha,goli moja halina dhamana kabisa.
 
Kweli MKuu, muhimu Point Tatu. Ila Ukishinda hakikisha unashinda Goli zaidi ya Tatu ili kuweka Heshima kwa Timu Pinzani. Huu Uzi huu
 
Kwani mechi yenyewe ni nani na nani,? usijekuta ni hii ya kesho kutwa Yanga vs Simba 😅😅😅...yaani aliyelala chini ni yanga ,mwanaume lazima utashindwa tu
 
Back
Top Bottom