KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Sidhani kuwa kuna wakati wowote ambapo chama kiliwahi kukuhitaji kama ilivyo kwa wakati huu.
Pengine utakuwa na sababu zako maalum zilizokufanya uwe mwanachama wa chama hicho, lakini hata kama sababu mojawapo si kwa sababu ya chama chako kusimamia HAKI, UHURU na DEMOKRASIA, bila shaka wajibu huu (mpya? wa chama chako haukuondolei mapenzi kwa chama hicho.
Katibu Mkuu John Mnyika katika taarifa yake hivi karibuni, alitaja "wajibu" alionao mwanachama wa chama hicho, ikiwa ni pamoja na "kukilinda dhidi ya mahasimu wake.
Nyote sasa, mnaelewa barabara kwamba chama chenu hakitakiwi kuwepo.
Kama wewe ni mwanachama wa CHADEMA, kuna sababu ipi zaidi ya kukilinda chama chako kisipotee?
Unaweza usiwe tayari kuitikia wito wa viongozi wako katika kushiriki katika baadhi ya mambo yanayoandaliwa na chama ili kuonyesha ulimwengu kwamba chama kina wanachama wanaokijali na wapo tayari kukilinda chama chao, lakini kama mwanachama, kweli utakosa kushiriki hata katika jambo moja tu la kuonyesha ujali wako kwa chama chako?
Kwani CHADEMA inao wanachama wangapi?
Hata milioni moja inatosha kabisa kwa wanachama kiasi hicho kuionyesha dunia kwamba chama chao hakiwezi kuchezewa..., siyo kwa kuvunja sheria, lakini kushiriki ndani ya sheria zilizopo, kumzuia SIRRO kujifanya kwamba yeye ndiye mwenye haki ya kuamua hatma ya nchi hii.
Kama wewe ni mTanzania, hata kama ni mwanachama wa CCM, anayejali hatma ya Tanzania yetu, hata wewe unao wajibu wa kukataa nchi yetu kuvurugwa na hawa viongozi waliokosa mwelekeo.
Hutakubali kukaa kimya na kujifanya yanayotokea wewe hayakuhusu. Wote yanatuhusu. Ni lazima tushiriki kwa njia mbalimbali kuwaonyesha hawa viongozi wetu kwamba wanayofanya sasa yanavuka mipaka, tuyakatae. SIRRO na jeshi lake lenye mitutu hawezi kudharau sauti zetu tukikataa upuuzi anaofanya.
Sisi wengine wote, tunaweza tusiwe na mapenzi yoyote na Chama cha CHADEMA, lakini uTanzania wetu pekee unatosha, tukatae kuvurugwa kwa HAKI ndani ya nchi yetu.
Tushiriki kadri tunavyoweza kuwazuia viongozi wakandamizaji wa haki bila kujali ni nani anayenyimwa haki yake.
Siyo lazima tuwe kwenye mikusanyiko ya CHADEMA, lakini kuna njia nyingi sana za kuwaunga mkono katika juhudi za kukataa uonevu.
Kazi hii itakuwa nyepesi tukishiriki kwa pamoja katika njia mbalimbali za kuunga mkono juhudi hizo. CHADEMA watachambua na kuzieleza njia hizo za wananchi wa makundi mbalimbali wanazoweza kushiriki katika mchango wao wa kuondoa ukandamizaji Tanzania.
Nimetirirka tu, kama kuna makosa, sahihisha.