Kama washauri wenyewe wa Chadema ndio hawa...

Kama washauri wenyewe wa Chadema ndio hawa...

Yours is a dull party. There are million ways of doing politics in Tanzania. The problem is dwarfism facing your party together with it entire leadership, which is conversant with only one way of doing politics in the country. The non-committal political campaign. Does your party have permanent qualifies personnel, office infrastructure, active party organisation machinery,? And if not why? The reason is obvious. Mbowe's inner motive is more focussing on making money than leading the party to victory. That is the real compromise factor. Try dissecting your party to know this and perhaps more.

Hiki kingereza cha Chahali hiki. Kaona aje kizungu zaidi kuonesha hisia zake
 
Kwa kimombo neo tija ni productivity. Hapa ulikolitumia na ulivyolitumia siko na siyo! Umeharibu kabisa maudhui na mtririko wa kimantiki wa Makala yako.

Chahali kwa nini usitumie tu account yako unahanganika kujificha huku? Hivi arguments za kutumia "kimombo" kama nyundo ya hoja zako zinajulikana. Kama maana ya "jita" ni "productivity" tatizo liko wapi? Kwani ulioyandika na mengine kwingine huwa unalenga yalete nini?
 
Kupata taarifa kwa TISS ya sasa not easy like that braza. Kitengo kwa sasa kina endeshwa kwa weledi na uzalendo. Wataishia kupata tetesi zisizo na uhalisia. Weewe unasikia hata siku izi Siri za vikao vya state house au vikao vikuu vya chama zinavuja kama zamani. Mambo yamebadilika sana na kiukweli nimeiamini ule msemo kuwa mtu mmoja anaweza kubadilisha mambo kabisa.
Kama kupotezwa kwa watu...kuzuia isijulikane zilipo 1.5t ndio uzalendo sawa
 
Chahali analysis yako ni very poor! Nilikuwa nakuamini sana katika haya mambo. Kumbe na wewe ni wale wale. Unasahau kuwa CDM is dealing with a BRUTAL DICTATOR in all senses. How do you deal with someone using a gun, police, army to silence opossition and not HOJA kupambana na upinzania? Unapambanaje na Dikiteita ambaye hata vikao vya ndani amevikataza, viongozi wote wanabambikiwa kesi? Mahakama compromised??? (kwa kiasi fulani CJ aliingilia siasa kidogo) .Ruhusu CDM iende kwa watu iwahubirie kinachoendelea uone kama haitaungwa mkono. Unapambanaje na Idd Amin, Kim Jong Un , Kagame ,,, (Diane Rwigima) , Museveni and the like. Nadhani umenielewa Evarist Chahali

Mpinzania wa Kagame ashitakiwa kwa kosa la uasi

By Rashid Bugi -

View attachment 823222

Mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.

Ameshtakiwa pamoja na mama yake mzazi aitwae Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.
Diane Rwigara aluzuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti nchini Rwanda ambapo rais Kagame alishinda kwa kishindo.
Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kuikuwa na udanganyifu madai yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.
Diane Rwigara pia ameshtakiwa kwa kubuni stakabadhi bandia.
Wachunguzi wanadai kuwa Bi Rwigara alivunja sheria za uchaguzi kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono ugombeaji wake.
Haijulikani ni kitu gani kilichangia afunguliwe mashtaka ya kuchochea uasi nchini humo pamona na ndugu zake.
Chahali wakusamehewa tu. Yeye na wenzie wameinjia Jiwe liwepo pale kwakuwa wanajua wameingiza watanzania matatizoni anajaribu kujivua lawama kwa kuangushia mzigo wengine
 
Zinawezekana sana. Unadhani operatives wote wa TISS wanapenda yanayoendelea? Hata na wao pia wanafamilia, wanaishi uraiani kama sisi.
Kama una bisha, Mange anapataje habari za humo ndani? Lissu alikuwa anazipataje?

Sema tu sasa hiv chama hakina watu wenye ushawishi tena. So wale operative wa TISS hawana imani kabisa nao hata kama wakiwavujishia habari.

kuna uwezekano wote waliokuwepo awali wame "lay low" kucheki upepo unavumaje huku wakivuta pumzi namna ya kurudi
 
Kupata taarifa kwa TISS ya sasa not easy like that braza. Kitengo kwa sasa kina endeshwa kwa weledi na uzalendo. Wataishia kupata tetesi zisizo na uhalisia. Weewe unasikia hata siku izi Siri za vikao vya state house au vikao vikuu vya chama zinavuja kama zamani. Mambo yamebadilika sana na kiukweli nimeiamini ule msemo kuwa mtu mmoja anaweza kubadilisha mambo kabisa.
HAPANA hii si kweli na ndio maana hata kina Lema waliweza bashiri hama hama hii miezi mitatu kabla hayajaanza wangejuaje?? Hata lisu alishajua kuna mpango wa kumuua miezi miwili kabla and so did saanane na gari lilelile linalomfuatilia ndilo linatajwa kuhusika sasa lisu angejuaje bila watu wa TISS kumtonya?? Vipi nyaraka za bombarider kushikiliwa???

Alafu kingine hayo ya kusema hakuna watu wa kuaminika si kweli maana sielewi kivp TISS wasiiamini CHADEMA alafu wakaiamini CCM ambayo kwenye wizi wa makinikia,almasi,tanzanite na madudu ya sheria za gesi kati ya waliohusika 90% ni makada wa CCM unaweza nipa sababu why TISS wawaamini CCM na so CHADEMA??? What has changed since 2015?? Kama shida ni lowassa je ana uongozi kwenye chama?? Mbona alipokuwa CCM alikuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwanni wamuamini akiwa CCM na akija upinzani asiaminike??

Mimi labda niseme tu ni kweli naweza kukubali kuwa madiwani na wabunge hawanunuliwi ila tuwe realistic kwa aina ya siasa za sasa hivi mbunge gani wa upinzani atarudi bungeni 2020?? Ni lazima wajisalimishe ili walinde viti vyao maana wanajua kinachoamua uwe mbunge sio tena sanduku la kura bali maelekezo kutoka lumumba je hata bila kununuliwa nani atabaki CHADEMA??

Hivyo Evarist Chahali kama ni kushauri ungesuggest mbowe atafute namna kusolve udikteta uliopo ili awarudishie confidence viongozi wake kuwa ushindi upo 2020 ila kusema compromising information na blah blah zingine cjui dk slaa hazina mashiko maana CCM hata kama hawana compromising information yeyote si wanaweza kwa mfano forge confession ya mwanachadema mmoja mahakamani ili adai kuwa alitumwa na viongozi wa chadema ili kumuua chacha wangwe au lissu hapo hapo mbowe au waitara au kalanga et al si bado wanaweza kuhukumiwa kunyongwa bila hta kuwa blackmailed wahamie CCM ili wafichiwe maovu yao!! Na majimbo yatabaki wazi na CCM watashinda kwa kishindo why walazimishe wakati kuna option B ya kuwatoa??

Na kingine kama wangeingia kwa blackmail ya kutishiwa hakuna angeruhusu wapewe ubunge tena ilihali wanajua wamekuja kwa shingo upande maana wataingia kwenye vikao vya chama pia vikao nyeti vya kiusalama n.k unless ungesema wajiuzulu siasa hapo sawa mimi naamini wanaingia CCM kwa mapenzi yao either ya pesa au vyeo ila sio kwa kulazimishwa hilo nakataa kwa SAUTI.

Labda niseme tu nahuzunika sana kuona mtanziko wa kisiasa uliopo lawama zinaenda upinzani yaani ni sawa na kuwalaumu besigye wa uganda au Diane Rwagira wa Rwanda eti wanakosa inteligentsia kupambana na madikteta does it make sense hivi hata Dr slaa angefanyeje kwa mfano mbele ya magufuli si angeshapigwa risasi na kupotezwa kma saanane na mawazo!!! Simple like that.....kma lissu aliyewapa upinzani hamasa ndio huyo kazawadiwa magazine ya SMG je Mbowe au mpinzani gani anao uwezo wa kupambana na chamadola (isomeke RISASI)?? Dr slaa??

Shida ni kubwa kuliko mnavyochangia kwa kuangalia upande mmoja humu ukitaka kuona hili... Leo magufuli amalize muda wake aje mama samia.... kwa udhaifu huu huu unaodai wa mbowe/intelligence ya chama n.k utashangaa CHADEMA inapaa zaidi sababu nini?? Chanzo kimeng'olewa

Embu tujikite kwenye chanzo

Cc chige Malcom Lumumba Pascal Mayalla tindo JokaKuu
 
Yours is a dull party. There are million ways of doing politics in Tanzania. The problem is dwarfism facing your party together with its entire leadership, which is conversant with only one way/approach of doing politics in the country - the non-committal non accountable political campaign. Does your party have permanent qualified personnel, office infrastructure (including live internet connectivity), active party organisation machinery, et la? And if not why? The reason is obvious. Mbowe's inner motive is more of focussing on making money than leading the party to victory. That is the real compromise factor your party and members altogether must endure. Try dissecting your party to know this and perhaps more maladies it has compromised.
Rubbish!
 
Nimesikitishwa mno na uchambuzi wa mtoa hoja,yaani kama middle class huyu anaongea hivi basi tumekwisha ,maana yule mkazi wa hapa Lingusenguse ambaye hajaona darasa,hana social netsworks kama hizi tunazotumia sisi(na mbaya zaidi ndio wengi ndani ya nchi yetu) nilitegemea uchambuzi wako uwe wa kweli uliojaa facts,level field ya kisiasa hapa nchini kwa sasa haipo sawa,huyu Docta uliyemtaja aliiongoza CDM kipindi hali ya kisiasa ilikuwa much moderate kuliko sasa,TISS ni idara ya chama tawala s haiku pale kuangalia usalama wa nchi au kumshauri our no1 kuhusu maswala mengi tu ndio maana teuzi zake nyingi tu zinabadilishwa kila wakati,ila yote yana mwisho jirani zetu ZIM kumeshakucha came next week wana Rais mpya na yeyote anayeshinda uchaguzi huu ZIM will NEVER BE THE SAME AGAIN;uchambuzi wako umejaa woga,unafiki,na kujikomba kwa watawala ambao unafikiria watatawala milele no,nchi hii belong to all of us sio ya wateule wachache who are having a big portion of a pie.
 
HAPANA hii si kweli na ndio maana hata kina Lema waliweza bashiri hama hama hii miezi mitatu kabla hayajaanza wangejuaje?? Hata lisu alishajua kuna mpango wa kumuua miezi miwili kabla and so did saanane na gari lilelile linalomfuatilia ndilo linatajwa kuhusika sasa lisu angejuaje bila watu wa TISS kumtonya?? Vipi nyaraka za bombarider kushikiliwa???

Alafu kingine hayo ya kusema hakuna watu wa kuaminika si kweli maana sielewi kivp TISS wasiiamini CHADEMA alafu wakaiamini CCM ambayo kwenye wizi wa makinikia,almasi,tanzanite na madudu ya sheria za gesi kati ya waliohusika 90% ni makada wa CCM unaweza nipa sababu why TISS wawaamini CCM na so CHADEMA??? What has changed since 2015?? Kama shida ni lowassa je ana uongozi kwenye chama?? Mbona alipokuwa CCM alikuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwanni wamuamini akiwa CCM na akija upinzani asiaminike??

Mimi labda niseme tu ni kweli naweza kukubali kuwa madiwani na wabunge hawanunuliwi ila tuwe realistic kwa aina ya siasa za sasa hivi mbunge gani wa upinzani atarudi bungeni 2020?? Ni lazima wajisalimishe ili walinde viti vyao maana wanajua kinachoamua uwe mbunge sio tena sanduku la kura bali maelekezo kutoka lumumba je hata bila kununuliwa nani atabaki CHADEMA??

Hivyo Evarist Chahali kama ni kushauri ungesuggest mbowe atafute namna kusolve udikteta uliopo ili awarudishie confidence viongozi wake kuwa ushindi upo 2020 ila kusema compromising information na blah blah zingine cjui dk slaa hazina mashiko maana CCM hata kama hawana compromising information yeyote si wanaweza kwa mfano forge confession ya mwanachadema mmoja mahakamani ili adai kuwa alitumwa na viongozi wa chadema ili kumuua chacha wangwe au lissu hapo hapo mbowe au waitara au kalanga et al si bado wanaweza kuhukumiwa kunyongwa bila hta kuwa blackmailed wahamie CCM ili wafichiwe maovu yao!! Na majimbo yatabaki wazi na CCM watashinda kwa kishindo why walazimishe wakati kuna option B ya kuwatoa??

Na kingine kama wangeingia kwa blackmail ya kutishiwa hakuna angeruhusu wapewe ubunge tena ilihali wanajua wamekuja kwa shingo upande maana wataingia kwenye vikao vya chama pia vikao nyeti vya kiusalama n.k unless ungesema wajiuzulu siasa hapo sawa mimi naamini wanaingia CCM kwa mapenzi yao either ya pesa au vyeo ila sio kwa kulazimishwa hilo nakataa kwa SAUTI.

Labda niseme tu nahuzunika sana kuona mtanziko wa kisiasa uliopo lawama zinaenda upinzani yaani ni sawa na kuwalaumu besigye wa uganda au Diane Rwagira wa Rwanda eti wanakosa inteligentsia kupambana na madikteta does it make sense hivi hata Dr slaa angefanyeje kwa mfano mbele ya magufuli si angeshapigwa risasi na kupotezwa kma saanane na mawazo!!! Simple like that.....kma lissu aliyewapa upinzani hamasa ndio huyo kazawadiwa magazine ya SMG je Mbowe au mpinzani gani anao uwezo wa kupambana na chamadola (isomeke RISASI)?? Dr slaa??

Shida ni kubwa kuliko mnavyochangia kwa kuangalia upande mmoja humu ukitaka kuona hili... Leo magufuli amalize muda wake aje mama samia.... kwa udhaifu huu huu unaodai wa mbowe/intelligence ya chama n.k utashangaa CHADEMA inapaa zaidi sababu nini?? Chanzo kimeng'olewa

Embu tujikite kwenye chanzo

Cc chige Malcom Lumumba Pascal Mayalla tindo JokaKuu

Mkuu umechambua vizuri sana ,ila Mwisho ume shauri Watu wadill na Chanzo (How ?)..

Tayari tuna Chanzo kisicho Amini ktk Ushindani hasa wa Hoja kama kukosolewa nk ,kwa Mwenendo huu unafikiri Speed yake itaishia Kikatiba Muda utakapo fika ?.
 
zitto junior,

Awali ya yote niongelee kwanza hoja yako uliyosema inawezekana wabunge hawa hawanunuliwi wala nini lakini ni ile tu kutafuta uhakika!

Kwa namna fulani, nakubaliana na wewe lakini trend inavyoenda, natishika kidogo! Kama ni kawaida tu ya kutaka kujihakikishia miliki yao, kwanini basi wasingesubiri hadi 2019 ndipo wakaanza harakati za kuhakikisha wanarudi bungeni kwa njia yoyote ile? Mbona mapema sana as if wanakuwa approached in advance?! Na kama wanakuwa approached, what's the motivational factor?

Anyway, kama nilivyosema hapo awali, naogopa! Kimsingi, hofu yangu kuu sio sasa bali kuanzia 2019 hadi 2020 mwanzoni... kwa trend hii, wapo wengi wanaoweza kujiunga CCM sio kwa sababu wamenunuliwa bali kutafuta uhakika wa kurudi bungeni!

That's one but two, hoja ya Chahali nayo sio ya kupuuzwa. Kwanza tunaposema mbinu kama hizo ni kwamba, that has nothing to do with CHADEMA kama chama bali victim wanakuwa targeted personally! Hizi mbinu zipo na kama alivyosema Mleta Mada, zinakuwa very effective kwa sababu Main Players wanakuwa watu wa Kitengo wenye data za watu!

Lakini hata pale wanapokosa compromising info kuhusu wewe, unaweza hata kuwa framed na usione pa kutokea na salama kwako inakuwa ni kukubali ya Mabwana Mkubwa! Hizi mbinu nazo zipo unless wakutane na mafyatu wenzao kama ambavyo KGB na CIA walivyokumbana na fyatu mwenzao... rais wa zamani wa Indonesia; Sukarno!!

Hata hivyo, mtu unaweza kuhoji hapa kwamba, kama issue ni kompromat, yanini basi CCM iendelee kuwapa favor hawa jamaa ambao wapo compromised?! Mtu ukishakuwa compromised unakuwa ndo kwisha habari yako na hakuna tena sababu ya kuendelea kukupa favor! Wanaweza kukupa favor ya kukuacha pale pale ulipo ili waendelee kukutumia!!!
 
Kupata taarifa kwa TISS ya sasa not easy like that braza. Kitengo kwa sasa kina endeshwa kwa weledi na uzalendo. Wataishia kupata tetesi zisizo na uhalisia. Weewe unasikia hata siku izi Siri za vikao vya state house au vikao vikuu vya chama zinavuja kama zamani. Mambo yamebadilika sana na kiukweli nimeiamini ule msemo kuwa mtu mmoja anaweza kubadilisha mambo kabisa.
Mtu mrefu Paulo kafanikiwa kabisa kwakweli.
 
Vaa mkuu! Tupia na kabendera kadogo cha mkononi, halafu na wimbo.
Ndege yetu ileeeee
Raisi wetu yuleeee.
Hapo lazima kieleweke, ni mwendo wa kusaka fursa tu.
Kuna Jirani yangu Bagamoyo njia ya Msata , Shambani kwake kapiga bendera ya kijani shamba zima. Basi hakuna mtu anayemsogelea.
 
Chahali tumekusoma ila mimi nina machache kwako:

Inawezekana una ushauri au mawazo mazuri wakati fulanifulani, hata hivyo hoja zako zinakosa tija mara nyingi kwa sababu kadhaa. Labda nikuambie chache kwa ujumla wa kauli zako ziada ya uliyoitoa hapa

Sikiliza Chahali: Wewe ni mtu unayejivunia sana kuwa afisa wa usalama wa taifa utadhani wewe ndio mtanzani apekee uwewahi kufanya hiyo kazi au wewe ndio ulikua mkurugezi mkuu wa TISS au afisa bora kuliko wote. Hakuna kitu unaandika au unasema bila kuingiza ama hisia, kauli, misemo, uzushi, misiamiti, na mbwembwe za mwanausalama. Hivi kama kila daktari, mhandishi, mwalimu, mwanajeshi, mkunga, na wengine kwenye taalama zao watakua wanazitumia katika kujenga hoja au kuonesha umuhim wao au kuelezea mambo ya kijamii, tutaelewana kweli? Unataka kumfanya kila mtu anayekusoma aone usalama wa taifa ndio kazi bora, nyeti, na ya maana kuliko zote hivyo mtu aliyepita huko basi yeye ni mjuaji wa kila kitu, anajua siri nyingi na ni wa kuogopewa. Huu ni uzushi. Una miaka zaidi ya 10 tangu umekimbia hapa nyumbani, siri zote ulizoondoka nazo kwa sasa sio siri tena na zimepitwa na wakati. Wengi uliofanya nao kazi wengine wamebadilika kwa mengi na kustaafu. Labda uliotuacha vijana wadogo tukianza kazi ndio tumebaki na kumbukumbu zako. Ni uzushi uliopita mipaka kila siku kuwaaminisha watu kwamba wewe una siri za nchi, una siri za serikali, unajua CCM inafanya nini, unajua Rais anahusikaje na kitengo, na mengine. Unatumia habari za kuokoteza mitandaoni kujenga taswira isiyo sahihi kabisa juu ya ujuaji wako na unautumia kupotosha. hakuna intellejensia unayoijua kwa sasa zaidi ya kwenye vitabu na maandishi mengine ambayo kila mtu anaweza kujisomea. Huwezi kua nje ya kitengo kwa miaka zaidi ya 10 na bado ukajidai unajua utendaji wake.

Sikiliza Chahali: Unapenda kujifanya wewe ni mjuaji sana wa mbinu na mikakati ya kisiasa. Ila kwa taarifa zako ambazo wewe mwenyewe umezijaza mitandaoni, hujawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi wa CCM wakati unakitumikia na kukisaidia kuiba kura. Hujawahi kusimama jukwaani wala kupigiwa kura. Hujawahi hata kuteuliwa kusaidia kazi za kisiasa. Ila ni ajabu sana unapokua mtaalamu juu wa wataalamu wote kuhusu siasa. Moja ya makala yako ulituambia jinsi ulivyohusika au kujua kama afisa wa TISS kuiba kura za wapinzani kuanzia mwaka 1995.. huo uzoefu sidhani kama CDM na wapinzani wengine wa kweliu wanauhitaji.

Sikiliza Chahali: Wewe ni kigeugeu, huna msimamo, na huna moral values za kuwanyooshea wengine vidole. Kwanza hadi leo hujawahi kutuambia watanzania nini kilikukimbiza Tanzani ukaenda kujificha huko Uingereza. Umebaki kujisifia ni afisa usalama mstaafu na kuitaja Scotland kama utambulisho wako na kama mafanikio yako makubwa. Wewe ulikua unaipinga CCM kwa miaka mingi lakini 2015 ghafla ukageuka kuwa mpiga debe wa CCM hata kuliko wenye chama chao. Hazijapita siku nyingi ukatuandikia kitabu cha kumsifu Magufuli ambacho leo hata wewe mwenyewe unakikimbia na huwezi kuikiongelea.. ulaji ulipokata CCM (ulituambia kwenye Makala uliyomwandikia Kinana) ghafla ukageuka kuwa mpinzani mkubwa wa mtu uliyempigia kampeni. Napata wasiwasi labda hakukupa asante na mshiko kwa kumuandikia kitabu cha kumsifu. Ulikua unabeza na kuwadhalilisha viongozi wa CDM mitandano ghafla ukaanza tena kuwa mtetezi wao. Umeona CDM hakuna ulaji na malipo kama uliyolipwa na CCM wakati wa kampeni sasa umegeuka kuwa KUNGWI wa kuwafundisha siasa na namna ya kupambana na CCM huku ukiwa umejificha nyuma ya kompyuta huko Uingereza. Unatoa wapi huo ujasiri wa kuwasema CDM wakati wenzako wako katika uwanja wa vita wananusa harufu ya damu?

Sikiliza Chahali: Tuchukulie kwamba una nia njema ya kuisaidia CDM au wapinzani wengine ambao wewe hutaki kujiunga nao. Ila umewahi kuona wapi askari walio kwenye kikosi cha mapambano wanaanza kudharauliana na kukebehiana hadharani na mbele ya adui wanayepambana naye? kwa nini usiwe unawasida CDM na wapinzani wengine kimkakati kwa kutumia huo utalaamu wako unajigamba nao? Kama unajua CDM haina kitengo cha intellejensia na wewe ni mwana intelejensia kwa nini usijiunge na kuwaonesha una msaada? unataka kila unachofanya dunia nzima ijue na kisiposikilizwa ghafla unageuka kuwa mkosaji. Ni mtu ambaye hajui ugumu wa siasa za Tanzania chini ya JPM pekee kama wewe anayeweza kuwa jasiri anayeweza kuwa na ujasiri wa kutumia muda mwingi kuwakosao na kupambana na watu kama CDM na wenzao wachache kama kina Zitto na Mtatito ambayo wameyaweka maisha yao rehani kuwasemea watanzania wasioweza kujieleza. Wewe uliyejificha nyuma ya kompyuta au simu yako, kikubwa ungewasaidia nyuma ya pazia kwa taarifa na mikakati kama unayo na sio kuwabwekea hadharani kila mara na kwamba hawashauriki.

Sikiliza Chahali: Inawekana kukaa huko ulikojificha kumekupa mwanga wa mambo kadha wa kadha kwa sababu zilizo wazi. Ila ni uzushi kutaka kuwaaminisha watanzania wewe unajua kila kitu. ninapopita kwenye miaandishi yako mitandaoni wewe ni mtaalamu wa kila kitu. unafundisha watu kila kitu kuanzia IT, mitandano, usalama, busara, maadili, biashara, uandishi, siasa, jinsi ya kufanikiwa, nk. Halafu ukiulizwa hata maswali ya kawaida kabisa ya ufafanuzi unakua mkali sana na kuanza kuporomosha matusi na kushambulia watu. Kwa umri wako na utaalamu unaojigamba unao havifanani kabisa na matusi unayotukana watu mitandaoni.

Sikiliza Chahali: Nikushauri kua inapokuja kwenye siasa za hapa Tanzania chini ya uongozi wa kikatili na kiimla uliopo, kama nawe hufurahishwi nayo huko nyuma ya kompyuta uliko jitahidi tu kutoa maoni na kukemea kama wengi wafanyavyo. Ila huna kabisa uwezo na mamlaka ya kimaadili na ujuzi wa kuwafunisha CDM au ACT au CUF namna ya kufanya siasa za kuimarisha vyama vyao, kuzuia watu kuhama, na namna ya kukabiliana na serikali inayoendeshwa na mitazamo katili. Kama vipi njoo ujiunge kwenye chama hata cha Dovutwa ili nawe ufanye harakati za kupambana na CCM uone inavyofanana. Maumivu tunayoyapata hapa nyumbani yanatuondolea kabisa uvumilivu wa kumsikiliza mtu yoyote anayetumia nguvu kuwakosoa wanaopambana kwa ajili yetu, tusio na vyama, wenye vyama, na hata walio ndani ya CCM na wamenyamaza kwa uvumilivu wakiogopa kupigwa wao na shangazi zao. Waache CDM na vyama vingine vyenye nia ya dhati ya kupammba na ukatili unaondelea wafanye waanachoweza.

Sikiliza Chahali: ninapomalizia nikushauri wewe na mtanzania mwingine yoyote aliye ndani ya nchi au huko nje kokkote nyuma ya TV au kompyuta ambaye anachukia yanayoendelea nyumbani, tafadhali watieni moyo sana wanaopambana kwa ajili yetu. Wawe ni ACT, CDM, CUF, NCCR, au watu mmoja mmoja wenye ujasiri wa kusema au wanaotumia mitandao kuandika kinyume na ukatili na ungozi mbovu unaota mizizi kila kona, watiwe moyo na wasidiewe nila kujali madhaifu yao yasiiyo na madhara kwetu. Askari asiyejua kushika silaha au kulenga shabaha asaidiwe au kufundishwa namana ya kufanya lakini isiwe kumzoea kwamba hajui kupigana au ni dhaifu.

Ni mimi afisa mwenzako (ila sijakimbia wala kusatafu)

Mutumishi wa umma
Huu ujumbe umebariki sana siku yangu leo
 
Siri nyingi CHADEMA walikuwa wakipewa na Lowasa na mtandao wake waliokuwa serikalini na ndani ya CCM.Baada ya mtandao ule kuvujwa serikalini na ndani ya CCM siri hazitoki hovyo tena si kwamba Chadema walikuwa na intelligencia kali
Hahahahhaa dah we jamaa na chuki kwa lowassa ina maana hadi zile nondo za slaa kumkaanga lowassa na serikali yake alipewa na lowassa mwenyewe?? hahahhaaa nmecheka sana
 
Hahahahhaa dah we jamaa na chuki kwa lowassa ina maana hadi zile nondo za slaa kumkaanga lowassa na serikali yake alipewa na lowassa mwenyewe?? hahahhaaa nmecheka sana
Walipewa Na team Sumaye
 
Back
Top Bottom