Kama washauri wenyewe wa Chadema ndio hawa...

Kama washauri wenyewe wa Chadema ndio hawa...

Yours is a dull party. There are million ways of doing politics in Tanzania. The problem is dwarfism facing your party together with its entire leadership, which is conversant with only one way/approach of doing politics in the country - the non-committal non accountable political campaign. Does your party have permanent qualified personnel, office infrastructure (including live internet connectivity), active party organisation machinery, et la? And if not why? The reason is obvious. Mbowe's inner motive is more of focussing on making money than leading the party to victory. That is the real compromise factor your party and members altogether must endure. Try dissecting your party to know this and perhaps more maladies it has compromised.
A. Can you precisely elaborate any strategy or another ''million way'' CHADEMA can do politics??

B. From the strategy you have proposed in A can you suggest how they can meet to discuss it without interference from the state?? That's if at all they won't be arrested prior to the meeting to discuss the strategy for inciting aka Uchochezi!!

C. In case the strategy you proposed in A works what reaction do you expect from the ruling JUNTA?? In case the master planner is shot like lissu or abducted like saanane what will be the way forward given that the police are under the same party which the strategy you suggested in A will affect them in one way or the other

Am patiently waiting for your reply mkuu
 
Chadema imepoteza wabunge wawili ndani ya takriban masaa 48. Kila anayefuatilia kwa karibu matukio haya anaifahamu drill: CCM watakaa pembeni wakiwa na kicheko kikubwa huku "waasi" kutoka Chadema wakifanya kazi ya kukaanga chama hicho kikuu cha upinzani. Then Chadema watakuja na script Ileile "acha waondoke. Chama bado imara." Baada ya hapo, maisha yanaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.

Ni rahisi kuilaumu CCM kwamba inatumia mbinu chafu "kulazimisha" wabunge na madiwani wa Chadema kujiunga na chama hicho tawala. Hilo la mbinu chafu ni kweli, na ni chafu kwelikweli. Kwa kifupi, nyenzo muhimu inayowezesha hamahama hiyo ni ile "ya Putin kwa Trump" yaani KOMPROMAT. Ileile ambayo JIWE anafanyiwa na "Mtu Mrefu Paulo." Yawezekana kabisa kuwa mbinu hii ambayo ni maarufu sana katika "sistema" huko Russia ikihusisha mashushushu, inaweza kuwa ni "msaada wa kiutawala" kwa Jiwe kutoka kwa "Mtu Mrefu Paulo."

Uzuri wa "kompromat" ni kwamba it usually works, tena kwa ufanisi. Fanikiwa kupata compromising info kuhusu mlengwa, basi huyo anakuwa mtumwa wako wa kudumu. Labda kuna siku nitapata wasaa wa kueleza hili kiundani ila ninachoweza kueleza kwa sasa ni kwamba hamahama hii inaambatana na udhalilishaji mkubwa ambao baadaye hutumika kwenye "kompromat."

Lakini Chadema haiwezi kukwepa lawama kwa haya yanayoisibu. Wakati flani, chama hicho kilikuwa na Idara ya intelijensia iliyokuwa hodari mno, yayumkinika kusema "hodari karibu au hata zaidi ya TISS." Hii ilikuwa Chadema ya enzi za kina Dokta Slaa. Ilikuwa both defensive and offensive. Defensive kwa namna ilivyoweza kubaini hujuma mbalimbali dhidi ya chama from CCM na kitengo. Offensive kwa namna ilivyoweza kujipenyeza serikalini na hata TISS na ndio maana iliwezekana kuibua skandali mbalimbali kama EPA, Richmond, nk.

Ninaweza kusema bila kusita kuwa laiti ingekuwa zama hizo, hawa wanaohama wangejulikana kabla hawajafanya "surprises" hizi za mfululizo. Kusema "ah huyu alikuwa mzigo" ilhali hamkumtimua mpaka akawakimbia ni utoto wa kisiasa. Kudai "acha waende" ilhali hatuambiwi kuwa "huyu na yule kamwe hawawezi kuhama" ni mzaha.

Kwa uelewa wangu, kuna wabunge wengine kadhaa wapo njiani kuhama. Na kama unadhani hizi ni porojo tu, zingatia "ubashiri" wangu huu nilioutoa majuzi na umetimia

Chadema kuilaumu CCM kwa mbinu chafu ni sawa na Yanga kuilaumu Simba kwa hujuma. Iwe kwa njia halali au zisizo halali, jukumu la kujikinga na hujuma za adui haliwezi kutegemea huruma ya adui. Kwamba "tuzembee, akitudhuru tumlaumu." Who cares?

Talking of mapungufu ya kiintelijensia ndani ya Chadema, nimekutana na bandiko la mmoja wa "think tanks" za chama hicho, Bwana Yericko. Let's be honest, kama "washauri wa kiintelijensia" wa Chadema ndio wa aina hii, basi mustakabali wa chama hicho upo hatarini. Hebu angalia bandiko hili hapa chini la Bwana Yericko kisha rejea bandiko halisi "aliloiba" huko Facebook.

Bandiko la Yericko ni hili hapa Kama nitasafiri kwa ndege moja na Polepole na Lugola nitaomba niwaelekeze haya:

Bandiko aliloiba kutoka kwa Mheshimiwa Ismail Jussa ni hili hapa Ismail Jussa

Labda hili halihusiani na "mapungufu" ya Chadema lakini nonetheless halileti picha nzuri, especially katika kipindi hiki ambapo chama hicho kikuu cha upinzani kinapitia kipindi kigumu.


View attachment 823207View attachment 823208View attachment 823209View attachment 823210View attachment 823211View attachment 823212View attachment 823213View attachment 823214View attachment 823215View attachment 823216View attachment 823217View attachment 823218

Sasa badala ya kulaumu Chadema, what are you doing to help the country? Naona post zako zote tu ni kulaumu Chadema, huku husaidii lolote, hata hizo intelligence info ambazo kila wakati hujidai unazo hakuna lolote la maana zaidi ya blah blah tu Evarist Chahali
 
Hakuna siasa chafu,nakumbuka 2013-2015 chadema ilipokea wana ccm wengi sana...hizo hazikuwa siasa chafu za chadema wala chadema haikununua mtu...
Nina uhakika leo hakuna anayenunuliwa...Ila watu hawaoni mwelekeo wao,hawaoni kesho yao....
Wapo wengi wanatamani kuondoka....Ila hawajui njia yakupita....

Siyo jambo lakufurahisha....Mbowe hajawahi kuwa kiongozi makini....
ww nae ndio tahira namba 1,kwani CDM ndio imeshika dola hadi mtu aione kesho yake? tokea mfumo wa vyama vingi uanze wamekuwepo viongozi waliopendwa katika msimu wao wa 1 kama kikwete zaidi ya magufuli kwa 98% lakini hukuona hata mbunge 1 akihama chama fulani kwenda chama fulani katikati ya ubunge wake ati waje kuhama kwa magufuli.
hivi inakuingia akilini mtu aache mapato yote anayoyapata kwa kuwa mbunge aache tu kisa ameona kuwa eti kwenye CCM kuna future?.tumie ubongo wako kuandika vitu vyenye maana sio kuandika kwa kuwa humpendi mtu.
 
Sasa badala ya kulaumu Chadema, what are you doing to help the country? Naona post zako zote tu ni kulaumu Chadema, huku husaidii lolote, hata hizo intelligence info ambazo kila wakati hujidai unazo hakuna lolote la maana zaidi ya blah blah tu Evarist Chahali
achana nae mkuu huyo ni mjinga namba 1 hajui hata analolizungumza-toka mwaka 1992 kulikuwa na vyama vya siasa na wabunge hawakuwahi kuhama vyama katikaati ya mihula yao,eti kwa miaka 25 yote intelejinsia ya vyama vya upinzani ilikuwa vizuei kuliko mwaka huu 2018-non sense.
 
Khaaaaa naona unahamisha magoli tu 😛😛
Wagombea uraisi CCM waliotakia kuteuliwa walikuwa 42 Na team zao walikuwa wakipana matope vibaya mno chadema ndio akawa agent wao Kila mtu kumchafua mwingine alikuwa akitumia kubenea Na magazeti yake,na Tundu Lisu na mabomu yake Na Slaa Na Zitto Kabwe Na Godbless Lema kusema tuna taarifa za uhakika nk Kwa hiyo usishangae Vita ya nani ashike waliipeleka chadema ili hao chadema wa infuence maamuzi ndani ya CCM .Intellinjia ya CCM ikadaka ikapiga zinga la chenga la mwili ikampa magufuli.The alliance of the frustrated waliotwangana vijembe Lowasa ,Sumaye,Makojgoro mahanga wakaamua waache tofauti zao wahamie chadema kumchafua steam out temporarily their frustrations.Ndani ya CCM hao walikuwa mahasimu wakubwa
 
A. Can you precisely elaborate any strategy or another ''million way'' CHADEMA can do politics??

B. From the strategy you have proposed in A can you suggest how they can meet to discuss it without interference from the state?? That's if at all they won't be arrested prior to the meeting to discuss the strategy for inciting aka Uchochezi!!

C. In case the strategy you proposed in A works what reaction do you expect from the ruling JUNTA?? In case the master planner is shot like lissu or abducted like saanane what will be the way forward given that the police are under the same party which the strategy you suggested in A will affect them in one way or the other

Am patiently waiting for your reply mkuu
Refined expertise has never been offered for free guy. Chadema has government subventions paid to its coffers every moon. Let it pay for such expertise if the leadership is interested in taking the party ahead of current turmoil.
 
Chahali una ugomvi binafsi na Yericko mtafute mmalizane.

Pia intelijensia ya Chadema ikijua fulani atanunuliwa siku fulani then itangazwe ndiyo huyo mtu ataghairi kununuliwa??
Binafsi nimegundua wana mgogoro wa kibiashara maana hao wote wana vitabu wanauza vya kijasusi/kishushu nahisi hapo ndio kwenye ugomvi wao mkuu.
 
Refined expertise has never been offered for free guy. Chadema has government subventions paid to its coffers every moon. Let it pay for such expertise if the leadership is interested in taking the party ahead of current turmoil.
I see..... But expertise critique is offered for free???
 
Refined expertise has never been offered for free guy. Chadema has government subventions paid to its coffers every moon. Let it pay for such expertise if the leadership is interested in taking the party ahead of current turmoil.

This is the risk of having multiple accounts on the same platform, one with real and other with fake name(s). Chahali has panicked and confused. He doesn't know whether he should use his real or fake account to respond on this thread. He is using his fake account (Sophist ) but speaking what he would always do when he shows his true colours.

Hizi kauli za kujiona ni mtaalamu anayehitajika kulipwa kwa anachokiita "utaalamu wa kijasusi au intelejensia" ni zake. Anadhani kwa kuwa "aliokoteza deal" ya kumpigia JPM kampeni mitandanoni mwaka 2015 na kulipwa na CCM, basi keshakua mtaalamu na anastahili kulipwa hata wa kutoa "ushauri wa ki-intelejensia" ya kizushi huku akiwa hana uzoefu wowote wa siasa na changamoto zake. Kauli anazozitoa na kuziita za kiitelejensia ni uzushi, umbea, na habari za kukukota tu mitaani na kujigamba ni mwanausalama. Kauli anazotoa na kuziita #markthistweet kule Twitter kwamba ni habari za ukweli, ni tabiri zisizo na tofauti na alizokua anatoa Shekhe Yahaya na vitu vingine ni vya kutabirika kabisa na sio ujuaji wala utaalamu. Hakuna namna kikosi cha TISS cha karne hii kikaendelea kuvujisha siri za nchi kwa mtu ambaye hata sura yake hawaikumbuki.

Acha kupoteza muda kuwashambuliwa askari walio kikosi cha mbele kupambana na ukatili na uongozi mbovu chini ya CCM kwa kigezo kwamba hawajui ufundi wa vita huku wewe ukiwa umekimbia uwanja wa vita ambavyo hujawahi pigana na hauna hata kikosi unachokiongoza toka huko "porini" nyuma ya keyboard. Nakufananisha na mshabiki ambaye ni fundi wa ukosoaji wachezaji na kocha huku yeye akiwa hajawahi hata kucheza mpira wa makaratasi mchangani. Karibu nyumbani uje upambane ukiwa kiwanjani kisha ushauri na kasoa zako kwa wapizani zitazingatiwa. Prophets of doom are good at demotivating and demoralising, and this is exactly what you are doing to CDM, unfortunately and miserably, for nobody's benefit.
 
Usajili wa wachezaji unaendelea naona wachezaji wanajikakamua ili waweze nunuliwa kwenda kwenye timu inayongoza ligi!

Ova
 
ww nae ndio tahira namba 1,kwani CDM ndio imeshika dola hadi mtu aione kesho yake? tokea mfumo wa vyama vingi uanze wamekuwepo viongozi waliopendwa katika msimu wao wa 1 kama kikwete zaidi ya magufuli kwa 98% lakini hukuona hata mbunge 1 akihama chama fulani kwenda chama fulani katikati ya ubunge wake ati waje kuhama kwa magufuli.
hivi inakuingia akilini mtu aache mapato yote anayoyapata kwa kuwa mbunge aache tu kisa ameona kuwa eti kwenye CCM kuna future?.tumie ubongo wako kuandika vitu vyenye maana sio kuandika kwa kuwa humpendi mtu.

Wewe umetumia ubongo wako kufikiri.
Hakuna haja ya kujibishana na wewe sina mda...macho yanaona,masikio yanasikia.
All the best
 
Chahali analysis yako ni very poor! Nilikuwa nakuamini sana katika haya mambo. Kumbe na wewe ni wale wale. Unasahau kuwa CDM is dealing with a BRUTAL DICTATOR in all senses. How do you deal with someone using a gun, police, army to silence opossition and not HOJA kupambana na upinzania? Unapambanaje na Dikiteita ambaye hata vikao vya ndani amevikataza, viongozi wote wanabambikiwa kesi? Mahakama compromised??? (kwa kiasi fulani CJ aliingilia siasa kidogo) .Ruhusu CDM iende kwa watu iwahubirie kinachoendelea uone kama haitaungwa mkono. Unapambanaje na Idd Amin, Kim Jong Un , Kagame ,,, (Diane Rwigima) , Museveni and the like. Nadhani umenielewa Evarist Chahali


Mpinzania wa Kagame ashitakiwa kwa kosa la uasi

By Rashid Bugi -

View attachment 823222

Mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.

Ameshtakiwa pamoja na mama yake mzazi aitwae Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.
Diane Rwigara aluzuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti nchini Rwanda ambapo rais Kagame alishinda kwa kishindo.
Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kuikuwa na udanganyifu madai yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.
Diane Rwigara pia ameshtakiwa kwa kubuni stakabadhi bandia.
Wachunguzi wanadai kuwa Bi Rwigara alivunja sheria za uchaguzi kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono ugombeaji wake.
Haijulikani ni kitu gani kilichangia afunguliwe mashtaka ya kuchochea uasi nchini humo pamona na ndugu zake.

You are so dumb
 
Chahali tumekusoma ila mimi nina machache kwako:

Inawezekana una ushauri au mawazo mazuri wakati fulanifulani, hata hivyo hoja zako zinakosa tija mara nyingi kwa sababu kadhaa. Labda nikuambie chache kwa ujumla wa kauli zako ziada ya uliyoitoa hapa

Sikiliza Chahali: Wewe ni mtu unayejivunia sana kuwa afisa wa usalama wa taifa utadhani wewe ndio mtanzani apekee uwewahi kufanya hiyo kazi au wewe ndio ulikua mkurugezi mkuu wa TISS au afisa bora kuliko wote. Hakuna kitu unaandika au unasema bila kuingiza ama hisia, kauli, misemo, uzushi, misiamiti, na mbwembwe za mwanausalama. Hivi kama kila daktari, mhandishi, mwalimu, mwanajeshi, mkunga, na wengine kwenye taalama zao watakua wanazitumia katika kujenga hoja au kuonesha umuhim wao au kuelezea mambo ya kijamii, tutaelewana kweli? Unataka kumfanya kila mtu anayekusoma aone usalama wa taifa ndio kazi bora, nyeti, na ya maana kuliko zote hivyo mtu aliyepita huko basi yeye ni mjuaji wa kila kitu, anajua siri nyingi na ni wa kuogopewa. Huu ni uzushi. Una miaka zaidi ya 10 tangu umekimbia hapa nyumbani, siri zote ulizoondoka nazo kwa sasa sio siri tena na zimepitwa na wakati. Wengi uliofanya nao kazi wengine wamebadilika kwa mengi na kustaafu. Labda uliotuacha vijana wadogo tukianza kazi ndio tumebaki na kumbukumbu zako. Ni uzushi uliopita mipaka kila siku kuwaaminisha watu kwamba wewe una siri za nchi, una siri za serikali, unajua CCM inafanya nini, unajua Rais anahusikaje na kitengo, na mengine. Unatumia habari za kuokoteza mitandaoni kujenga taswira isiyo sahihi kabisa juu ya ujuaji wako na unautumia kupotosha. hakuna intellejensia unayoijua kwa sasa zaidi ya kwenye vitabu na maandishi mengine ambayo kila mtu anaweza kujisomea. Huwezi kua nje ya kitengo kwa miaka zaidi ya 10 na bado ukajidai unajua utendaji wake.

Sikiliza Chahali: Unapenda kujifanya wewe ni mjuaji sana wa mbinu na mikakati ya kisiasa. Ila kwa taarifa zako ambazo wewe mwenyewe umezijaza mitandaoni, hujawahi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi wa CCM wakati unakitumikia na kukisaidia kuiba kura. Hujawahi kusimama jukwaani wala kupigiwa kura. Hujawahi hata kuteuliwa kusaidia kazi za kisiasa. Ila ni ajabu sana unapokua mtaalamu juu wa wataalamu wote kuhusu siasa. Moja ya makala yako ulituambia jinsi ulivyohusika au kujua kama afisa wa TISS kuiba kura za wapinzani kuanzia mwaka 1995.. huo uzoefu sidhani kama CDM na wapinzani wengine wa kweliu wanauhitaji.

Sikiliza Chahali: Wewe ni kigeugeu, huna msimamo, na huna moral values za kuwanyooshea wengine vidole. Kwanza hadi leo hujawahi kutuambia watanzania nini kilikukimbiza Tanzani ukaenda kujificha huko Uingereza. Umebaki kujisifia ni afisa usalama mstaafu na kuitaja Scotland kama utambulisho wako na kama mafanikio yako makubwa. Wewe ulikua unaipinga CCM kwa miaka mingi lakini 2015 ghafla ukageuka kuwa mpiga debe wa CCM hata kuliko wenye chama chao. Hazijapita siku nyingi ukatuandikia kitabu cha kumsifu Magufuli ambacho leo hata wewe mwenyewe unakikimbia na huwezi kuikiongelea.. ulaji ulipokata CCM (ulituambia kwenye Makala uliyomwandikia Kinana) ghafla ukageuka kuwa mpinzani mkubwa wa mtu uliyempigia kampeni. Napata wasiwasi labda hakukupa asante na mshiko kwa kumuandikia kitabu cha kumsifu. Ulikua unabeza na kuwadhalilisha viongozi wa CDM mitandano ghafla ukaanza tena kuwa mtetezi wao. Umeona CDM hakuna ulaji na malipo kama uliyolipwa na CCM wakati wa kampeni sasa umegeuka kuwa KUNGWI wa kuwafundisha siasa na namna ya kupambana na CCM huku ukiwa umejificha nyuma ya kompyuta huko Uingereza. Unatoa wapi huo ujasiri wa kuwasema CDM wakati wenzako wako katika uwanja wa vita wananusa harufu ya damu?

Sikiliza Chahali: Tuchukulie kwamba una nia njema ya kuisaidia CDM au wapinzani wengine ambao wewe hutaki kujiunga nao. Ila umewahi kuona wapi askari walio kwenye kikosi cha mapambano wanaanza kudharauliana na kukebehiana hadharani na mbele ya adui wanayepambana naye? kwa nini usiwe unawasida CDM na wapinzani wengine kimkakati kwa kutumia huo utalaamu wako unajigamba nao? Kama unajua CDM haina kitengo cha intellejensia na wewe ni mwana intelejensia kwa nini usijiunge na kuwaonesha una msaada? unataka kila unachofanya dunia nzima ijue na kisiposikilizwa ghafla unageuka kuwa mkosaji. Ni mtu ambaye hajui ugumu wa siasa za Tanzania chini ya JPM pekee kama wewe anayeweza kuwa jasiri anayeweza kuwa na ujasiri wa kutumia muda mwingi kuwakosao na kupambana na watu kama CDM na wenzao wachache kama kina Zitto na Mtatito ambayo wameyaweka maisha yao rehani kuwasemea watanzania wasioweza kujieleza. Wewe uliyejificha nyuma ya kompyuta au simu yako, kikubwa ungewasaidia nyuma ya pazia kwa taarifa na mikakati kama unayo na sio kuwabwekea hadharani kila mara na kwamba hawashauriki.

Sikiliza Chahali: Inawekana kukaa huko ulikojificha kumekupa mwanga wa mambo kadha wa kadha kwa sababu zilizo wazi. Ila ni uzushi kutaka kuwaaminisha watanzania wewe unajua kila kitu. ninapopita kwenye miaandishi yako mitandaoni wewe ni mtaalamu wa kila kitu. unafundisha watu kila kitu kuanzia IT, mitandano, usalama, busara, maadili, biashara, uandishi, siasa, jinsi ya kufanikiwa, nk. Halafu ukiulizwa hata maswali ya kawaida kabisa ya ufafanuzi unakua mkali sana na kuanza kuporomosha matusi na kushambulia watu. Kwa umri wako na utaalamu unaojigamba unao havifanani kabisa na matusi unayotukana watu mitandaoni.

Sikiliza Chahali: Nikushauri kua inapokuja kwenye siasa za hapa Tanzania chini ya uongozi wa kikatili na kiimla uliopo, kama nawe hufurahishwi nayo huko nyuma ya kompyuta uliko jitahidi tu kutoa maoni na kukemea kama wengi wafanyavyo. Ila huna kabisa uwezo na mamlaka ya kimaadili na ujuzi wa kuwafunisha CDM au ACT au CUF namna ya kufanya siasa za kuimarisha vyama vyao, kuzuia watu kuhama, na namna ya kukabiliana na serikali inayoendeshwa na mitazamo katili. Kama vipi njoo ujiunge kwenye chama hata cha Dovutwa ili nawe ufanye harakati za kupambana na CCM uone inavyofanana. Maumivu tunayoyapata hapa nyumbani yanatuondolea kabisa uvumilivu wa kumsikiliza mtu yoyote anayetumia nguvu kuwakosoa wanaopambana kwa ajili yetu, tusio na vyama, wenye vyama, na hata walio ndani ya CCM na wamenyamaza kwa uvumilivu wakiogopa kupigwa wao na shangazi zao. Waache CDM na vyama vingine vyenye nia ya dhati ya kupammba na ukatili unaondelea wafanye waanachoweza.

Sikiliza Chahali: ninapomalizia nikushauri wewe na mtanzania mwingine yoyote aliye ndani ya nchi au huko nje kokkote nyuma ya TV au kompyuta ambaye anachukia yanayoendelea nyumbani, tafadhali watieni moyo sana wanaopambana kwa ajili yetu. Wawe ni ACT, CDM, CUF, NCCR, au watu mmoja mmoja wenye ujasiri wa kusema au wanaotumia mitandao kuandika kinyume na ukatili na ungozi mbovu unaota mizizi kila kona, watiwe moyo na wasidiewe nila kujali madhaifu yao yasiiyo na madhara kwetu. Askari asiyejua kushika silaha au kulenga shabaha asaidiwe au kufundishwa namana ya kufanya lakini isiwe kumzoea kwamba hajui kupigana au ni dhaifu.

Ni mimi afisa mwenzako (ila sijakimbia wala kusatafu)

Mutumishi wa umma

Gazeti refu linalotueleza hamko tayari kuelewa mtu yeyote atoaye hoja kingana. Nawaza mngepewa nchi angepona mtu. Madogo ndo Hivi je makubwa.
 
Back
Top Bottom