Kama utawala huu utarudi madarakani 2020-2025 basi watanzania tujiandae kisaikolojia

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Poleni sana Watanzania wote napenda kutoa angalizo kuwa hali itakuwa tofauti sana endapo utawala huu utarejea madarakani.

Kama ambavyo Marekani alishaonya kuhusu tume huru ya uchaguzi.

1: Huenda tukawekewa vikwazo vya kiuchumi hasa na taifa la Marekani.

2: Huenda wanasiasa watakaopigwa marufuku kusafiri Marekani wakaongezeka na kuwa wengi

3: Huenda Uhusiano wetu na WB&IMF ukawa kwenye msukosuko.

4: Huenda taifa likazidi kugawanyika kwa misingi ya kisiasa na kijamii.

5: Huenda bidhaa kutoka Marekani na Ulaya zikawa adimu kutokana na vikwazo.

6: Natabiri pesa yetu kuporomoka kutokana na vikwazo vya kuuza nje.

7: Kuendelea kwa misuguano ya kisiasa kwa miaka 5 mpaka 2025 atimaye uchumi kuporomoka na kupoteza mwelekeo kabisa.

Poleni sana, Uzuri vikwazo havitaangalia wewe ni CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NCCR au TLP vitakuwa kwa wote endeleeni kuwashangilia watawala.

Ingawa bado kuna nafasi ya kurekebisha haya ila sioni utashi wa kisiasa wa utawala uliopo madarakani kubadilisha chochote.
 
Itategemea watarudi vipi madarakani, wakirudi kwa njia za kihuni kulazimisha ushindi watakiona cha mtema kuni, wanapiga kelele wanasahau bajeti yao mpaka leo inamtegemea beberu awajazie.
 
Poleni sana Watanzania wote napenda kutoa angalizo kuwa hali itakuwa tofauti sana endapo utawala huu utalejea madarakani.
1: Uenda tukawekewa vikwazo vya kiuchumi hasa na taifa la Marekani. 2: Uenda wanasiasa watakaopigwa marufuku kusafiri Marekani wakaongezeka na kuwa wengi 3: Uenda Uhusiano wetu na WB&IMF
Pia Zimbabwe ya Mugabe itafika Tanzania!
 
Poleni sana Watanzania wote napenda kutoa angalizo kuwa hali itakuwa tofauti sana endapo utawala huu utalejea madarakani.
1: Uenda tukawekewa vikwazo vya kiuchumi hasa na taifa la Marekani. 2: Uenda wanasiasa watakaopigwa marufuku kusafiri Marekani wakaongezeka na kuwa wengi 3: Uenda Uhusiano wetu na WB&IMF ukawa kwenye msukosuko. 4: Uenda taifa likazidi kugawanyika kwa misingi ya kisiasa na kijamii. 5: Uenda bidhaa kutoka Marekani na ulaya zikawa adimu kutokana na vikwazo.
Hakuna namna mkuu utawala huu usirudi madarakani. Wewe anza maandalizi ya saikolojia mapema. Sisi tunajiandaa kuendana nao na tuzidi kuneemeka shauri yako wewe.
 
Hahah Chadema mkiwa nyuma ya keyboard mkwara sana.
Itategemea watarudi vipi madarakani, wakirudi kwa njia za kihuni kulazimisha ushindi watakiona cha mtema kuni, wanapiga kelele wanasahau bajeti yao mpaka leo inamtegemea beberu awajazie.
 
Magufuli hata asipofanya kampeni ushindi ni 98%

Yes, 98% ila kwa wapiga kura wachache mno. Maana watakaoshiriki huo uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi, ni wazee na vijana wasiojitambua.
 
Mkuu Ccm ya sasa sio ya jana

Ccm inakubalika kuliko wakati wowote ule

Haikubaliki, bali inaoogopeka, maana kwa sasa hakuna ccm kama chama cha siasa, bali kuna vyombo vya dola na kundi la watu wasiojulikana.
 
Acha iwe maana tunao uwezo wa kujifukiza bira msaada wa hao mabeberu
Mbona jana tu yule mimacho kodo kasema amempigia beberu wa Ireland kuomba msaada. Huku wanawaita mabeberu huku wanatembeza bakuli. Na sasa mmeba bakuli mkuu ni Kbud
 
Back
Top Bottom