Kama upo ARUSHA hii inakuhusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama upo ARUSHA hii inakuhusu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bushbaby, Jun 21, 2011.

 1. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Nimetoka kuongea na Customer care Tanesco (kwa simu namba 0732 979280) kuhusu mgao mpya wa umeme cha kusikitisha jamaa anaongea huku akicheka kuwa sehemu kubwa ya Arusha haitakuwa na umeme kabisa mchana kwa majuma kadhaa..(sishangai kwani sakina kuanznia j'pili hatuna umeme) nilipomuuuliza mpaka lini akasema Mungu ndo anajua....sasa najiuliza hilo jibu maana yake ni nini wakati rais ni juzi ameingiza kampuni ya Kimarekani kuzalisha umeme....au ile kampuni ni kanyaboya wahusika wanaendelea na ishu nyingine? Jamani tutaishije tunaochomelea....wafugaji wa kuku...wauza samaki wabichi.....internet cafe......saloon sawmill mashine za kusaga.....hii mbona ni kama kukomoana?
   
 2. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jana kwetu Ngurero umerudi asubuhi saa 12. baada ya kukatika kwa siku mbili. TANESCO ni bora ibinafsishwe tu ni kwero sana halafu hawa wafanyakazi wake wana dharau sana.
   
 3. Madikizela

  Madikizela JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2009
  Messages: 319
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nipo hapa golden rose kwa warsha umeme ni kero inabidi kutumia generator kelele mtindo mmoja:majani7:
   
 4. K

  Kipre tchetche JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanesco Arusha sasa mnaharibu na
  kuua uchumi wa watu maana sasa mmegeuka
  wanasiasa na sio wafanyabiashara umeme
  Haukatiki kwa sababu kuna hitlafu mahali
  ni siasa za kipumbavu tu natoa wito kwa Wana Arusha wote tuamke sasa tudai haki zetu hata kwa maandamano umeme
  ni haki yetu sote kwanini baadhi ya maeneo haukatiki uzunguni line za jeshi na ikulu ndogo viwanda vya waasia hawakati watanzania wanateseka kwenye nchi Yao wenyewe kuna siku Arusha itaamka na kusema basi.
   
 5. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tutamkumbuka EL
   
 6. S

  Schofild JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wanasema kisa ni Arusha kuchagua Chadema.Tunakomolewa.
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  HTML:
  
  
  Sasa kama hoja ni hiyo, vipi Tengeru Usa mpaka Kikatiti nao walimchagua Lema?

  Hivi hakuna sheria ya kuwadai fidia Tanesco kwa kosa la kuzima umeme makusudi?
   
 8. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  sasa kwa mawazo yao wakitunyima umeme ndo tutarudi ccm?.... naombeni namba ya mbunge wetu nimuukize kama anataarifa za hujuma hii...
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  angalau wange toa taarifa basi tujue kutakuwa na mgao mpaka lini...
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ndg zangu hakika umeme ni kero hasa huku kwe2 lain ya Sakina tangu cjui ni lini hakuna wakati 2mepata masaa 10 mfululizo umeme. Yani hawa jamaa wa Tanesco wana madharau ya hasara. Yani wana2ladhimisha kwenda kununua jenereta ya kichina sasa. Kweli umeme ni kero haswa lain ye2 ya Sakina.
   
 11. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mkuu hiyo generator mafuta utaweka ya sh.ngapi na kazi inaingiza sh.ngapi...... mafuta ndi hayo 2100 per lt sasa si utakuwa unawafanyia wauza mafuta kazi....
   
 12. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Kwa ufupi tunaomba wajitolee watu kama siyo Mh. G.Lema basi madiwani wetu ili wawatangazie wakazi wa maeneo yaliyoathirika kwa gari la matangazo ili woote twende pale Ofisi za TANESCO Mkoa tushinde hapo siku nzima tukiimba nyimbo za Ukombozi hadi pale tatizo la umeme litakapopatiwa ufumbuzi. Tunapoteza hata kile tulichokuwa tumetafuta na hiini kuongeza umaskini kwa kiwango ambacho hakijawahi onekana. wauza vinywaj baridi, wauza samaki , wafuga kuku, watu wa grills, saloon, saw mills na mashine za kusaga na kukoboa hawana mapato kabisa. Vijana waliojiajiri kurekodi nyimbo wanaocharge betri, mafundi electronics, mafundi nguo, wajaza upepo wa magari, carwash zoote hizi zinakufa na watu wanakosa ajira. Kitendo cha customer care kufanya mzaha kwa tatizo la umeme ni kudharau wananchi na inabidi tukapige kambi pale na wasitoke hata mmoja humo ndani na ikibidi wafundishwe adabu mpaka hapo watakapojua wanatakiwa watoe majibu na si ushuzi.
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Yaani imekuwa kero hii issue ya umeme hapa Arusha maana huku tunakoishi unakatika kuanzia saa kumi na mbili jioni mpaka kesho yake saa mbili asubuhi kwa maana usiku kucha hatuna umeme. Na hii imeanza toka wiki kama mbili zilizopita na hakuna taarifa wala nini
   
 14. A

  Anold JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kwa sasa mlie tu maana hamna kiongozi anayeweza kuwatetea, kipindi cha nyuma Mzee mzima angeshawapigia simu maana hakuwa anataka ishu za kijinga, lazima angemuita meneja Dodoma aeleze mgao unatokana na nini?
   
 15. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Jenereta inakula mafuta sana na ukiweka mafuta ya elfu 10 utaweka kila siku na ukijua kabisa lita ya petroli ni ghali sana. Ndugu zanguni magari yetu tunaendesha tu pale ambapo ni muhimu kufanya hivyo kwani mafuta ni ghali halafu tena umeme ndio huo unatuletea kichefuchefu.

  Tutangaziane twende kwa amani pale TANESCO na wakiona shughuli zimesimama basi akili zinaweza kuwajia na kutoa majibu yenye akili.
   
 16. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nadhani sasa hivi vibaka wa Arusha wataneemeka sana kipindi hiki.Sipati picha hapo Unga ltd na giza totoro jinsi panavyochimbika! Ngoja niwasiliane na Mganga mkuu wa Mt.Meru waongeze idadi ya nyuzi za kushonea majeraha maana vibaka wa Arusha bila kumwaga damu bado hawajakuibia.
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ni kweli kabisa kwa sasa vibaka ni wengi mbaya maana wanakata umeme usiku
   
 18. a

  andynaza Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwani lini mgao ulikwisha uko palepale poleni
   
 19. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Sakina ndo targeted area,..na hasa kuanzia maeneo ya tecnical kuja huku juu,...nafikiri wanafanya makusudi ingawa sijui lengo ni nini hasa,hili tatizo halijaanza juzi ni muda kitambo kwa sisi tunaoishi huku maeneo ya technical.
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  njoo dar uonje
   
Loading...