Kwa ufupi tunaomba wajitolee watu kama siyo Mh. G.Lema basi madiwani wetu ili wawatangazie wakazi wa maeneo yaliyoathirika kwa gari la matangazo ili woote twende pale Ofisi za TANESCO Mkoa tushinde hapo siku nzima tukiimba nyimbo za Ukombozi hadi pale tatizo la umeme litakapopatiwa ufumbuzi. Tunapoteza hata kile tulichokuwa tumetafuta na hiini kuongeza umaskini kwa kiwango ambacho hakijawahi onekana. wauza vinywaj baridi, wauza samaki , wafuga kuku, watu wa grills, saloon, saw mills na mashine za kusaga na kukoboa hawana mapato kabisa. Vijana waliojiajiri kurekodi nyimbo wanaocharge betri, mafundi electronics, mafundi nguo, wajaza upepo wa magari, carwash zoote hizi zinakufa na watu wanakosa ajira. Kitendo cha customer care kufanya mzaha kwa tatizo la umeme ni kudharau wananchi na inabidi tukapige kambi pale na wasitoke hata mmoja humo ndani na ikibidi wafundishwe adabu mpaka hapo watakapojua wanatakiwa watoe majibu na si ushuzi.