Mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Taifa ya Uandishi bunifu(TuzoNyerere) 2025 nyanja ya Ushairi Sheikh Hussein Kondo Abdallah Almaarufu Daruweshi Mkulu Wanyika atangaza neema kwa watunzi.
Ameweka chapisho lifuatalo katika ukurasa wake wa Facebook;
TANGAZO LA CHALENJI KUBWA YA WATUNZI.
Nichukue nafasi hii kuwapongeza washairi na waghani waliojitokeza katika chalenji nilizowahi kuandaa hakika kumeonekana manufaa na natija ,si hivyo tu lakini kupitia chalenji hizi ushairi wetu umezidi kushika kasi kubwa katika jamii.
Baada ya chalenji ya shairi la Rejea Ayuni nimepokea maoni mengi na maombi mengi ya washairi wakihitaji kuwepo na chalenji ya watunzi ama watungi chambilecho Profesa Ibrahim Noor,nami kwakuwa nimejitoa muhanga kupigania tasnia ya ushairi nimelipokea kwa mikono miwili na sasa natoa taarifa rasmi kama ifuatavyo;
Tutakuwa na chalenji ya watunzi ambapo mshindi wa kwanza atapata elfu hamsini kamili na mshindi wa pili atapata elfu 25.
Chalenji hii itakuwa ni kutunga shairi litakalo toa majibu ya aina yoyote kujibu shairi langu nilililowahi kutunga 29/9/mwaka Jana liitwalo Simu kuivunja ndoa,hili ni miongoni mwa Yale mashairi yangu ya visa ambayo yalitokea kupendwa na kufatiliwa sana baada ya lile ombiz kugeuzwa deni ,unayekufuru tubu na jasiri ama dhalimu.
1.Kwa hivyo kinachotakikana kwa mshiriki ni lazima ataje jina kuwa shairi hili (Fulani)ni Jawabu la shairi la Daruweshi Mkulu Wanyika Simu kuivunja ndoa .
2.Katika shairi lake atoe ufumbuzi wa nani mwenye hatia kupitia kisa hiki cha simu kuivunja ndoa.
3.Kwa Facebook anaweza kunitag,ikiwa ametuma mitandao mingine anitumie screen shot au link ya mtandao pamoja na shairi husika katika namba ya Whatsapp ±255689 969 098.Mashairi Yote Yatawekwa katika ukurasa rasmi wa Facebook wa Mtunzi unaotambulika kwa jina la Daruweshi Mkulu Wanyika.
4.Mshiriki anaruhusiwa kusambaza katika mtandao wowote iwe Facebook, Instagram, Whatsapp,x au hata tittok anaweza hata kughani hilo shairi alilotunga akiamua .
5.Mshindi ni yule atakayepata like nyingi,zitahesabiwa zilizopo kwenye Ukurasa wa mwandishi na kujumlishwa na zilizopo kwenye mitandao mingine iwe kwenye group la Whatsapp,iwe Instagram,iwe Facebook au TikTok ,au popote ambapo utatuma,kitakachohitajika ni kutuma screenshot au link kwa mtunzi,iliziweze kuonekana hizo like na kuhesabiwa.
6.Chalenji itaanza ijumaa ya kesho kutwa yaani tarehe 2/5/2025 na kutamatika tarehe 16/5/2024.Muda wote wakati chalenji inaendelea anaruhusiwa mtu kutuma shairi na kushiriki.
7.Hii ni chalenji sio shindano rasmi hivyo anaruhusiwa kushiriki mtu yoyote,na kutuma shairi la aina yoyote ile .
SIMU KUIVUNJA NDOA
Wivu kushindwa nyopoa
Metokea mfaraka
Hakika hili ni doa
Doa lisilo futika
Mapenzi likaondoa
Tama ndoa kuvunjika
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Ni mwezi ulitimia
Tangu ndoa kufungika
Mambo yakiwa sawia
Na upendo usoshaka
Hadi ilipoingia
Simu ya kujanjaruka
Yametokea chanika
simu kuivunja ndoa
Mashoga walichochea
Mke simu kuitaka
Zawadi akamgea
Wake mume kwa haraka
Asije aka nyongea
Na wenzake kumcheka
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Mume alipopekua
Ndipo jumbe kuzidaka
Zawatu asowajua
Mke wake wamtaka
Wameyatuma maua
Na katuni zakucheka
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Akamba n'takuua
Ewe usio ridhika
Kisu akakichukua
Mwili ukitetemeka
Kamkita cha kifua
Na mke kufafaruka
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Jirani wakasikia
Mwao ndani wakafika
Mke kumsaidia
Tibani kumpeleka
Huku mume kakimbia
Mjini ametoweka
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Siku ziliposogea
Mkewe amepoweka
Ndipo mume kutokea
Akiwa Mwenye mashaka
Wakwe wakampokea
Na kikao kufanyika
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Ikabidi kuongea
Ipate kufahamika
Hayo yaliotokea
Kiini kubainika
Cha ndoa kuteketea
Kwa ugomvi na talaka
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Mke akiwa alia
Huku tama ameshika
Akaanza hadithia
Chozi likitiririka
Kisa kilipoanzia
Mpaka kutamatika
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Kumbe shogaye Hadia
Simuye liharibika
Aka omba kutumia
Ya kwake kuhabarika
Nywila zake akatia
Na kuanza kuchatika
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Alipo mrejeshea
Haikupita dakika
Mumewe akarejea
Na matatizo kuzuka
Sikwamba alizoea
Mitandaoni kufika
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
Nawauliza jamia
Mnijibu kwa haraka
Ninani Mwenye hatia
Hadi ndoa kuchanguka
Yasije kujirudia
Yalotokea chanika
Yametokea chanika
Simu kuivunja ndoa
DARUWESH MKULU WANYIKA
29/9/2024
MAGOMENI MWEMBECHAI DAARUSSALAAM