Kaka hawa ndiyo hupotosha watu, huu ndiyo ufugaji wa vitabuni - hajui bei ya chakula wiki hii ni ngapi? hajui bei ya tray moja ya mayai ni ngapi kwa wiki hii?Mleta mada ni aina ya watu wanaoamini anajua kila kitu, hayupo tayari kujifunza kwa wengine lakini pia kufunza wengine, kwa ufupi mbinafsi. Au pengine tusimalize maneno, hajui namna ya kufikisha ujumbe. Moja kati ya hayo linamhusu.
Ukisoma mada yake utaona anapoint fulani, ila hajaiwakilisha kifasaha, ameandikaa juu juu tu kwa kujiamini yeye anajua na wengine wote hamjui kitu na hayupo tayari kufafanua.
Huyu ni kuachana naye tu, binafsi sina uzoefu mkubwa wa ufugaji lakini ninashauri watanzania kwny mijadala yetu tujiepushe sana kutoka nje ya mada. Yaani usipoteze muda nje ya mada kama ninavyofanya hapa. Ongelea Kuku, tetea upande unaouamini kwa hoja imara na vielelezo halisi, hiyo ni faida sana kwa wote.
Siku njema