Kama unataka kuondoka kwenye umasikini, waepuke masikini kama ukoma

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Rafiki yangu mpendwa,

Hivi unajua ya kwamba umasikini huwa unaambukizwa kama magonjwa yanayoambukizwa?

Ndiyo, hiyo ni kweli kabisa, pale unapokaa na masikini, wanakusababisha uendelee kubaki kwenye umasikini.

Huenda kwa kusoma sentensi hizo chache umejisikia vibaya, umenichukulia mbaguzi na mwenye dharau.

Sitakushangaa kwa hilo, kwani hata mimi wakati najifunza hili kwa mara ya kwanza sikulielewa haraka.
Ni mpaka pale niliposoma tafiti baada ya tafiti kwenye nguvu ya wale wanaotuzunguka na jinsi tabia inavyoweza kuambukizwa.

Kuhusu nguvu ya wanaokuzunguka, Jim Rhon alikuwa akinukuliwa mara kwa mara akisema vile ulivyo ni wastani wa watu watano unaotumia nao muda wako mwingi.

Hili unaweza kulithibitisha wewe mwenyewe, bila hata ya kutumia nguvu sana.
Yaangalie maisha yako, kisha angalia maisha ya marafiki zako wa karibu.
Angalia wana watoto wangapi, wana magari ya aiba gani, wana nyumba au wanakaa maeneo gani, kazi na/au biashara wanazofanya.

Utashangaa jinsi ambavyo mna ufanano mkubwa.
Je unadhani hilo limetokea tu kama ajali?

Hapana, kuna nguvu kubwa sana inayofanya kazi, nguvu inayohakikisha hutofautiani sana na wale unaotumia nao muda wako mwingi.

Kwa kujua hili basi, unakuwa umepata silaha ya kwanza muhimu ya kuondoka kwenye umasikini, ambayo ni kuhakikisha hutumii muda wako mwingi na masikini.

Hakikisha wale watu wa karibu kabisa kwako siyo masikini, hata kama bado hawajawa matajiri, basi wasiwe watu wanaovumilia umasikini, wawe watu wanaopambana kweli kweli kuondoka kwenye umasikini.


richvspoor6.jpg


Kwa upande wa tabia kuambikizwa, tafiti zinaonyesha tabia za watu wetu wa karibu huwa zinatuathiri moja kwa moja, hata kama watu hao wapo mbali.

Utafiti mkubwa kabisa uliowahi kufanywa wa kufuatilia maisha ya watu kwa muda mrefu (The Framingham study) umeonyesha kwamba unywaji, uvutaji na hata unene ni vitu vinavyoambukizwa.

Hiyo ina maana kwamba kama una rafiki ambaye ni mlevi, anavuta sigara au ni mnene unakuwa kwenye hatari ya wewe kuwa kama yeye.
Hata kama hukuwa na tabia hizo kabisa, kitendo cha kuwa na urafiki na mwenye tabia hizo, kinakuweka kwenye hatari kubwa ya kujenga tabia za aina hiyo pia.

Na hili siyo jipya kwenye maisha yako.
Unakumbuka ulipokuwa mtoto wakati wazazi wako wanakukataza usicheze au kuongozana na watoto wenye tabia mbaya?
Hawakuwa wanaona unafaidi sana, walijua, kupitia uzoefu kwamba haitachukua muda na wewe utakuwa na tabia kama zao.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye umasikini, ukiwa na rafiki masikini, unakuwa kwenye hatari kubwa ya wewe kuwa masikini pia.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nakushauri kama unataka kuondoka kwenye umasikini, hatua ya kwanza kwako kuchukua ni kuwaepuka masikini kama ukoma.

Rafiki, niweke hili wazi kwamba adui yetu mkubwa ni umasikini, na hivyo kuwaepuka masikini haimaanishi wao ni watu wabaya, ila tunajikinga wasituambukize umasikini wao.

Kama una ndugu yako ni mgonjwa wa ukimwi na ana kidonda, hutakigusa kwa mikono mitupu, lazima utavaa mipira ya kujikinga. Japo unampenda ndugu yako kweli, lakini kile alichonacho hukipendi, hivyo unajikinga nacho.

Na hilo ndiyo nataka ujifunze hapa, siyo uwadharau masikini, siyo uwabague na kuwanyanyapaa.

Badala yake uwaepuke, usitumie nao muda wako mwingi, usisikilize ushauri wao hasa kwenye mambo ya fedha.

Ni kwa njia hizo ndiyo unaweza kuepuka kuambukizwa umasikini ili mapambano unayoendesha dhidi ya umasikini yawe na tija.

Kitu kingine ambacho nimekuwa naksafani sana kwenye hii safari ya kuondoka kwenye umasikini ni hiki; njia bora ya kuwasaidia masikini ni kwa wewe kutokuwa masikini kama wao.

Kama ambavyo maelekezo ya kwenye ndege yanaeleza, inapotokea dharura, jipe kwanza hewa ya oksijeni ndiyo uweze kuwasaidia wengine hasa watoto.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye umasikini, huwezi kuwasaidia masikini huku na wewe ukiwa masikini.

Hivyo rafiki yangu, waepuke masikini ili utoke kwenye umasikini.
Na ukishatoka kwenye umasikini ndiyo utaweza kuwasaidia vizuri masikini hao.

Rafiki, kama bado hujaelewa namna bora ya kuwaepuka masikini, kuvunja tabia za kimasikini ulizojijengea na kujenga tabia mpya za kitajiri, nina habari njema kwako.

Habari njema ni kwamba kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, kitabu ambacho kinakupa mwongozo wa kuvunja tabia za kimasilini na kujenga tabia za kitajiri kipo tayari.

Hiki ni kitabu muhimu sana cha kusomwa na kila ambaye ameshachoshwa na laana ya umasikini na hataki tena kuendelea hivyo.

Kitabu hiki ni silaha imara ya kumshinda adui mkuu wa maisha yetu ambaye ni UMASIKINI.

Karibu sana usome kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, ujifunze kwa kina na kuondoka na silaha muhimu ya kwenda kuivunja laana ya umasikini ambayo imekuandama maisha yako yote.


huwezi-kuwaridhisha313.png


JINSI YA KUPATA KITABU.
Kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy) na nakala tete (softcopy).
Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo kwa hardcopy au kama utanunua softcopy utatumiwa kwa email.

Na kama upo nje ya Dar es salaam utatumiwa kitabu kule ulipo.
Kujipatia nakala yako ya kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI, wasiliana na namba 0752 977 170 au 0678 977 007.


20220430_075702.jpg


Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
 
ZAWADI YA KITABU.

Rafiki yangu mpendwa,
Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu, nakwenda kukupa kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI KAMA ZAWADI.

Hivyo kwa siku hizi chache utakipata kitabu hiki kwa bei ya punguzo ambayo ni tsh elfu kumi na tano (15,000/=), badala ya bei yake halisi ambayo ni tsh elfu 20
Kitabu hiki kina thamani ya mamilioni kwako, ila wewe unakipata sawa na bure kabisa, kwa tsh elfu 15 tu.

Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kukikosa, kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.

Chukua hatua sasa rafiki yangu, zawadi hii ni ya muda mfupi, bei ya kitabu itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.

Utajiri ni haki na wajibu wako, kama wapo wengine walioweza kufikia utajiri, na wewe pia unaweza kuufikia. Unachohitaji ni kuijua kanuni sahihi na kuifuata.

Kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI kina kanuni hizo, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na utajiri kwako unakuwa swala la muda tu.

Jipatie kitabu chako sasa kwa bei ya zawadi, wasiliana na 0752 977 170 kukipata kitabu popote pale ulipo.
 
Nachojua umasikini ni tabia na utajiri ni tabia. Pia ipo nguvu ya uvutano kuelekea tabia halisi. Umasikini ni negative power utajiri ni positive power. Na hizi nguvu umuathiri mtu kulingana na wingi wa nguvu husika.
 
Nachojua ktk Ulimwengu wa Roho. Wachawi wa mtaa au kijiji usiku Saa sita kamili wachawi baada ya kupigwa filimbi ya kichawi ukitana kijiweni kwao then kabla awajanza kuwanga huwa wanazunguka njia au barabara zote za kijiji au mtaa huku wakitamka na kuwanenea laana ya umasikini, magonjwa,na dhiki za KILA aina wakaazi wote wa mtaa au kijiji husika, wakimaliza ndipo uruka kuwanga na wakirudi ufanya hivyo hivyo kupiga laana kwa watu waliolala then ndipo utawanyika. So mtu yeyeto kuanzia aflajiri atakaekanyaga au tumia barabara hizo zile laaana zitamvaa kama hana nguvu nyingine ya ziada au usaidizi mwingine, thus unakuta mtaa au kijiji wote level moja ya maisha ya dhiki kama umasikini ni wote, nyumba chakavu wote, Hakuna anaefaulu iwe elimu, maisha wote level sawa, unakuta mtaa mzima hakuna hata mwenye kumudu kuweka taa nje.
Ukiona ufanikiwi mtaa fulani au eneo fulani kama huna nguvu ya ziada au usaidizi, ushauri hama. Laana ndio uleta tabia na tabia ndio uzaa umasikini. Na umasikini ndio chanzo cha mambo yote maovu.
 
Nachojua ktk Ulimwengu wa Roho. Wachawi wa mtaa au kijiji usiku Saa sita kamili wachawi baada ya kupigwa filimbi ya kichawi ukitana kijiweni kwao then kabla awajanza kuwanga huwa wanazunguka njia au barabara zote za kijiji au mtaa huku wakitamka na kuwanenea laana ya umasikini, magonjwa,na dhiki za KILA aina wakaazi wote wa mtaa au kijiji husika, wakimaliza ndipo uruka kuwanga na wakirudi ufanya hivyo hivyo kupiga laana kwa watu waliolala then ndipo utawanyika. So mtu yeyeto kuanzia aflajiri atakaekanyaga au tumia barabara hizo zile laaana zitamvaa kama hana nguvu nyingine ya ziada au usaidizi mwingine, thus unakuta mtaa au kijiji wote level moja ya maisha ya dhiki kama umasikini ni wote, nyumba chakavu wote, Hakuna anaefaulu iwe elimu, maisha wote level sawa, unakuta mtaa mzima hakuna hata mwenye kumudu kuweka taa nje.
Ukiona ufanikiwi mtaa fulani au eneo fulani kama huna nguvu ya ziada au usaidizi, ushauri hama. Laana ndio uleta tabia na tabia ndio uzaa umasikini. Na umasikini ndio chanzo cha mambo yote maovu.
Duh
 
Ambacho hujajua,
Matajiri mitaji wote wakubwa, mitaji yao Ni watu maskini.

Kuanzia wafanyakazi, bidhaa zao Hadi Bei wanazouza sokoni Ni kwa ajili ya watu maskini
Lakini pia wao kuwa matajiri hakuwazuii wengine kuwa matajiri.
Maana hata uwe tajiri kiasi gani bado utanunua chakula, mavazi n.k.
Hivyo tuache kujifariji na umasikini, hauna faraja wala manufaa yoyote.
 
Ambacho hujajua,
Matajiri mitaji wote wakubwa, mitaji yao Ni watu maskini.

Kuanzia wafanyakazi, bidhaa zao Hadi Bei wanazouza sokoni Ni kwa ajili ya watu maskini
Tajiri mmoja nyuma yake wapo masikini 200.Ila still chance ya masikini kuwa tajiri ni kubwa akiamua.
 
Masikini waliowengi huwa wanashauriana mambo ya kwenda kunywa pombe kutafuta Madanga na kuosha rungu, kudiskasi mambo ya Diamondi na Simba na Yanga.

Siku imeisha hiyo siku ya pili ni kulalamika kuwa Raisi demu hafai.
 
Matajiri wengi wazinzi tu ..hamna lolote hapo. Hiyo ni biashara ya kitabu unafanya. Utajiri ni Neema ya Mungu tu. Kuna wenye juhudi nyingi za kuupata lakini wameambulia hasara tu.
Nakubaliana nawewe 100% Suala la Utajiri linategemea na Mungu alivyokupangia Maisha yako yaweje.
Kuna watu wanaHustle litaa eg. MACHIMBON miaka pilikichi lakin mwingine anaaanza leo anapata Jiwe ananyanyuka kiuchumi vivo hivyo kwa Wakulima.
Wanalima kila mwaka lakin wakulima wachache sana wanaotoboa maisha.

Ila nimeona mdau anatupanga tununuwe kitabu chake Anasahau Mungu ndio kila kitu katk maisha.
Teh teh teh teh
 
Nimeanza kushuhudia Watu wengi wanalihama Jiji na kurudi Mikoani na Vijijini angalao huko Ugali na Mboga za Majani ni bei nafuu.

Daadeq Watu waliacha Mashamba yao na kuja kufanya Umachinga Jijini kwa kuitikia wito wa Punguwani. Imekula kwao.
 
Lakini pia wao kuwa matajiri hakuwazuii wengine kuwa matajiri.
Maana hata uwe tajiri kiasi gani bado utanunua chakula, mavazi n.k.
Hivyo tuache kujifariji na umasikini, hauna faraja wala manufaa yoyote.
Makirita Amani

Kwako kipimo cha utajiri ni kipi?

Inawezekana Bill Gates anamwona Mzee Bakhressa ni Masikini wa kutupwa
 
Back
Top Bottom