mgunga pori
JF-Expert Member
- Jul 23, 2016
- 4,093
- 4,925
Daah wanawake wanakaziii kweli kweli
Mkuu kuna wadudu anatafuna ndoa(talaka) na ugomvi wa wanandoa usioisha cjui huyu mdudu unawasaidiaje mkuuHabari wakuu!
Limezuka kundi kubwa la maelfu ya wanawake wanaokesha na kuomba kwa ajili ya kupata wenzi wa maisha. Wapo wanakesha makanisani, misikitini na wengine kukimbizana na kuku kwa kalimanzila. Hii huonyesha jinsi ndoa ilivyomuhimu kwa mwanamke.
Kuolewa ni moja ya maendeleo binafsi ya mwanamke kijamii (social development). Mwanamke hukamilika na kujitukuza kuwa yeye ni mwanamke mzuri pale aolewapo. Uzuri wa mwanamke huweza kuwa si chochote endapo umri utakuwa umesonga alafu hana mume. Mwanamke asiyeolewa hudharaulika na yeye mwenyewe hujidharau akisimama mbele ya wanawake wenzake. Wanawake wote wenye akili timamu na afya njema hujua thamani ya kuolewa.
Ewe mwanamke kwa ulimwengu usipokuwa makini utaambulia kuzalishwa na kuachwa hapo. Kama hiyo haitoshi utaishia kuwa mke wa pili au wanne. Hivyo kuna mambo muhimu lazima ufanye ili nawe uwe miongoni mwa wanawake wenye wanaume zao.
Mambo yafuatayo ni muhimu kwa karne hii ili upate kuolewa:-
Yote juu ya yote, fanya kazi upate mwanaume anayeeleweka na mwenye kazi. Vinginevyo utaishia kucheza nage.
- Hakikisha unakazi: Hii ndio nguzo ya kwanza kwa karne hii kwa mwanamke ili apate tiketi ya kuolewa. Hakuna mwanaume mwenye kutaka maendeleo atakayetaka kuoa mwanamke aliyekaa bila kujishuhulisha. Tafuta hata kazi ya kijungu jiko, ususi au ushonaji. Sio kwenda kuomba kwa waganga wakienyeji na makanisani wanaume wenye kazi wakati wewe huna. Wanaume tupo makini sana hasa kwenye ishu ya uchumi tunapohitaji wenza wa maisha. Kigezo hiki ndio kigezo namba moja kwa karne ambacho hufungua macho ya wanaume kuona sifa nyinginezo za mwanamke amtakaye kama mke. Dada zangu naomba mnielewe vizuri, ukitaka kuolewa mapema bila maombi makali basi jishuhulishe lakini ukitaka cha uvunguni basi lazima utainama.
- MALIZA NGOME: Akija mwanaume ambaye unahisi kumpenda basi tumia akili nyingi sana. Ikiwezekana shirikisha wazazi wako indirect wakupe mbinu. Usione aibu kuhangaikia kitu ukipendacho. Maliza ngome ya umpendao. Ngome ni watu wa karibu wa mwanaume hasa Mama Mkwe wako. Kisha unamaliza na ngome kuu ambayo ni Mungu. Hakikisha unamshawishi na kuonyesha haja na nia ya dhati. Ukimuomba Mungu basi kila kitu kinakuwa sawa. Huko kwa Mama mkwe unamtumia vivocha, vitenge na vitu vidogo vodogo. Uone kama hutatikisa nyavu. Kwa Mungu napo unatoa sadaka na zaka. Hapo umemaliza mchezo. Ndio maana nikasema lazima ujishuhulishe ili upate vijihela.
- Tumia mali: Usione aibu kumhonga mwanume. Mpe hela na vijizawadi vya hapa na pale. Kama umefungua mgahawa basi muongezee chakula na madiko diko. Onyesha kuwa unaweza timiza kauli ya kusaidiana. Wanawake wengi wanaotumia mbinu hii hufanikiwa kutikisa nyavu za ndoa na kuchukua point tatu. Hata wanaume wanapenda kupewa vitu. Usitake kupewa kila siku. Akikupa nawe unampa yaani bampa tu bampa. Ndio maana nikasema lazima uwe na kazi ya kukuingizia kipato.
- Jipendekeze: Usisubiri kupigiwa, piga simu na usitume tafadhili nipigie. Wakati wewe unasubiri umtakaye akupigie wenzako wanampigia, tena wengine wanafika mbali zaidi kwa kumtumia vocha ikibidi kumtumia picha za uchi. Kama hujipendekezi lazima utasota. Sio kwenye mapenzi tuu hata katika maisha ya kawaida. Ukijifanya huna shobo utaishia kulia lia maisha magumu. Hakuna aliyefanikiwa bila kujipendekeza. Kumbuka: Huwezi jipendekeza kwa mwanaume kama huna hela utaishia kuonekana malaya ndio maana nikasema fanya kazi upate vipesa mshenzi
- Kuwa Msikivu na Mtiifu: Mwanaume hujiona kidume akiheshimiwa na kutiiwa na mwanamke. Ukiwa kwenye mahusiano usipende kujipandisha na ubishi usio na maana. Jifanye mtiifu hata kwa kuigiza ili mbuzi wako aingie zizini. Wanaume tunajivunia kuheshimiwa na wake zetu kuliku uzuri wao. Uzuri unazoeleka lakini heshima haizoeleki. Uzuri unaisha lakini heshima na utii vinadumu. Ukimtii mwanaume uwapo kwenye mahusiano lazima moyo wake utakufikiria tuu kama yupo vizuri kichwani.
- Kauli: mwanamke lazima uwe na kauli nzuri. Kauli huumba. Kwa wanaume wenye akili hujua umuhimu wa kuoa mwanamke mwenye kauli nzuri. Ukiwa na kauli nzuri na maneno yenye staha utaolewa kwa urahisi tuu. Huna haja ya kufunga na kuomba wala kwenda kutoa mbuzi wa kafara.
- Mavazi na Urembo: Mwanamke lazima uvae mavazi masafi na kuvutia. Wanaume huvutiwa na mavazi na urembo wa wanawake. Ukiwa na sifa zote huko juu ukimaliza na hii basi kuolewa ni asubuhi kabisa.
Nawasilisha
Unawadanganya mabinti na upuuzi wako...hizo zote hakuna sabb hata moja ya kumvuta mume wa ndoa...Habari wakuu!

Unapimaje U-smart wa mtu?