Kama unamuamini Mungu na huamini haya mambo matano ni afadhali uache kumuamini au uanze upya

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,591
15,387
1. Miujiza
Miujiza na uwezo wa Mungu kufanya kitu ambacho kibinadamu hakiwezekani. Mfano Kufufua mtu aliyekufa, kutembea juu ya maji, kupasua bahari, e.t.c kama huamini miujiza humiamini Mungu. Ni afadhali uache kuamini uungane na wapinga Mungu au uanze upya.

2. Kiyama cha dunia hii
Hii namaanisha Hii dunia itafungwa, kila kitu kitachomwa, Mungu atawachukua wanaomuamini kipitia Yesu, atakaa nao miaka 1000 mbinguni kisha atatengeneza dunia mpya atatuweka hapo na yeye atakaa na sisi live milele zote. Kama huamini hili, upeo wako umeishia kwenye haka kadunia mufirisi tu bado humuamini Mungu.

3. Uwezo wa Mungu kufanya jambo papo hapo
Namaanisha jambo ambalo lingechukua miaka 100 kufanywa kwako ndani ya sekunde. Kama huamini hili humuamini Mungu. Unamuwekea mipaka. Unapoingia ibadani amini anaweza kukufanyia kitu kikubwa kuliko unavyofikiri na kuomba papo hapo bila kujali michakato ya kidunia inavyosema.

4. Kama ni mkristo, basi wewe umeshakufa siku Yesu alipokufa
Uhai ulionao unao katika kristo. Ukimuacha Kristo umeacha uhai na kurudia kifo chako. Uhai ulio nao katika kristo hakuna mtu, taasisi, serikali au kikao au uchawi unaweza kukuchukulia uhai ulio nao katika kristo. Kama hauamini hivyo bado humuamini Mungu. Hivyo mkristo hazungumzii kifo anazungumzia uhai. Hata ukilala haka kauzingizi ka muda tunakaita kifo, ni mapumziko tu ya muda mfupi ili siku ukiamshwa ule mema ya milele. Hii itakupa amani sana.

5. Wewe ni mtoto wa Mungu wa kuzaliwa
Mali zote za Mungu unahaki nazo na ni zako. Hivyo wewe ni mtoto wa anayemiliki sio dunia tu bali matrillioni mara trillioni ya mali na sayari zenye viumbe na mali zisizohesabika. Wewe ni mtoto wa kifalme. Mungu wako sio masikini. Hata akizuia usipate kitu sasa ili usijekupotoka kwa namna anavyokujua, unaendelea kuamini amekutunzia vyako hivyo huna wasiwasi na suala la uchumi na pesa.

Kama bado huabudu kisa unatafuta maisha, hujaanza kumuamini Mungu.

Asanteni, ni hayo tu kwa leo.

Matunduizi wa JF.
 
Back
Top Bottom