❗️❗️Kama unamiliki hisa za Benki hakikisha uanaelewa hizi ratio mbili muhimu: CIR & NPL.❗️❗️

❗️❗️Kama unamiliki hisa za Benki hakikisha uanaelewa hizi ratio mbili muhimu: CIR & NPL.❗️❗️

Joined
Aug 26, 2022
Posts
64
Reaction score
119
🔎 Unapowekeza kwenye hisa za benki, kuna vipengele vingi vya kuzingatia. Lakini kwa mwekezaji makini, kuna ratio mbili muhimu zinazopima ubora wa biashara ya benki:

1️⃣ NPL – Non Performing Loans (Mikopo Chechefu)
Hii hupima ubora wa mikopo inayotolewa na benki. Kadri kiwango kinavyokuwa chini, ndivyo mikopo mingi inavyolipika na hatari ya hasara inavyopungua.
➡️ Miongozo ya BOT: Benki inapaswa kuwa na NPL chini ya 5%.

2️⃣ CIR – Cost to Income Ratio (Uwiano wa gharama kwa kipato)
Hii hupima ufanisi wa benki katika kutumia gharama zake za uendeshaji. Kadri CIR inavyokuwa chini, ndivyo benki inavyofanya kazi kwa tija zaidi.
➡️ Miongozo ya BOT: Uwiano huu unapaswa kuwa chini ya 55%.

📊 Mfano wa matokeo ya robo ya pili ya mwaka (Q2):

■ CRDB Bank → NPL 3%, CIR 43%
■ NMB Bank → NPL 3%, CIR 38%
■ MKCB Bank → NPL 3%, CIR 44%

✅ Hii inamaanisha benki zote tatu ziko salama na zinaendeshwa kwa ufanisi kulingana na viwango vya BOT — jambo linaloweza kuwapa wawekezaji imani zaidi.

GODFREY DENIS
0763 721 523 (WhatsApp)

Link:
View: https://www.instagram.com/p/DNlcq-uomf8/?igsh=MTczcnB1NDB1b2dmaQ==
 
Kwa sasa DCB haifanyi vizuri kibiashara - ila ndani ya miaka ijayo wanaweza kufanya vizuri. Kwa sasa unaweza kupata faida ya ongezeko la mtaji, lakini kuhusu gawio inabidi uvumilie kidogo. Kutokana na muongozo wa BOT hili benki itoe gawio inabidi NPL (Mikopo chechefu) iwe chini ya 5% na CIR (Uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato) iwe chini ya 55% — ukiangalia taarifa za DCB bado hizi ratio zipo juu sana.
 
Back
Top Bottom