Kama Uchaguzi Mkuu Ungefanyika Leo...


Naona bado hujaacha tabia yako ya kuipiga vita CUF popote pale unapopata nafasi. Unadai nguvu hizo za mwaka huu haziwezi kulinganishwa na za mwaka 2005. Je hamkuwa nyinyi waandishi wa habari mliokuwa mnatuambia mwaka 2005 kuwa mpambano wa urais ni kati ya Kikwete na Mbowe tu na kumtoa kwenye kinyang'anyiro Lipumba? Sasa leo mnakuja na hoja kuwa alikuwa na nguvu mwaka 2005 ila mwaka huu ndiyo hana nguvu kama ile ya mwaka 2005? Sasa nikuulize vigezo vipi ama takwimu zipi ulizozitumia kufikia hitimisho kuwa Lipumba 2010 hana nguvu kama wa 2005?

Nimekuwa nasisitiza kote huko kuangalia matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana. Uchaguzi uliofanyika miezi 11 tu iliyopita na matokeo yake yanaonyesha kuwa CUF imeongeza viti mara 3 ya vile walivyopata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2004. Sasa nyinyi mnaojifanya magwiji wa siasa mnaweza mkatueleza vipi na kwanini miezi 11 CUF ifanye vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ila baada ya miezi 11 hali ikabadilika ghafla? Nakuomba utumie vigezo vinavyoambatana na takwimu siyo hizi kelele za sijui nani "kabadilisha upepo wa kisiasa". Kwangu mimi hizi zote ni b.s. at it's best.

Je unaweza ukatueleza hizo ni "nyakati" gani ambazo CUF inaonekana kuwa chama rafiki wa CCM? Vigezo vipi umevitumia kama siyo kuendeleza mawazo na propaganda ya Chadema?
 


:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13: Mkuu maggad naona wewe umeogwa na CCM

Yangu macho
 
Hoja yangu nimeihamishia kule kwenye uwanja wa Siasa..
 
Bw. Mjengwa sasa uzalendo umekushinda, umeamua uwe muwazi juu ya ukereketwa wako kwa jk na chama chake. Kwa sisi watu makini, tulikubaini mapema tangu jk alipoingia madarakani. Hata uandishi wako umebadilika sana. Najua umetumwa na unalipwa ujira kwa uandishi wa kipropaganda huo. Lakini ninataka nikuhakikishie kwamba hata silaha za aina hiyo inafika mahali zinashindwa mbele ya vuguvugu la wananchi kutaka mabadiliko. Wewe endelea kula hela ya mafisadi na uvimbiwe na ole wako mageuzi yatakapotokea nchi utailaani kalamu yako kama watakavyofanya akina Salva na Muhingo Rweyemamu.
 
BWANA MJENGWA,

HIVI WEWE HUKUPATA KUAMBIWA KUWA UKITAKA KUWEKA HOJA HUMU NI SHURTI IWE ILA INAYOWAPENDEZA KWENYE MASIKIO YA WANA-CHADEMA? Sasa swali langu haya mabandiko ya kusifia Chadema sijui ndiyo yataongeza kura kwenye sanduku la kudumbukizia kura siku ya uchaguzi ama what is the logic behind the wasted energy? :tonguez:
 
Nimemwandikia mhariri wa mtandao huu ( JF) kumwomba abadilishe title ya thread hii; " Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?". ( Kule kwenye jukwaa la habari za uchaguzi mkuu)

Hata kama title ya thread imewekwa katika mtindo wa swali bado jibu la swali hilo ninalo, kuwa HAPANA.

Niko Iringa na naendelea na kazi zangu za kila siku katika ajira yangu. Baada ya kazi niko na familia yangu, kazi za kublog na shughuli nyingine za kijamii. Sijajihusisha kwa namna ye yote na kampeni za siasa, iwe Udiwani, Ubunge na Urais, kwa mgombea ye yote na Chama cho chote kile, iwe katika chaguzi zilizopita na hata uchaguzi wa mwaka huu. Anayeweza kuthibitisha kinyume chake aje.

Watu wana uhuru kuchangia maoni yao hata kama wanafikiria hivyo. Lakini kuweka title katika mtindo huo kunaweza kuwafanya wengine waamini ndio ukweli wenyewe.

Ni matumaini yangu mhariri wa JF atatanguliza uungwana na kubadilisha title hiyo ya thread hii. Inanipa usumbufu, mimi na hata familia yangu, kwa vile haina chembe ya ukweli.

Natanguliza shukrani.
 
Maggid,
nilikuta jana kuna thread umeanzisha kulalama kuhusu kupopolewa hoja yako hii uliyoianzisha. mimi nikakujibu kwa mtazamo wangu hasa yale niliyoyaona kwenye hoja zako na bila kusahau mtazamo wako HURU. ila pia unajitahidi kujinasua kutoka ktk kundi la kumkampeinia JK ingawa ulishaanza zamani sana. Kumbuka in 100 days alizokaa kikwete madarakani wenye macho tulishaanza kuona kukengeuka kwake kuacha ile misingi aliyoihubiri ktk kampeni 2005. lakini wewe hukuona hiyo kitu na ukaendelea kumwaga sifa kwake. na alipotimiza miaka mitatu madarakani niliinasa hiyo post yako hapo chini ukielezea jinsi alivyofanikiwa na hukueleza mabadiliko ya kushuka kwa kiwango cha utendaji na kimajukumu kwa yeye na wasaidizi wake dhidi ya wananchi. Nahisi wewe umeshalipiwa bill ya kila bidhaa ndo maana huoni mfumuko wa bei, uhaba wa huduma n.k.
Naomba nikutukane tena kwa kuweka hii makala yako hapa jamvini

 


Mkuu Msanii, asante - hii ndiyo maana naipenda JF na huwa nawaonya rafiki zangu wawe waangalifu sana wanapotoa maoni yao humu ndani kwani yanaweza kuja kukusuta baadaye. Huyu Maggid sijui kama ameona mapokezi aliyoyapata Dr. Slaa mjini Iringa leo na kama ameyaona bado atatetea msimamo wake ambao ana jeuri ya kuuita tathmini kumbe ni kumpigia debe Kikwete, aiyemwona kama tumaini la Watanzania. Siamini kuwa huyo Jakaya Kikwete anayemwongelea Maggiid ndiye huyu huyu mwenye jeuri ya kusimama jukwaani kuwanadi wezi na wahujumu uchumi wa taifa letu. Hata hivyo sasa baada ya kulisoma hilo bandiko lake la miaka ya nyuma, sidhani kama nitendelea kuchangia tena katika hizi mada zake zisizo na kichwa wala miguu.
 
Mkuu umepiga msumari wa mwisho.
Mtu anakuja na majibu mepesi kuhusu masuala magumu yahuyuso nchi. Hawa wenzetu wanaolipwa kwa kufanya kazi za kupangusa viatu vya watawala wanasahau kwamba hata mtu aoge vipi hawezi kuutakatisha moyo wake. Dawa ni kukiri na kuomba radhi na siyo kuendelea kuukumbatia UJINGA.
Kula thenksi mkuu.
 
Kudakeki,
Na wewe unaweza kuanzisha jukwaa lako ambako mtajadilia mapenzi yenu kwa CCM na Kiwete. Hakuna anayewazuia. Hakuna cha wasted energy hapa!
 

kwani ulipotoka RAI NGUVU YA HOJA habari za kuandika udaku uliacha? unapokuwa unaogwa na RA
NAHISI UTAKUWA UNAKALIBIA KUZAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…