With all due respect Mjengwa, sikubaliani na findings zako. Kigezo gani ulichotumia kufikia hiyo conclusion kuwa ccm watashinda? Hii ni ccm ya JK siyo CCM ya JKN. Kama watanzania hawajaona hilo, basi ni kuhalalisha ccm itawale milele. Hii ni ccm iliyofuta Azimio la Arusha, iliyoondoa misingi yote ya baba wa Taifa, kuwa cheo ni dhamana, rushwa ni audi wa haki, na binadamu wote ni sawa. Hii ni ccm tunayoambiwa kuwa elimu kutolewa bure haiwezekani. Wote tunafahamu, tukiwemo wewe na mimi, na JK na mawaziri wake wengi ambao tulikuwa nao mashuleni na vyuoni enzi za Mwalimu, kuwa tulisoma bure kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu. Hatukulipa ada, hatukulipia vitabu, wala madawati. Na hatukuwa na tuition ya baada ya shule. Waalimu wetu waliwajibika ipasavyo, mitihani haikuibiwa na wanafunzi walifaulu kwa kiasi kikubwa. Iliwezekana wakati ule, haiwezekani leo. Wakati kila mmoja wetu anafahamu kuwa Tanzania ya leo imeendelea zaidi kuliko wakati ule, nadhani hata kirasilmali na uwezo wa kuzitumia kwa makini zaidi sasa tunaweza zaidi. Tanzania ya leo inao wataalamu wengi zaidi wa kila fani, hata wa kuweza kuishauri serikali vizuri zaidi tunao. Wataalamu wazawa, sio wa kigeni wapo kwenye kila fani. Kama bado tunaifagilia ccm, pamoja na kuwa upeo wetu umeendelea kuliko miaka mitano iliyopita, ni kuisaliti nchi yetu. Watu wa vijijini wanaweza kuwa hawafahamu kama ccm siyo CCM. Lakini ni jukumu letu wewe, mimi na yule kuwaeleza hivyo, ili wafanye uamuzi wenye busara, utakaoweza kuikomboa nchi yetu. Mwalimu aliwahi kusema, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Mtu yeyote anayefikiria ccm ni baba yake au mama yake ni msaliti wa watanzania. Mjengwa una nafasi nzuri sana ya kuwaelimisha watanzania kupitia blog yako. Unaweza kuwaelimisha hata watu walioko huko vijijini ambako mara nyingi huwa unatuletea picha za matukio mbalimbali. Kwa maoni yangu unachokifanya hapa ni kupigia debe mafisadi na washirika wao, ambao hawaitakii mema nchi yetu.