CUF: Chama cha Wananchi
Katika hali ya kushangaza, CUF ( Bara) safari hii kinaonekana zaidi kuwa jokeli katika karata za kisiasa. Profesa Ibrahim Lipumba bado anaonekana kuwa na nguvu katika kanda ya Pwani na mikoa ya kusini. Lakini, nguvu hizo haziwezi kulinganishwa na za katika uchaguzi mkuu uliopita. Profesa Lipumba aliyeanza kuwania Urais tangu 1995 sasa anaonekana zaidi kuwa ni mtu anayepita kuwaaga Watanzania kuliko kuomba kura zao.
Na kuna wakati, CUF wanaonekana kama Chama Rafiki na CCM kuliko chama cha upinzani. Na laiti urafiki huo wa kisiasa ungekuwa kati ya Profesa Lipumba na Dk Slaa, basi, mgombea Urais wa CCM angekuwa na kibarua kigumu zaidi, lakini si kwa sasa, siku 45 kabla ya Oktoba 31. Ninapoandika fikra hizi huru. Urafiki huo wa CCM na CUF unaweza pia kumgharimu mgombea wa CCM, Rais Kikwete na kujikuta akigawana kura na Profesa Lipumba na si kura za upinzani kugawanywa. Hilo linaweza kutokea na kuwashitua CCM.
Jumapili, Septemba 12, 2010.
Na Maggid Mjengwa,
HUU ni mjadala niliouanzisha kule kwenye jukwaa la Jamii (www.jamiiforums.com). Nauendeleza hapa ili uwafikie wengi zaidi.
Ni tathimini yangu. Ni mtazamo wangu huru. Katika kuishi kwangu kuna chaguzi nilizozishuhudia kwa macho na nilizosoma vitabuni. Hivyo, ninachoandika kinatokana na uzoefu wangu wa kufuatilia kwa karibu mienendo ya chaguzi zetu.
Naam. Zikiwa zimebaki siku 45( Leo Jumatano, Septemba 15, 2010) naiona hali ifuatayo kama uchaguzi ungefanyika hii leo;
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Mrisho Kikwete angeibuka mshindi . Dk Wilbroad Slaa ( CHADEMA) angechukua nafasi ya pili na huku Profesa Ibrahim Lipumba ( CUF) akishika nafasi ya tatu. Wagombea wa vyama vilivyobaki wangekuwa wasindikizaji kwa kupata chini ya asilimia 5 ya kura zote kwa pamoja.
Hali hiyo ingeakisi pia matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani ( Bara). Tafsiri yake; Jakaya Mrisho Kikwete angeunda Serikali huku yeye na chama chake wakikabiliwa na changamoto kubwa kutokana na upinzani utakaokuwa umeongezeka nguvu ndani na nje ya bunge kutokana na ujio wa Dk Slaa kama mgombea Urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Ni dhahiri kuwa Chama Cha Mapinduzi baada ya Oktoba 31, kinatakiwa kijipange upya kuikabili hali mpya katika uwanja wa kisiasa. Viashiria vya jamii inayotaka mabadiliko vimeshaonekana. CCM itakuwa na mawili ya kuchagua; kuchukua jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo au kusubiri kuzamishwa na mkondo wa maji ya mabadiliko hayo.
CCM ianze sasa kufikiria namna itakavyounda Serikali miaka ijayo kwa kushirikiana na vyama vingine. Ifikirie pia uwezekano wa kuwapo Serikali ya Mseto hata Tanzania bara. Ndio, kutoa fursa kwa chama au vyama pinzani vitakavyokuwa na idadi kubwa ya wabunge kushiriki kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Na hakika miaka mitano mpaka kumi ijayo, tutakuwa na Tanzania tofauti na ya sasa. Na mtaziona ishara. Kauli za Kidumu Chama Cha Mapinduzi! Na CCM Daima! Zitaonekana na wapiga kura kuwa ni za waliopitwa na wakati. Hiki ni kizazi kipya na dunia imebadilika.
Kwa hali ilivyo kwa sasa, CCM wanajivunia:
Kuwa ni chama kikongwe, kikubwa na kilichotawala kwa muda mrefu. Kuna hata wanaokipigia kura chama hicho Kwa mazoea tu. Na katika nchi zetu hizi; kukiondoa chama kilicho madarakani, Chama kilichopigania uhuru au kinachotokana na chama kilichopigania uhuru ni kazi ngumu sana. Kwa anayetaka kufanikiwa katika hilo, anahitaji kwenda ilipo mizizi ya chama hicho. Ni vijijini. Na huko vijijini kwa leo hii chama wanachokijua ni CCM. Naam. Ndio Zimwi wanalolijua.
Mwanakijiji atatembea kwa miguu kilomita kumi kwenda kuhudhuria mkutano wa CCM. Atakwambia amepewa taarifa ya mkutano na Balozi wake wa Nyumba Kumi. Hivyo basi, CCM wanajivunia mtandao wao wa kichama kuanzia ngazi ya Balozi wa Nyumba Kumi, shina, tawi na kuendelea. Na hata mtandao wa Kiserikali.
Na hakika, mara zote ni vema na ni busara kusema yaliyo kweli na tunayoyaamini, hata kama ukweli mwingine unahuzunisha, ni vema ukasemwa. Kuufumbia macho ni sawa na kuogelea kwenye mapovu wakati maji yapo.
Udhaifu wa CCM:
Pamoja na kuwa ni chama kikongwe na chenye uzoefu, wakati mwingine inashangaza kuona katika maeneo kadhaa kinavyoshindwa kusoma alama za nyakati. Kura za maoni ni mfano wa udhaifu wa CCM kushindwa kubaini kuwa kwa utaratibu mpya ulijiojiwekea katika kupata wagombea walisahau umuhimu wa kuyapitia na kuyachuja majina ya wanachama wake waliotangaza nia ya kugombea na kuchukua fomu kabla ya kuyapeleka kwa wanachama wake kupigiwa kura za maoni.
Badala yake, CCM iliacha wanachama waamue halafu bado chama nacho kikaingilia kati kuamua tena. Kuna adhabu ya chama kutoka kwa wanachama wake inakuja kutoka katika baadhi ya majimbo. Kwa utaratibu uliotumika sasa, wanachama wa CCM huko tuendako wanaweza kujikuta wakiwapigia kura za maoni wagombea wenye fedha chafu zinazotokana na shughuli haramu. Na kinachojitokeza zaidi sasa ni kubadilika kwa mwenendo wa wapiga kura. Kidogo kidogo wapiga kura wameanza kuangalia zaidi watu na si chama. Ni kwenye ngazi ya udiwani na ubunge. Hizi ni dalili mpya za kubadilika kwa mwenendo wa wapiga kura. Kwamba mtu kwanza, ilani ya chama baadae.
CHADEMA: Ujio wa Dk Slaa:
Sio tu umewashangaza CCM na mgombea wake urais, bali pia unaonekana kuwashangaza CHADEMA wenyewe wanaoonekana kutokujiandaa na namna Dk Slaa alivyopokewa na wananchi. Na kama ilivyotabiriwa na Mwalimu, CHADEMA inaonekana kuwa ndio chama cha upinzani chenye nguvu na chenye nafasi ya kuipoka CCM mamlaka ya kuongoza dola endapo CCM kama chama haitafanya juhudi za makusudi za kufanya mabadiliko ya kimsingi yatakayoonekana na wapiga kura.
Udhaifu wa CHADEMA
Unajidhihirisha kwenye eneo la oganaizesheni na kifedha. Bado CHADEMA haina uwakilishi mpana katika ngazi za mashina na matawi. Dk Slaa anaweza kutua na helikopta Pawaga, Iringa. Lakini, mara ile akiruka, huku nyuma hakuna watendaji wa CHADEMA wa kufanya kazi ya CHADEMA. Kuna taarifa pia za wagombea wake ubunge na udiwani wa CHADEMA kukosa nguvu za kifedha kuendesha kampeni . Taarifa hizo zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari haziwezi kupuuzwa tu. Hapa inahusu udhaifu katika maandalizi. Kuna wagombea wa CHADEMA watakaoanguka katika chaguzi kwa tatizo hilo.
Zitto Kabwe:
Huyu ni kada nyota ndani ya CHADEMA. Hata hivyo, sarakasi zake za kisiasa huenda zinachangia kukidhohofisha chama chake kuliko kukipa nguvu. Majuzi hapa aliripotiwa na magazeti kutamka hadharani kuwa anajiandaa kugombea urais 2015. Zitto Kabwe anaacha maswali; Kulikoni ndani ya CHADEMA? Je, Dk Slaa ni mgombea wa msimu tu? Au ndio sababu Zitto Kabwe hakuhudhuria Mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CHADEMA pale viwanja vya Jangwani?
Inachojivunia CHADEMA:
Bado ni chama kinachoonyesha kuwa na mvuto kama kitajipanga vema. Kesi iliyofunguliwa Mahakamani dhidi ya Dk Slaa kuhusiana na masuala binafsi ya mahusiano inaonyesha kumtangaza na kujenga zaidi Dk Slaa kwa wapiga kura wanaotia shaka wakati uliotumiwa kuibuliwa kwa suala hilo. Kuna watakaompigia Dk Slaa Kura za Kumhurumia.
Umakini wa CHADEMA:
CHADEMA imekuwa ikijinadi kama chama makini machoni mwa wapiga kura. Hata hivyo, taarifa zilizoripotiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu , CHADEMA, Zanzibar Hamad Yussuf huenda akaondolewa kwenye timu ya kampeni ya Dk Slaa kwa kuwa amekuwa kero inaonyesha namna timu ya kampeni ya CHADEMA ilivyoshindwa kubaini mapema, Hamad Yussuf alikuwa kero kwa wapiga kura. Maana, kwa utamaduni wa Watanzania, namna Naibu yule Katibu Mkuu alivyokuwa akimfananisha Dk Slaa na Bwana harusi na kauli nyingine pale viwanja vya Jangwani ilikuwa ni matusi hata kama kuna waliotaka kupewa tafsiri sahihi ya neno hilo. Ni heri kwa CHADEMA wameamka na kubaini kero hiyo ndani ya nyumba yao.
Kauli na Ishara:
Kama hakuna aliyelifikiria hili ndani ya CHADEMA, basi, hata kama CCM wanaimba Wapinzani tuwalete , tuwakatekate , hilo ni kosa ambalo halipaswi kujibiwa na kufanya kosa lingine, Ni pale viongozi wa CHADEMA wanapotamka maneno ya Kiingereza; Peoples . Power! Huku wakiamrisha wafuasi wao kusokota ngumi . Kitendo hicho kinatoa ishara mbaya kwa mpiga kura wa kawaida. Bado kuna Watanzania wengi waliopokea maelekezo ya tangu enzi za Mwalimu kuwa; Tujiadhari na wanaotaka kutusababishia vita na mapigano katika nchi. Kukunja ngumi ni ishara ya kujiandaa kupigana. Kuna kura zinazokimbia kutoka CHADEMA kwa ngumi hizo.
CUF: Chama cha Wananchi
Katika hali ya kushangaza, CUF ( Bara) safari hii kinaonekana zaidi kuwa jokeli katika karata za kisiasa. Profesa Ibrahim Lipumba bado anaonekana kuwa na nguvu katika kanda ya Pwani na mikoa ya kusini. Lakini, nguvu hizo haziwezi kulinganishwa na za katika uchaguzi mkuu uliopita. Profesa Lipumba aliyeanza kuwania Urais tangu 1995 sasa anaonekana zaidi kuwa ni mtu anayepita kuwaaga Watanzania kuliko kuomba kura zao.
Na kuna wakati, CUF wanaonekana kama Chama Rafiki na CCM kuliko chama cha upinzani. Na laiti urafiki huo wa kisiasa ungekuwa kati ya Profesa Lipumba na Dk Slaa, basi, mgombea Urais wa CCM angekuwa na kibarua kigumu zaidi, lakini si kwa sasa, siku 45 kabla ya Oktoba 31. Ninapoandika fikra hizi huru. Urafiki huo wa CCM na CUF unaweza pia kumgharimu mgombea wa CCM, Rais Kikwete na kujikuta akigawana kura na Profesa Lipumba na si kura za upinzani kugawanywa. Hilo linaweza kutokea na kuwashitua CCM.
CHANZO: Raia Mwema
========================================================
Originally Posted by Majid Mjengwa
NAENDELEA na tathmini yangu binafsi ya miaka mitatu ya Uongozi wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete.
Naam. Linapotokea jambo jema na zuri katika nchi, basi, ni vizuri jema hilo likaelezwa, vivyo hivyo kinyume chake. Kubwa kabisa linalotokea sasa ni ukweli kuwa Watanzania wameanza kurejewa na imani na uongozi wa juu pale wanaposhuhudia baadhi ya ‘vigogo' wakifikishwa mahakamani.
Hata kama ni chache kwa sasa, lakini hizi ni hatua za maana za uongozi wa Awamu ya Nne. Kwa Jakaya Kikwete, huu ni mtaji wa imani anaoanza kuuwekeza kwa umma. Kwa mwendo huu, mtaji huu unaweza kulipatia taifa mavuno makubwa, pengine si katika awamu yake, bali kwa awamu zijazo.
Katika kutathmini miaka mitatu ya Jakaya Kikwete madarakani bado nitarudi nyuma alikoanzia, maana huko nilipata pia kuandika fikra zangu kwa jinsi nilivyomwona akiianza awamu yake. Nilikuwa Bagamoyo siku tatu kabla ya Jakaya Kikwete kuhutubia Bunge la kwanza la Uongozi wa Awamu ya Nne, Desemba 30, 2005.
Nikiwa Bagamoyo nilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wananchi, kusikia maoni yao juu ya mtu huyu, Jakaya Kikwete. Nilitaka kupata maoni ya watu wa kawaida juu ya matarajio yao kwake.
Nakumbuka kuzungumza na kijana mwuza ‘chipsi' pale sokoni Bagamoyo. Huyu aliniambia; " Braza, Jakaya huwa anapita hapa kwa miguu akienda nyumbani kwake. Na kichochoro anachopita hiki hapa. Ukimaliza kichochoro hiki nyuma hapo utaukuta mti wa mkungu, mbele kidogo kuna kiwanja cha watoto, nyumba yake inaonekana kwa mbele".
Watu kadhaa walinipa simulizi zenye kufanana juu ya Jakaya Kikwete aliye karibu na watu. Jakaya waliyezoea kumwona akikatisha mitaa ya Bagamoyo kwa miguu na kuzungumza na wananchi. Kwa namna moja au nyingine, simulizi hizi zilionyesha ni kwa jinsi gani mtu huyu Jakaya Kikwete asivyo na makuu.
Na hakika, kiongozi wa watu hatakiwi awe mtu mwenye makuu, mbinafsi, mwenye tamaa ya mali na fisadi. Na katika hili la kuwa upande wa wananchi, Kikwete, kama mtu aliyekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kushika nafasi ya ukuu wa nchi, naamini amesoma kwa kina maandiko ya wanafalsafa mbalimbali kama vile Niccolo Machiaveli na hata Plato.
Na kwa kupitia maandiko ya Machiavelli, " The Prince", yaani, "Mwana Mfalme", Kikwete ana mengi ya kujifunza . Machiaevelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kupata utawala. Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yao kutimiziwa.
Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine. Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa Mwana Mfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maadui wachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, na hapa ni wananchi.. Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan. Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia milango.
Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya wengi.
Katika ubinafsi wa viongozi wetu, kiongozi wa Kiafrika, mara nyingi hapendi kukosolewa. Hana busara ya kutambua, kuwa, hakuna mwelevu wa kila jambo, kwamba sote hatujakamilika, tuna mapungufu yetu. Kwa kiongozi wa staili hii, akitamka jambo, basi hakuna wa kufikiri jingine. Fikra zake siku zote ni sahihi.
Plato, mwanafalsafa wa Uyunani ya kale anasema; katika nchi, kiongozi wa namna hii, hufikia kukoma kuwa kama wanadamu wengine, hugeuka mbweha. Atawaandama "wapinzani" wake. Wengine atawaua kwa kuwapachikia mashitaka batili, na wengine atawalazimisha kwenda kuishi uhamishoni.
Haya ni masuala ya kimaadili. Katika machapisho yake ya "Republic", yaani , "Jamhuri", Plato anazungumzia kwa kina juu ya ubinafsi na maadili. Je, kuna sababu gani nzuri na za kimsingi za kuwa mtenda haki na si kinyume chake, yaani mtenda maovu? Glaucon, ndugu wa Plato anajibu; "Binadamu wote kwa asili yetu tu wabinafsi, tunajijali sisi wenyewe kila tunapopata nafasi ya kufanya hivyo. Bila kujali kama jambo hilo si la haki kiasi gani kwa wengine. Lakini, kwa bahati mbaya, nasi pia hufikwa na hali kama hiyo kwa kufanyiwa yasiyo haki na wengine. Jambo hilo huwa si la kufurahia."
Maana. mlevi wa madaraka hupungukiwa haraka maadili ya uongozi. Basi, ghafla huwa mla rushwa mkubwa kwa kutumia ofisi aliyokabidhiwa . Na hatimaye, ghafla huwa tajiri mkubwa, bilionea! Vyote hivi huweza kumtokea kiongozi wa Kiafrika kwa kasi ya kutisha sana. Leo unapishana na Mwafrika mwenzako akiendesha baiskeli, kesho anaukwaa uongozi. Baada ya miaka 10 tu, anajenga "ikulu" yake mwenyewe ya kifahari, anaweza kuwa nazo mbili au tatu za namna hiyo na magari kadhaa ya kifahari. Je, yote haya ni kwa kipato halali cha "mteule" huyu kutokana na kazi yake?!nadhani muungwana alianza kuufuata ushauri wako huu. kwani kuna hekalu anaziangusha maeneo fulani huko kunakojulikana....
Mtu wa namna hii kamwe hawezi kukupa historia yenye kueleweka juu ya utajiri wake wa ghafla. Huyo si mhalifu kama walivyo wezi wa kuku au wenye kuvunja madirisha usiku. Huyo ni jambazi, ni mhalifu mkubwa anayetishia usalama wa taifa husika.
Hivyo basi, ili kuwapo na mazingira ya kuishi kwa amani na usalama ni vema, kwa mujibu wa mwanafalsafa Plato, kukawapo na taratibu za kuishi kistaarabu. Ndipo hapa dhana ya kuwapo kwa Mkataba wa Kijamii (Social Contract) ikaingia akilini kwa mwanadamu. Ndilo chimbuko la katiba za nchi. Chimbuko la misingi ya utawala bora.
Na hii ni changamoto kwa Rais Jakaya Kikwete na uongozi wake wa Awamu ya Nne. Ana nafasi ya kuwawekea Watanzania misingi na taratibu za kistaarabu za kuishi katika nchi yao. Aendelee na juhudi za kukirekebisha chama chake ili apate msingi wa kufanya marekebisho ya Katiba ya nchi. Ni kazi ngumu, lakini inawezekana, na hususan anapokuwa na umma nyuma yake.
Maggid,
nilikuta jana kuna thread umeanzisha kulalama kuhusu kupopolewa hoja yako hii uliyoianzisha. mimi nikakujibu kwa mtazamo wangu hasa yale niliyoyaona kwenye hoja zako na bila kusahau mtazamo wako HURU. ila pia unajitahidi kujinasua kutoka ktk kundi la kumkampeinia JK ingawa ulishaanza zamani sana. Kumbuka in 100 days alizokaa kikwete madarakani wenye macho tulishaanza kuona kukengeuka kwake kuacha ile misingi aliyoihubiri ktk kampeni 2005. lakini wewe hukuona hiyo kitu na ukaendelea kumwaga sifa kwake. na alipotimiza miaka mitatu madarakani niliinasa hiyo post yako hapo chini ukielezea jinsi alivyofanikiwa na hukueleza mabadiliko ya kushuka kwa kiwango cha utendaji na kimajukumu kwa yeye na wasaidizi wake dhidi ya wananchi. Nahisi wewe umeshalipiwa bill ya kila bidhaa ndo maana huoni mfumuko wa bei, uhaba wa huduma n.k.
Naomba nikutukane tena kwa kuweka hii makala yako hapa jamvini
Maggid said:Nikiwa Bagamoyo nilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wananchi, kusikia maoni yao juu ya mtu huyu, Jakaya Kikwete. Nilitaka kupata maoni ya watu wa kawaida juu ya matarajio yao kwake.
Nakumbuka kuzungumza na kijana mwuza chipsi pale sokoni Bagamoyo. Huyu aliniambia; Braza, Jakaya huwa anapita hapa kwa miguu akienda nyumbani kwake. Na kichochoro anachopita hiki hapa. Ukimaliza kichochoro hiki nyuma hapo utaukuta mti wa mkungu, mbele kidogo kuna kiwanja cha watoto, nyumba yake inaonekana kwa mbele.
Watu kadhaa walinipa simulizi zenye kufanana juu ya Jakaya Kikwete aliye karibu na watu. Jakaya waliyezoea kumwona akikatisha mitaa ya Bagamoyo kwa miguu na kuzungumza na wananchi. Kwa namna moja au nyingine, simulizi hizi zilionyesha ni kwa jinsi gani mtu huyu Jakaya Kikwete asivyo na makuu.
Mkuu umepiga msumari wa mwisho.Mkuu Msanii, asante - hii ndiyo maana naipenda JF na huwa nawaonya rafiki zangu wawe waangalifu sana wanapotoa maoni yao humu ndani kwani yanaweza kuja kukusuta baadaye. Huyu Maggid sijui kama ameona mapokezi aliyoyapata Dr. Slaa mjini Iringa leo na kama ameyaona bado atatetea msimamo wake ambao ana jeuri ya kuuita tathmini kumbe ni kumpigia debe Kikwete, aiyemwona kama tumaini la Watanzania. Siamini kuwa huyo Jakaya Kikwete anayemwongelea Maggiid ndiye huyu huyu mwenye jeuri ya kusimama jukwaani kuwanadi wezi na wahujumu uchumi wa taifa letu. Hata hivyo sasa baada ya kulisoma hilo bandiko lake la miaka ya nyuma, sidhani kama nitendelea kuchangia tena katika hizi mada zake zisizo na kichwa wala miguu.
Kudakeki,BWANA MJENGWA,
HIVI WEWE HUKUPATA KUAMBIWA KUWA UKITAKA KUWEKA HOJA HUMU NI SHURTI IWE ILA INAYOWAPENDEZA KWENYE MASIKIO YA WANA-CHADEMA? Sasa swali langu haya mabandiko ya kusifia Chadema sijui ndiyo yataongeza kura kwenye sanduku la kudumbukizia kura siku ya uchaguzi ama what is the logic behind the wasted energy? :tonguez:
Nimemwandikia mhariri wa mtandao huu ( JF) kumwomba abadilishe title ya thread hii; " Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?". ( Kule kwenye jukwaa la habari za uchaguzi mkuu)
Hata kama title ya thread imewekwa katika mtindo wa swali bado jibu la swali hilo ninalo, kuwa HAPANA.
Niko Iringa na naendelea na kazi zangu za kila siku katika ajira yangu. Baada ya kazi niko na familia yangu, kazi za kublog na shughuli nyingine za kijamii. Sijajihusisha kwa namna ye yote na kampeni za siasa, iwe Udiwani, Ubunge na Urais, kwa mgombea ye yote na Chama cho chote kile, iwe katika chaguzi zilizopita na hata uchaguzi wa mwaka huu. Anayeweza kuthibitisha kinyume chake aje.
Watu wana uhuru kuchangia maoni yao hata kama wanafikiria hivyo. Lakini kuweka title katika mtindo huo kunaweza kuwafanya wengine waamini ndio ukweli wenyewe.
Ni matumaini yangu mhariri wa JF atatanguliza uungwana na kubadilisha title hiyo ya thread hii. Inanipa usumbufu, mimi na hata familia yangu, kwa vile haina chembe ya ukweli.
Natanguliza shukrani.