Kama system ingekuwa fair basi Bashe na Mtaka walipaswa kuandaliwa kwa Urais wa nchi yetu, wanafaa sana

Naomba nikiri wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila ni mwananchi mwenye shauku ya kutaka kuiona nchi yangu inapiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Kutokana na kwamba ili mpige hatua kubwa za kimaendeleo mnalazimika kuwa na viongozi wenye maono, wabunifu, wenye ushawishi, wasio na tamaa lakini wenye ujasiri wa kusimamia wanayoyaamini, ndipo nikaona kwa namna hawa wawili wanavyotekeleza majukumu yao wanaweza kuwa wanafaa sana kushika hiyo nafasi ya juu katika nchi yetu.

Tatizo la dunia ya siasa huwa mambo huja kiajaliajali Kwa jinsi hiyo unakuta mtu ambaye angafaa kutuongoza na kuliletea taifa maendeleo kutokana na kushika nafasi nyeti za kufanya maamuzi anaachwa pembeni, analetwa mtu Kwa maslahi ya genge fulani.

Ikiwa kuna watu wa system humu ndani naomba mnisaidie kuwapigania hawa vijana taifa letu litapiga hatua sana ikiwa mmojawapo atashika madaraka ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.
Naunga mkono hoja !!
 
😄😄eti Rais wa WCB daah we mkuu sio powa 🙌😁
Huwa sijali sana suala la imani, mtu akiwa Smart ni smart haijalishi imani yake. Kama tunachagua mtu kwa imani yake basi hii nchi haitokaa iendelee. Mtaka sioni la maana lolote kichwani mwake mtu aanze hapa kusema anafaa kuwa Rais. Labda Rais wa WCB.
 
Hivi kile kitendo cha Anthony Mtaka kipindi alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kumpiga vijembe PUBLICLY alyekuwa Waziri wa Elimu wa kipindi hicho kabla ya huyu aliyepo sasa; kilikuwa ni halisi au yalikuwa ni maigizo? Na kama yalikuwa ni maigizo, unaweza kujua hayo maigizo WALIYAFANYA wakiwa wamekusudia ku-potray picha gani kwa Watanzania?

Picha niliyokuwa nayo awali kuhusiana na huyu mtu, ilitoweka ghafla siku hiyo. Kwa sasa sioni kitu, naona blurr tu! Hakuna watu ninaowaogopa mimi kama watu wa kufanya maigizo kwenye maswala serious ya nchi. Unaweza ukastukia hata wanakuletea kampuni hewa ya kununua korosho! Bashe is among the best URT ministers at the momnent
 
Bashe is good ila levels za utendaji yaani prime minister inamfaa kuliko kuwa president, he is another magufuli kwa utendaji sasa hawa ni type inayotakiwa wawe below someone, wasiwe wao ndo wao!
 
Naomba nikiri wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila ni mwananchi mwenye shauku ya kutaka kuiona nchi yangu inapiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Kutokana na kwamba ili mpige hatua kubwa za kimaendeleo mnalazimika kuwa na viongozi wenye maono, wabunifu, wenye ushawishi, wasio na tamaa lakini wenye ujasiri wa kusimamia wanayoyaamini, ndipo nikaona kwa namna hawa wawili wanavyotekeleza majukumu yao wanaweza kuwa wanafaa sana kushika hiyo nafasi ya juu katika nchi yetu.

Tatizo la dunia ya siasa huwa mambo huja kiajaliajali Kwa jinsi hiyo unakuta mtu ambaye angafaa kutuongoza na kuliletea taifa maendeleo kutokana na kushika nafasi nyeti za kufanya maamuzi anaachwa pembeni, analetwa mtu Kwa maslahi ya genge fulani.

Ikiwa kuna watu wa system humu ndani naomba mnisaidie kuwapigania hawa vijana taifa letu litapiga hatua sana ikiwa mmojawapo atashika madaraka ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.
Umegonga penyewe mkuu, yaani hawa watu wawili Wana uwezo mkubwa sana
 
Bashe is good ila levels za utendaji yaani prime minister inamfaa kuliko kuwa president, he is another magufuli kwa utendaji sasa hawa ni type inayotakiwa wawe below someone, wasiwe wao ndo wao!
Inafikirisha !! Kweli wengine ni wazuri sana lakini awepo MTU juu wa kuwafunga speed governor !!
 
Yule mwanasheria class A Paskali Mayalla alishadiriki humu kutuambia Makonda anafaa kuwa Rais.

Yani akili za Watanzania wanazijuwa wenyewe.
Mwanzoni alionekana hivyo lakini kadri muda ulivyopita akaanza kukengeuka na baadaye kulewa madaraka !!
 
Obama jaluo from kogelo !! Boris Johnson from Turkey !! Lakini wameruhusiwa kutawala Nchi ambazo ni Super power in the world !!! USA + UK !!
Taasisi za Ulaya na US huwezi kuzifananisha na zetu, huku ukiwa rais unakuwa juu ya sheria Mungu mtu unaweza kuuza hata mlima Kilimanjaro hakuna wa kukushitaki, leo Trump yuko mahakamani anajibu kesi.
 
ukitaka kumjua vizuri hilo bashe nenda pale habari corporation shekilango sinza au tafuta mtu anayefanya Kazi hapo ndipo utajua huyo jamaa ni mtu wa hovyo sana
ni hivi system yetu ni ya hovyo sana kuruhusu huyu jamaa kuwa waziri
Hawamjui hao mzee.
 
Nimekueleza mtaka sio kiongozi mzuri hata kidogo, kwa wale wa simiyu wanaelewa alichokua akifanya kwenye miradi.

Ila ww mpaka mtu awe ndugu yako katika imani ndio unamkubali.
Mbona Dr Mwigulu, Mpango, Muhongo, Chenge nawakubali kwa usmart wao. JAFFO, UMMY siwakubali??
 
ukitaka kumjua vizuri hilo bashe nenda pale habari corporation shekilango sinza au tafuta mtu anayefanya Kazi hapo ndipo utajua huyo jamaa ni mtu wa hovyo sana
ni hivi system yetu ni ya hovyo sana kuruhusu huyu jamaa kuwa waziri
Mimi kitendo cha kusambaratisha ndoa ya Bona na Karua kisha yeye Bashe kumuoa Bona ndio nimemuona mpumbavu kabisa.

Nachukia sana watu wanaofarakanisha familia nyingine, wanawake wamejaa kibao huwaoni mpaka umkule mke wa mtu?

Sasa huyu umpe Urais si ndio atapora kila mwanamke atakayemtaka?
 
Watanzania tunapenda sana maneno matamu labda kwakua jina la nchi ndivyo lilivyo.

Tanganyika, tuache kuwa wadanganyika.
 
Obama jaluo from kogelo !! Boris Johnson from Turkey !! Lakini wameruhusiwa kutawala Nchi ambazo ni Super power in the world !!! USA + UK !!

Ongezea na Rishi Sunak na Priti Patel pamoja na Mayor wa London wote asili yao ni Asia

Ila dunia hii bila kuchanganya damu hatutoboi
Akili moja tu haifai tunakuwa masikini maisha
Mimi naona ni wakati sasa wa kuwekeza kwa asili zingine kuanzia wazawa Wahindi, Wasomali, waarabu na majirani zetu waliozaliwa na kukulia kwetu

Mbona tungeendelea sana
Hivi imagine Rishi Sunak angekuwa waziri ww fedha Tanzania wabaguzi wangepiga kelele sana

Bashe tu wanalia
 
Back
Top Bottom