Kama system ingekuwa fair basi Bashe na Mtaka walipaswa kuandaliwa kwa Urais wa nchi yetu, wanafaa sana

Naomba nikiri wazi kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila ni mwananchi mwenye shauku ya kutaka kuiona nchi yangu inapiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Kutokana na kwamba ili mpige hatua kubwa za kimaendeleo mnalazimika kuwa na viongozi wenye maono, wabunifu, wenye ushawishi, wasio na tamaa lakini wenye ujasiri wa kusimamia wanayoyaamini, ndipo nikaona kwa namna hawa wawili wanavyotekeleza majukumu yao wanaweza kuwa wanafaa sana kushika hiyo nafasi ya juu katika nchi yetu.

Tatizo la dunia ya siasa huwa mambo huja kiajaliajali Kwa jinsi hiyo unakuta mtu ambaye angafaa kutuongoza na kuliletea taifa maendeleo kutokana na kushika nafasi nyeti za kufanya maamuzi anaachwa pembeni, analetwa mtu Kwa maslahi ya genge fulani.

Ikiwa kuna watu wa system humu ndani naomba mnisaidie kuwapigania hawa vijana taifa letu litapiga hatua sana ikiwa mmojawapo atashika madaraka ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.
Umetumwa na Bashe
 
Back
Top Bottom