Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

mwezi umeisha bila baraza la mawaziri, mtu mbili tu zinaendesha nchi magufuli na ombeni tosha kabisa, pale bungeni walivyokuwa wanafanya fujo angelifuta bunge palepale ingekuwa bonge la big up.
Mkuu, Rais wa Nigeria alipo chaguliwa amekaa miezi sita bila ya Baraza la Mawaziri na Nchi ikawa anaiongoza kwa ufanisi mkubwa!!!
 
hihihi wazeewa10% naona watakuwa kazini kusaka waganga wa kumnyamazisha magu.......

bora awakomeshe kuna haja gan kutumbuua milioni 265 ilhali kuna mwananji anakufa mahali kwa kukosa mseto wa buku wakome
 
Muache hawe dictator.

Hela za Escrow mligawana mkasame ni za mtu binafsi kagawa sadaka. Leo hizi nazo ndio za makampuni binafsi zilitolewa kwa ajili ya kupikia chapati wabunge lakini kwa vile wote walikuja wameshiba rais akasema zikanunulie vitanda hili wagonjwa wapumzike.

Uditekta mwingine ni mzuri, kitu chochote kina ubaya na uzuri wake na hapa rais katumia uditekta vizuri.
 
huwezi elekeza pesa zilizochangwa kwa shughuli fulani iende kufanya jambo lingine hata kama hilo jambo lina faida zaidi. sheria hizi zipo kuzuia ishu za kutakatisha pesa na kuchangisha fedha kwaajili ya magaidi.

Shame on you.

Pesa zote zilizopotea kwenye nchi hii na kwenda kwa viongozi walafi leo mil 250 imeenda kwa wagonjwa maskini mnataka kupiga kelele?
 
kusema 2016 tushereke kawaida,leo tufanye usafi na fedha zitumike pengine bila kusema wapi hii maanake ni hakuna pesa hazina na propaganda za kiini macho kwa washabaki ila sio waelewa,ilhali ni KUDHARAU SIKU TULIYOPATA UHURU kwa kuficha yasiyofichika shame
 
huwezi elekeza pesa zilizochangwa kwa shughuli fulani iende kufanya jambo lingine hata kama hilo jambo lina faida zaidi. sheria hizi zipo kuzuia ishu za kutakatisha pesa na kuchangisha fedha kwaajili ya magaidi.

Ukinipa mchango wa sherehe ni maamuzi yangu nitumiaje pesa hio either kwa ajili ya sherehe hio au nipeleke kwingine hio aikuhusu as long as your part is done,zilichangwa yes na alipendekeza hakutoa amri,alichopendekeza kimefanyika is it bad?hebu tuambie amekosea wapi
 
Tanzania is already a police state. THERE IS NO QUESTION ABOUT THAT. WHAT MAGUFULI IS DOING IS JUST TO IMPLEMENT WHAT IS ALREADY IN PLACE.
 
huwezi elekeza pesa zilizochangwa kwa shughuli fulani iende kufanya jambo lingine hata kama hilo jambo lina faida zaidi. sheria hizi zipo kuzuia ishu za kutakatisha pesa na kuchangisha fedha kwaajili ya magaidi.

sijui taaluma yako ila nadhani masuala ya budget management huyajui.
 
HADI SASA HAKUNA MTU HATA MMOJA ALIYE JIBU HOJA ZA PASCO.
Wote wanahoroja kishabiki wasijue iko kesho tena kesho itayo washangaza hata wao !
-MZARAUNI PASCO LEO ILA KESHO MTA MWELEWA SANA ..

JAPO ITAKUWA TOO LATE!

Hivi wewe akili zako zinamtegemea Pasco?..... Ama unahisi kua Pasco hua yuko Sahihi wa kila bandiko?.... Acha kua na hisia dependent jisimamie ukiona watu 95 kwenye 100 wakagomea hoja yako lzm ujitambue kua umechemka..... Moja ya kusababisha mambo mazuri kwenye jamii iliyochoka kama TZ ni kubana matumizi..... Si utashangaa sana siku akisema hapandishi mishahara yenu na ukiwa mzembe kwa ajili ama lengo la kumkomoa rais itakula kwako...... Fikiria kabla ya kusema unahitaji kusherekea.... Kuna shida nyingi sana kwa watz,,,,, na ni kweli haziwezi kumalizwa na magufuli lkn bora atoe mwanga kwa watakaomfuata....... Magufuli tumamaga namhala....
 
kusema 2016 tushereke kawaida,leo tufanye usafi na fedha zitumike pengine bila kusema wapi hii maanake ni hakuna pesa hazina na propaganda za kiini macho kwa washabaki ila sio waelewa,ilhali ni KUDHARAU SIKU TULIYOPATA UHURU kwa kuficha yasiyofichika shame

ndiyo hazina hakuna hela wewe ulitaka iweje?
 
kusema 2016 tushereke kawaida,leo tufanye usafi na fedha zitumike pengine bila kusema wapi hii maanake ni hakuna pesa hazina na propaganda za kiini macho kwa washabaki ila sio waelewa,ilhali ni KUDHARAU SIKU TULIYOPATA UHURU kwa kuficha yasiyofichika shame

Walewale...... Cheka sana eti kudharau Siku ya UHURU..... Inakusaidia nini? Jipange kwa ajili ya kusherehekea BIRTHDAY YAKO hiyo ni bora kabisa kuliko
 
Idea inayonijia kichwan ni kuwa miaka ya nyuma mtoa mada ulikua unafaidika na ulaji wa % fulani ndo maana inakuuma. Sawa ulimkubali Magufuli lakini hukujua atakupotezea ulaji....samahani ni maoni tu
 
huwezi elekeza pesa zilizochangwa kwa shughuli fulani iende kufanya jambo lingine hata kama hilo jambo lina faida zaidi. sheria hizi zipo kuzuia ishu za kutakatisha pesa na kuchangisha fedha kwaajili ya magaidi.

Kwani hiyo paty ambayo ilitumia 10% ya original budget haikua party? Kwa hali ya kawaida tanzania party ya 200M inakua na mayai ya gold au nini?
 
mh raisi kwa hili nakupa big up na nakuomba tupilia mbali kabisa mbio za mwenge.
 
Na huu si udictator ndo inaitwa "authoritarian" kama akili yangu imejaa vizuri. Tumwache. Nchi imeyumbwa kwa kukosa wenye kuinyosha kwenye mstari.
Kama Utawala wa sheria umeprove lawlessness kwa nini msitumie dictatorship. Na kwanza ni ninyi wenyewe mnaoshindwa kujiendesha kwa haki chini ya sheria mnamfanya awadictate. Msipo fikiri mtafikiriwa na mhe president. Ndo maana Donald Trump aliiwazia Africa zaidi ya udictator, yaani kuicolonize upya for another 100 years, ili mjifunze Utawala wa democracy ya sheria. Viva Magu
 
Kuna msemo unasema ili ule nyama lazima uchinje inamaana kiumbe kitaumia ila wewe utafaidi nyama hivyo hivyo kwenye maamuzi magumu muda flani inabidi baadhi ya watu waumie ili ufikie malengo ambayo yatawanufaisha wote
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.

Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu 'YES!", "ndiyo mzee!". Ila kwa hali ninayoina sasa, jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kamu huu Sio Udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria, kuamua kuongoza kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani kina anachokotaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli atafanikiwa sana!.

Rais alipoamuru zile pesa "private money", zilizochangwa na private entities, zikiwemo public corporation, kama sehemu yao ya CSR kuwakiimu wabunge wapya kwa mlo wa usiku!, alitumia mamlaka gani?!. Yaani rais anaweza kuamuru private entities watumieje fedha zao?!, kwa sheria ipi, kanuni ipi na taratibu ipi?!. Huu kama sio udikiteta ni nini?!.

Alipoamua hayo, wengi wameishia tuu kupiga makofi, hakuna aliyejiuliza, agizo hilo amelitoa kwa mamlaka gani?!.

Njuavyo mimi mashirika na makampuni yanatenga fungu fulani za kufanya shughuli za CSR ili ku achieve specific objectives kwenye strategic plans zao!. Kama Bunge liliomba udhamini wa mlo wa usiku, na mashiika na makampuni wakaona zina fit kwenye zile CSR zao, wakatoa, rais alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia na kuamuru diferent use ya private money?!.

Hata kama rais ameona matimizi yale yalikuwa ni anasa tuu, angeliamuu bunge likatae michango hiyo, na kuirudisha kwa wenyewe ili zipangiwe CSR nyingine, na rais kama alihitaji hizo fedha zipelekwe kuhudumia wagonjwa Muhimbili wenye uhitaji mkubwa zaidi wa vitanda kuliko mlo wa wabunge, angeomba kama waombaji wengine!.

Baada ya kufanikiwa kwenye hili na kupongezwa, leo rais wetu ameibuka na jinginekufuta parade ya uhuru!. Swali ninalojiuliza hivi kumbe parede ya uhuru ni miongoni mwa sherehe zinazoadhimishwa at the pleasure of the president?!. Nilifikiri hii ndio the no 1 state event na ipo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni?!, hivi ni kweli ais wa nchi anaweza tuu kuamka asubuhi na kuamuru maandimisho ya parade ya uhuru yafutwe just like that?!, mamlaka hayo rais wetu ameyatoa wapi?!.

Mbaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama atasitisha utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia pesidential decrees pekee?!.

Najua kuna watu humu wanaweza kulitafsii bandiko langu hili na chuki binfsi!, nawaomba sana wanisome hapa!, mimi ni mmoja wa waliosema kuwa Mgombea wa CCM atakuwa ni John Pombe Magufuli tena kwa sababu maalum. Angalia kwa makini bandiko hili ni la lini
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 ni John Pombe Magufuli-Aug 15, 2014


Na baada ya CCM kumpitisha rasmi Magufuli, nilipandisha bandiko hili
Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Yaishe!.


Na baada ya ushindi wa Magufuli, nilipandisha uzi huu
Ushauri Wa Bure kwa ENL, Chadema na UKAWA, Tukubali Kushindwa, Tuyakubali Matokeo...


If You Can't Beat Them, Join Them!, He is a Worst Dictator!.

Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Pasco.



Mkuu Pasco Ninakuheshimu sana kwa hoja ulizo weka hazina nguvu sana Nchi yetu chafu umasikini wa kumwaga maradhi ndio usiseme. Mheshimiwa Rais Magufuli hajafanya kosa kuiondosha

Sherehe za uhuru wa nchi na badala yake amaeagiza nchi nizima Wananchi tuungane kusafisha nchi kwa

sababu ya maradhi ya kipindupindu huoni Rais Magufuli amefanya jambo la maana sana? Sherehe za Uhuru kila mwaka zipo zisipofanyika mwaka huu mwakani tutazifanya Mkuu pasco kwa

maneno yako ya kumkosoa Muheshimiwa Rais Magufuli hapo sipo pamoja na wewe. Mkuu Pasco twende

kule kwenye Jukwaa la Jamii Intelligence tukazungumze mambo ya nyota achana na mambo ya Kisiasa Mkuu Pasco .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom