Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

kwa hili la kufuta sherehe za uhuru namsapoti kabsa rais wetu jpm namwomba pia lile dude la mwanga na kutoa moshi mweusi alitupilie mbali makumbushooo butiama kwa mwalimu jk wa kwanza.
 
Kwa hali ilivyo sasa hakuna namna ya kumkwepa Rais kama Mheshimiwa Magufuli, huyu mtu kwa sasa anatufaa sana, muacheni ainyooshe nchi ikae kwenye mstari sahihi. Anayempinga ana lake jambo, kama si kufaidika na mfumo wa rushwa, Ufisadi na uvivu uliokuwa umeanza kujengeka kwa kasi.
 
Majipu yameanza kutumbuka?Rais hakufuta siku ya uhuru.ipo pale kisheria.alichofuta ni sherehe,,kama mkapa alipofuta matamasha na miziki kumuomboleza baba wa taifa.mwezi mzima hakuna mziki,
 
Kama Taifa tulihitaji rais aina Ya Magufuli Na tumempata ndio Magufuli mwenyewe.

Wazee wa kutumia fursa wakati wenu umepita Na sasa unapumzika Msoga, sasa hivi ni wakati wa sisi wananchi wa kawaida kufaidika Na nchi yetu.

Magufuli ni Rais wa wanyonge Na adui wa wapiga dili!
 
Mh. Rais akijaribu kuwasijiliza watu wanaojifanya washauri na wanaojifanya wanataka utawala bora basi atapotea, hawa watu walimcheka JK na kuponda kitu kinaitwa utawala bora sasa sisi wananchi tulikupigia kura Mh. Raisi hatuuhitaji huo wimbo wa utawala bora kamwe, sisi tuna njaa ya chakula na kiu ya maji na tunaumwa maradhi hatari, tunahitaji huduma tu hizi nyimbo za utawala bora tumezichoka, wakijua umuhimu wa sisi wanyonge na wakagawana na sisi tutawaunga mkono kwenye haya matakwa yao ya utawala bora(chaka la mafisadi)
 
Kwa nchi ilipofikia haina jinsi, Maamuzi magumu kama sera ya lowassa inambidi atekeleze, bila hivyo yakakuwa ni yaleyale.

#MaamuziMagumu#

Sorry, hayo c maamuz magum mkuu bali ni maamuz MAKINI na ya busara... Maamuzi magum ni kama kujinyonga, kuhonga 280000 kutoka laki tatu pekee uliyonayo, kujisaidia haja kuu barabarani ilihal u mtu mzima timamu, kutumia gharama kuuuubwa kutafuta cheo na bado ukashindwa na aliyetumia gharama kidogo tu NK, NK (in le presida's voice)
 
mwezi umeisha bila baraza la mawaziri, mtu mbili tu zinaendesha nchi magufuli na ombeni tosha kabisa, pale bungeni walivyokuwa wanafanya fujo angelifuta bunge palepale ingekuwa bonge la big up.
Uzumbukuku ni tabu sana
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.

Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu 'YES!", "ndiyo mzee!". Ila kwa hali ninayoina sasa, jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kamu huu Sio Udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria, kuamua kuongoza kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani kina anachokotaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli atafanikiwa sana!.

Rais alipoamuru zile pesa "private money", zilizochangwa na private entities, zikiwemo public corporation, kama sehemu yao ya CSR kuwakiimu wabunge wapya kwa mlo wa usiku!, alitumia mamlaka gani?!. Yaani rais anaweza kuamuru private entities watumieje fedha zao?!, kwa sheria ipi, kanuni ipi na taratibu ipi?!. Huu kama sio udikiteta ni nini?!.

Alipoamua hayo, wengi wameishia tuu kupiga makofi, hakuna aliyejiuliza, agizo hilo amelitoa kwa mamlaka gani?!.

Njuavyo mimi mashirika na makampuni yanatenga fungu fulani za kufanya shughuli za CSR ili ku achieve specific objectives kwenye strategic plans zao!. Kama Bunge liliomba udhamini wa mlo wa usiku, na mashiika na makampuni wakaona zina fit kwenye zile CSR zao, wakatoa, rais alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia na kuamuru diferent use ya private money?!.

Hata kama rais ameona matimizi yale yalikuwa ni anasa tuu, angeliamuu bunge likatae michango hiyo, na kuirudisha kwa wenyewe ili zipangiwe CSR nyingine, na rais kama alihitaji hizo fedha zipelekwe kuhudumia wagonjwa Muhimbili wenye uhitaji mkubwa zaidi wa vitanda kuliko mlo wa wabunge, angeomba kama waombaji wengine!.

Baada ya kufanikiwa kwenye hili na kupongezwa, leo rais wetu ameibuka na jinginekufuta parade ya uhuru!. Swali ninalojiuliza hivi kumbe parede ya uhuru ni miongoni mwa sherehe zinazoadhimishwa at the pleasure of the president?!. Nilifikiri hii ndio the no 1 state event na ipo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni?!, hivi ni kweli ais wa nchi anaweza tuu kuamka asubuhi na kuamuru maandimisho ya parade ya uhuru yafutwe just like that?!, mamlaka hayo rais wetu ameyatoa wapi?!.

Mbaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama atasitisha utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia pesidential decrees pekee?!.

Kuna Jambo niliwahi kulizungumza hapa, sasa naona kama linakwenda kutokea!.

[h=3]If You Can't Beat Them, Join Them!, He is a Worst Dictator!.[/h]Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Pasco.



Kama Utawala wa sheria umeprove lawlessness kwa nini msitumie dictatorship. Na kwanza ni ninyi wenyewe mnaoshindwa kujiendesha kwa haki chini ya sheria mnamfanya awadictate. Msipo fikiri mtafikiriwa na mhe president. Ndo maana Donald Trump aliiwazia Africa zaidi ya udictator, yaani kuicolonize upya for another 100 years, ili mjifunze Utawala wa democracy ya sheria. Viva Magu
 
Twende Baba Magufuli Twende! Maamuzi yako yanaleta ahueni kwa walalahoi tulio wengi. Nchi hii kuna watu wameshadhani ni yao na familia zao. Mpaka lugha familia nzima kiswahili ndio lugha ya kigeni kwao. Upuuzi na utumwa wa fikra. Futulia mbali wote na usiangalie sura ya mtu. Kazi tu asiyeweza akae pembeni.
 
Tanzania ilikuwa inahitaji mtu Kama magufuli ambaye hajawekwa na mtandao wowote,sio wa kucheka,chekaa tu.Magufuli piga Kazi.

Bora udikteta unaojali maslahi kwa wananchi,kumbe pasco Hauna huruma na hii nchi
 
Sorry, hayo c maamuz magum mkuu bali ni maamuz MAKINI na ya busara... Maamuzi magum ni kama kujinyonga, kuhonga 280000 kutoka laki tatu pekee uliyonayo, kujisaidia haja kuu barabarani ilihal u mtu mzima timamu, kutumia gharama kuuuubwa kutafuta cheo na bado ukashindwa na aliyetumia gharama kidogo tu NK, NK (in le presida's voice)

Kufanya maamuzi kama hayo huwa yanawakwamisha wengi na kuwachukiza waliomtanguliaa, hivyo lazima tuseme ni #maamuzimagumu#
 
Kwangu hata akisema ku.tom.ba mara moja tu kwa wiki na goli moja tu na muda uliobaki tukafanye kazi ili tutoke hapa, sawa tu! Kama unataka mambo ya demokrasia, kuandamana na kuunda tume ya kila upuuzi hamia Kenya huko ndiyo kuna huwo upuuzi, ila hapa kwetu ni amri tu ktk juu kushuka chini na hakuna kupingwa!
Nimekudharau sana.
 
Manina zako!
Yani wewe sisi tulikuwa tunalala chini hilo wewe hukuliona sio??
Sasa tunalala kwenye vitanda pia hujaliona hilo!??
Kama huu ndio idikteta basi tunautaka!!!
Hutaki shauri yako!!!
 
Naona Pasco ni mojawapo wa majipu yanayoanza kutumbuliwa, tulia tu hadi usaha wote utoke.
Kuhusu hela za makampuni kwa tafrija ya bunge, baada tu ya kutoa hela hizo zilikuwa mali ya Serikali kupitia Bunge, na Raisi ni accounting officer no.1 wa pesa yote ya serikali, kwa hiyo alikuwa na mamlaka ya kuzielekeza kufanya jambo jingine.
Go JPM Gooooooooooo.....hivi ndivyo jinsi y kuinyoosha hii nchi iliyokwishageuka shamba la bibi.
 
Mhe. Kikwete aliitwa legelege pamoja na serikali yake. Mhe. Magufuli ni dikteta. Nafikiri tuletewe Malaika katika uchaguzi ujao nao wagombee!
 
Hayo makampuni na mashirika wanajisikia furaha kubwa sana kwa kuwa fedha yao imetumika kisahihi zaidi kwa wagonjwa masikini sana hapo muhimbili kuliko zingetumiwa zote kwa bia na kuku. Ndio maana tunasema zidumu fikra za rais wetu magofuli. Ni mapinduzi si mabadiliko. Ndicho Watanzania walichokesha kuomba. Yawezekana Mungu amesikia kilio chetu. Sala yako ya kumnyanganya rais mamlaka ya kufanya mapinduzi ya maendeleo ni ya kishetani.
 
Back
Top Bottom