Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

...hapajawahi kutokea watu wagumu (na vigeugeu) kama watanzania, sherehe zingekuwapo jioni hiyo hiyo ungewaona humu wanaandika watu wanalala chini temeke, sisi tunasherehekea miaka "....sijui hata imefika mingapi tena". Tena hawataishia hapo, ungewasikia wakienda mbali zaidi na kupendekeza " hivi ingekuwaje kama tungekuwa tunasherehekea kila baada ya miaka 10 au 20?" Ili hizo pesa tuziokoee..

WTF is wrong with us!! Seriously tulikosea wapi mpaka tukawa na huu ukigeugeu wa ajabu namna hii? Tuna mlolongo wa sherehe/ maadhimisho ambayo kimsingi kadri miaka inavyokwenda tunazidi kuona hakuna tija?

Afterall kwa hili limekaa kwa technicalities tu, kuwa siku imebaki ila namna ya ukumbukaji wake ndio itabadilika. We have to start somewhere sasa vikianza tu mnaanza tena kulalamika.

Labda kama hatukubaliani kwa pamoja kuwa tulipofikia kwa sasa yanahitajika maamuzi magumu! Ila kama tunakubaliana basi tutulie tu dawa iingie kwa sasa maana hakuna namna nyingine kwa kweli.

Hawa ni wapinzani wa damu,nyama na roho.hawa lolote linalofanywa na serikali kwao baya....au haumjui PASCO????
 
Wewe unauelewa wa kutosha za kujua au kuona jitihada za rais za kujaribu kutoa nchi kwenye hili shimo. Pasco ni adui wa mabadiliko! Wewe ni adui wa mabadiliko unanitia kichefchefu

JIBU HOJA ACHA KUKURUPUKA we kilaza ..hatuwezi kuwa na mihimili mitatu halafu mtu anahodhi mamlaka ..
 
Last edited by a moderator:
Duuh, sikutegemea kwa weledi wako unaweza kuandika uzi kama huu, najiuliza bado uko kwenye siasa na kampeni? maana uzi huu umekuwa wa ki-shutuma zaidi na kusema uongo dhidi ya Rais Magufuli.
 
Na wewe nae ukitoa mchango wa mfano harudi huwa unatoa maagizo itumikaje? Wakila wewe inakuhusu nini hata wakiamua kununulia chu.pi au kitotumia katika sherehe utakayoalikwa?

Lazima wengi muumie sababu pesa nyingi mlikuwa mnaweka mfukoni

Aaaagh funzo wasitoe tena sababu wanatoa kupata marudisho ya aina tofauti baadae.
 
Jukumu la kiongozi ni kuongoza; kama watu wabunge wangeona Rais kaingilia lilikuwa ni jukumu lao kutetea muhimili wao na kumwambia Rais kuwa pendekezo au agizo lake hilo haliwezi kutekelezeka kwa sababu fedha zilitolewa kama mchango na watu binafsi. Kamati ya Uongozi wa Bunge ilitakiwa kusoma alama za nyakati. Sasa Rais kachaguliwa kuongoza na bahati nzuri anaongoza Watanzania wote...

Wangeng'ang'ania kusema watatumia fedha hizo zote kwa ajili ya sherehe na yeye angesema haendi huko hawezi kuwa mshirika wa madudu kama hayo. Walielewa ndio maana walikubali (comply).

Inaonekana kwa muda Magufuli itabidi atumie madaraka yake kama Rais kuinitiate mambo mengi maana wengi hawawezi kufanya bila kuongozwa kufanya.

Anachofanya sasa ni Udikteta wa Sheria tu; na subirini yale mabadiliko ya sheria mbalimbali ambayo yataanza kusukumwa kuanzia kikao kijacho cha Bunge... mstari umechorwa na wapo watakaovuka watakiona cha moto!
 
Ile sherehe raisi ndio alikuwa mgeni rasmi,alikuwa na maamuzi ya kupunguza hizo anasa.Tulikuwa tunalilia mabadiliko now yameanza tunaanza kulialia,tunamuomba Raisi aendelee kutumbua majipu
 
Binafsi nilikuwa natamani sana utawala wa kidikteta, nilichoshwa na mambo ya urasimu mara tuko kwenye mchakato, mara upembuzi yakinifu na upuuzi kibao ilimradi kuchelewesha mambo acha aamue kila kitu mwenyewe kama imekugusa kale malimao

Umenena haswa, Na akayale haswa malimao

Wamezoea kula pesa sasa hiyo paredi sijui inamsaidia nini mvivu huyu.

No kushika fagio na kufanya usafi na kisafisha nchi

Uhuru ndani ya nchi safi sio kuishi na uchafu

Wanalo wavivu na wala pesa za bure.

Hapa kazi tu
 
duuh, sikutegemea kwa weledi wako unaweza kuandika uzi kama huu, najiuliza bado uko kwenye siasa na kampeni? Maana uzi huu umekuwa wa ki-shutuma zaidi na kusema uongo dhidi ya rais magufuli.

jibu hoja za pasco acha uzumbukuku we ngariba!
 
Mwanzisha mada kakojoe ulale. Hapa ni mwendo wa kama akina Capt Thomas Sankara. Hapa ni kijeshi tu time ishapita ya mambo yenu ya procedures na upuuzi mwingineo. Pambaf!
 
Ila tuacheni utani huko Serikalini kuna waRASIMU kweli kweli kama atafaniliwa kuwanyoosha atakuwa ameisaidia sana hii acha kabisa MTU unaenda kwenye Ofis I ya Serikali yako lkn unaonekana kama unaenda kuomba huduma nje ya NCH
 
Jukumu la kiongozi ni kuongoza; kama watu wabunge wangeona Rais kaingilia lilikuwa ni jukumu lao kutetea muhimili wao na kumwambia Rais kuwa pendekezo au agizo lake hilo haliwezi kutekelezeka kwa sababu fedha zilitolewa kama mchango na watu binafsi. Kamati ya Uongozi wa Bunge ilitakiwa kusoma alama za nyakati. Sasa Rais kachaguliwa kuongoza na bahati nzuri anaongoza Watanzania wote...

Wangeng'ang'ania kusema watatumia fedha hizo zote kwa ajili ya sherehe na yeye angesema haendi huko hawezi kuwa mshirika wa madudu kama hayo. Walielewa ndio maana walikubali (comply).

Inaonekana kwa muda Magufuli itabidi atumie madaraka yake kama Rais kuinitiate mambo mengi maana wengi hawawezi kufanya bila kuongozwa kufanya.

Anachofanya sasa ni Udikteta wa Sheria tu; na subirini yale mabadiliko ya sheria mbalimbali ambayo yataanza kusukumwa kuanzia kikao kijacho cha Bunge... mstari umechorwa na wapo watakaovuka watakiona cha moto!

Now I know you, you are a political harlot!
 
Wanabodi,

Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.

Hata kama Dr. Magufuli ni rais wetu, haina maana ana inherent powers kuamua chochote na watendaji walio chini yake kazi yao ni kusema tuu 'YES!", "ndiyo mzee!". Ila kwa hali ninayoina sasa, jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kamu huu Sio Udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria, kuamua kuongoza kwa kutumia Presidential Decrees!, yaani kina anachokotaka rais na kukisema kinaandikwa na kinakuwa sheria!, kiukweli atafanikiwa sana!.

Rais alipoamuru zile pesa "private money", zilizochangwa na private entities, zikiwemo public corporation, kama sehemu yao ya CSR kuwakiimu wabunge wapya kwa mlo wa usiku!, alitumia mamlaka gani?!. Yaani rais anaweza kuamuru private entities watumieje fedha zao?!, kwa sheria ipi, kanuni ipi na taratibu ipi?!. Huu kama sio udikiteta ni nini?!.

Alipoamua hayo, wengi wameishia tuu kupiga makofi, hakuna aliyejiuliza, agizo hilo amelitoa kwa mamlaka gani?!.

Njuavyo mimi mashirika na makampuni yanatenga fungu fulani za kufanya shughuli za CSR ili ku achieve specific objectives kwenye strategic plans zao!. Kama Bunge liliomba udhamini wa mlo wa usiku, na mashiika na makampuni wakaona zina fit kwenye zile CSR zao, wakatoa, rais alikuwa na mamlaka gani ya kuingilia na kuamuru diferent use ya private money?!.

Hata kama rais ameona matimizi yale yalikuwa ni anasa tuu, angeliamuu bunge likatae michango hiyo, na kuirudisha kwa wenyewe ili zipangiwe CSR nyingine, na rais kama alihitaji hizo fedha zipelekwe kuhudumia wagonjwa Muhimbili wenye uhitaji mkubwa zaidi wa vitanda kuliko mlo wa wabunge, angeomba kama waombaji wengine!.

Baada ya kufanikiwa kwenye hili na kupongezwa, leo rais wetu ameibuka na jinginekufuta parade ya uhuru!. Swali ninalojiuliza hivi kumbe parede ya uhuru ni miongoni mwa sherehe zinazoadhimishwa at the pleasure of the president?!. Nilifikiri hii ndio the no 1 state event na ipo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni?!, hivi ni kweli ais wa nchi anaweza tuu kuamka asubuhi na kuamuru maandimisho ya parade ya uhuru yafutwe just like that?!, mamlaka hayo rais wetu ameyatoa wapi?!.

Mbaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama atasitisha utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia pesidential decrees pekee?!.

Kuna Jambo niliwahi kulizungumza hapa, sasa naona kama linakwenda kutokea!.

[h=3]If You Can't Beat Them, Join Them!, He is a Worst Dictator!.[/h]Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Pasco.



Ndo rais tuliojitakia
 
Himawari, watu wanakasirika kwa sababu;
1. Mirija ya kupata tender za kutengeneza kifia, t-shirts na kupamba uwanja imekatwa.
2. Posho za kukaa uwanjani(sitting allowance) kama ya kule bungeni ya kuanzia 100,000 - 500,000 zimekatwa.
3. 10% walizokuwa wanapiga zimekatwa....
...ngoja walalamike, ili mradi sio wengi, just a handful hakuna shida

Nakusoma Eli79, zama hizi ni za kula kwa kuvuja jasho haswa..., wale waliozoea kulipwa kwa kukaa tu au wale wazee wa kuchangamkia fursa za kupasiana watakufa njaa muda si mrefu.....!
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nilikuwa natamani sana utawala wa kidikteta, nilichoshwa na mambo ya urasimu mara tuko kwenye mchakato, mara upembuzi yakinifu na upuuzi kibao ilimradi kuchelewesha mambo acha aamue kila kitu mwenyewe kama imekugusa kale malimao
Nakubaliana nawe bora atawale kidikteta kama Kagame.
 
Yani kuna watu wameshikiwa akili. Hivi Watanzania mnataka nn? mtoa Maada unatafuta umaarufu au nn? Huna haya wewe. Muogope Mungu. Wenzako tumeuguza na tumezika. Nenda muhimbili akaone palivyo. Hakika Mungu atakuadhibu kwa kutetea Masikin waendelee kuumia. Yani kapige magoti umuombe Mungu Msamaha. Yani watu wale na kunywa na kulewa wakati kuna watu wanalala chini?
 
Back
Top Bottom