Wanabodi,
Tanzania ni nchi inayofuata Katiba na kuendeshwa kwa utawala wa sheria, hivyo itaongozwa kwa mujibu wa Katiba, sheria taratibu na kanuni!, no one is above the law!. Katika kufuata sheria hizo, taratibu na kanuni, pia kuna mamlaka ambayo katiba imempa rais wetu wa JMT kuyatekeleza at his pleasure, yaani vile rais atakavyoona inafaa, ikiwemo presidential appointments powers, and the power to hire and fire civil and public servants!.
Kwa hali ninayoiona sasa, Rais Magufuli anakoelekea, asipodhibitiwa, na vyombo vya udhibiti ambavyo ni Mhimili wa Bunge na Mhimili wa Mahakama, very soon kuna watu sio tuu watalia na kusaga meno, bali Tanzania kama nchi na taifa, tutaumia!.
Jee kuna ubaya tukimshauri rais wetu, kama huu anaoufanya sio udikiteta?!, then ni bora sana, Mhe. Rais aka "Futilia Mbali Utawala wa Sheria, akaiweka katiba pembeni kwa muda kidogo tuu (wa miaka 20 au 30, sio kama Mugabe, Kageme au Museveni,)kwa kutangaza hali ya hatari?!", na ndipo sasa ainyooshe nchi, na ikiisha nyooka ndipo airejeshe katiba.
Mnaonaje mkiungana na mimi, tumshauri rais wetu ili kuyanyoosha mambo yake vizuri, awe na mamlaka ya kufanya kila anachotaka, mnaonaje kama tutamshauri asitishe utawala wa sheria kwa muda, badala yake aongoze kwa kutumia presidential decrees pekee?!, mambo yakiisha tengamaa, ndipo turudishe utawala wa sheria?!.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Mbariki Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli atimize majukumu yake kwa mujibu wa katiba.
Paskali