Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Udigital huo umesahau maonyesho kwenye msiba wa kanumba?
mi nidhani ni ushamba wangu tu ndo unanisumbuaHuu usasa umeharibu sana tamaduni zetu.
ni bora kujistaafia aisee lakini hali inatisha....Hata mimi nashangaa mkubwa mwenzangu,
Siku hizi kuna watu wamegeuza misiba kuwa kama mashindano ya mavazi au urembo...
Anyway..yetu macho, tena ukizingatia tulishajistaafia..
Babu DC!!
kama niliposema hapo juu kweli sishangai sana kwa watu wa mbali walioenda msibani....Mambo yalianza kubadilika tangu zamani sana lakini hatukushituka. Vile vile misiba imekuwa mingi kiasi kwamba watu wamezoea. Pamoja na yote msiba unakuhusu huwezi kuuzoea.
ni bora kujistaafia aisee lakini hali inatisha....
nimejaribu kuchukulia poa watu ambao wanaenda kuzika wakiwa wamevalia sababu labda wao siyo ndugu na hawana uchungu na marehemu,
lakini inapofikia mtu kafiwa na close relative halafu anakimbilia salon kujisopua, ukweli hainiingii kichwani mkubwa mwenzangu
Haya bwana,
Mimi nilishajinyamazia...
Unaenda kwenye msiba na kuambiwa kuwa bajeti ya mazishi ni 10mil....
Wakati huo unahangaika na karo za watoto ambazo ni <4mil....
Ngoja kwanaza tulimbuke...
Babu DC!!
ha haaaaa, na ushamba huu nani angenipa hiyo tenda?Siku hizi msiba ni show tupu my dear. Hawakuongelea mwenye saluni akawapake makeup ama maznat alishawahi tenda?
Ningekuwa mie ndo wewe mbona ningechomekea tenda ya sare!
Juzi nilikuwa namtafuta shosti kwa dharura, akaniambia yupo salon anasuka, akanielekeza nikaona nimfwate....
wakati tunaongea, kulikuwa na mrembo mmoja pembeni anashonea weaving na kutengenezwa kucha, kope, nyusi, n.k.
mara simu ya mrembo ikaita, maongezi yakaanza..... "yaani we acha tu, ndo mambo ya dunia lakini, Tunamshukuru Mungu..... asante sana....
tunaaga kesho mchana na safari ya kwenda Moshi kwa mazishi itaanza baada ya kuaga, kweli tutammiss sana kaka yetu....."
baada ya hapo maongezi yakawa yanaendelea akawa anasimulia kuwa kakake kabisa kafariki, kaumwa siku 2 tu kafa.....
sijui ndo ukijijini au ushamba wangu! kweli nilisikitika sana.....
sipati picha kakangu anafariki, mimi naweza kuwa na nguvu kwenda salon kujipiga msasa ili niende kuzika kakangu au ndugu yangu wa karibu.
Nikajiuliza mambo mengi sana.
1) ni kwamba watu siku hizi wamezoea sana misiba kiasi kwamba wanaona ni kitu cha ajabu tu kufiwa?
2) watu hatuna uchungu tena na ndugu zetu?
3) u-kisasa unatufanya tuwe hivyo?
kweli mahusiano na ndugu/jamaa/marafiki yamepungua kiasi hiki mpaka tunachukulia misiba ya ndugu zetu kirahisi namna hii?
Wewe kweli babu! Bajeti ya msiba ya milioni 10 ilikuwa miaka 3 ama 4 nyuma. Sasa tunaongelea mil 15 baba. Na familia ina minimum contribution!
kwetu kijijini gharama huwa ni ya jeneza tu...... vingine vyote bure...Haya bwana,
Mimi nilishajinyamazia...
Unaenda kwenye msiba na kuambiwa kuwa bajeti ya mazishi ni 10mil....
Wakati huo unahangaika na karo za watoto ambazo ni <4mil....
Ngoja kwanaza tulimbuke...
Babu DC!!