Kama nyumbani kuna panya na huna paka fanya hili utakuja nishukuru

Muota Ndoto

Member
Dec 4, 2007
89
125
Wadau, moja kwa moja kwenye mada:

1. Utangulizi.
Maendeleo ya teknolojia huenda yamewafikia panya wasumbufu na waharibifu majumbani mwetu. Siku hizi wanakwepa mitego, wanatambua na kukwepa sumu na huku wamezidisha chokochoko na kujengeana hasira. Mtu ukiwa na bunduki waweza jikuta unamfyatulia panya risasi bila kujali ukubwa wake. Kwa kifupi panya mamboleo wamekuwa wajanja sana.

2. Mazingira ya nyumbani na sakata la panya.
Nyumba yangu ina fensi ya matofali na kweye geti kuna nafasi ambapo mnyama mdogo aweza kupenya kwa chini akaingia ndani au kutoka nje. Uani mwa nyumba kuna masalia ya mbao, mabati na makorokoro mengine yaliyotokana na ujenzi. Pia kuna shimo la taka ambapo humwaga taka zinazooza yakiwepo masalia ya chakula. Mazingira haya yalikaribisha panya na kwa muda mfupi walikuwepo wengi sana. Pia walizaliana ambapo vitoto nya panya viliweza kupenya na kuingia ndani ya nyumba na kutawala. Niliweka sumu ya panya, siikufanikiwa kuwaangamiza. Nikaweka mtego wa chuma na wa wavu pia hola. Nikaja na mtego wenye gundi pia wakaugundua na wakawa wanaukwepa. Huko nje kulikuwa kama uwanja wa michezo wa panya (wale wakubwa). Hali hii pamoja na uharibifu wa mali ndani ya vyumba ilinikera na nikawa natafakari njia mbadala. Mimi siwapendi paka kabisa na siwezi hata kuwa karibu nao. Hivyo kufuga paka haukuwa mmoja wa mipango mbadala.

3. Suluhisho
Mwishowe akili ilichanganya vizuri kwamba nitumie teknolojia na haswa kumtengeneza paka angavu (virtual cat - hii ni namna yangu ya kutafsiri nilichofanya). Nilitembelea Youtube na ku-download souti mbalimbali za paka. Paka mmoja akilia, wengine wakiwe wengi wakilia kwa namna ambayo paka wanafanya wanapojamiiana (huwa na kelele nyingi na ishara ya vurugu). Niliweka sauti hizi kwenye simu yangu ambayo kwa bahati inatoa sauti ya kutosha unapocheza audio. Nilicheza hizo sauti na kuzuka kwenye vyumba vyote kama paka anayetembea. Kwa muda mfupi na kwa mara ya kwanza mtego wa gundi ulinasa panya kadhaa ambao walikuwa wakikimbia kwa mfadhaiko kumkwepa paka huyu angavu. Huko nje niliongeza vionjo. Pamoja na kucheza sauti za paka wakiwa kwenye vurugu, nilijiongeza kwa kupita huku na huko nikipiga piga mabati na takataka nyingine ambako panya walijificha. Baada ya muda mfupi nilirudi ndani na kuchungulia walikokuwa wamejificha panya. Niliona wakichungulia kwa makini na kuchomoka mbio kuelekea getini na kutokomea. Mwishowe wote walihama. Sijaongea na jirani huenda wamehamia kwake. Sasa kama anasoma ujumbe huu nae ajiongeze. Hii ndio teknolojia mpya ya kukabiliana na panya. Asanteni.​
 
Attachments

  • 20221210_Paka wagomvi.aac
    1.3 MB · Views: 100
  • 20221210_Paka.aac
    273.5 KB · Views: 72
Niliwahi kupata shida kama hio, nikanunua kidude cha kutumia umeme, kinatoa sauti ya nyoka, sauti hii kwa sikio la kawaida la binadamu, huwezi kuisikia, ila panya anaisikia sana. Baada ya kukifunga hicho kidude, panya wote walikimbia.

Vidude hivi vinapatikana amazon, vina sauti tofauti tofauti, ya nyoka, paka etc. Na bei zinatofautiana kutokana na specifications tofauti tofauti. (utrasonic mice sepeller gadgets)
 
Hao panya wa kwako watakuwa wa kizamani. Kuna mapanya hata yakimwona paka, acha kusikia mlio wake... hayakimbii. Na paka akikaa vibaya atajikuta kwenye wakati mgumu...
 
Niliwahi kupata shida kama hio, nikanunua kidude cha kutumia umeme, kinatoa sauti ya nyoka, sauti hii kwa sikio la kawaida la binadamu, huwezi kuisikia, ila panya anaisikia sana. Baada ya kukifunga hicho kidude, panya wote walikimbia.

Vidude hivi vinapatikana amazon, vina sauti tofauti tofauti, ya nyoka, paka etc. Na bei zinatofautiana kutokana na specifications tofauti tofauti. (utrasonic mice sepeller gadgets)
👌
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom