Kama ningekutana na Sheikh Makaburi na Aboud Logo

chief72

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
625
302
Abubakar Shariff (Makaburi) na Aboud Logo walikuwa watu wenye elimu kubwa ya kidini hasa ufasaha katika kur ani, kwa hilo tu Allah awalipe insha allah, lakini jambo moja walilonishangaza ni kule kuwatetea kundi la vijana wa alshababi kwa kile walicho kiita eti JIHAD.

Hakuna jihad inayopiganwa kwa karne hii, hasa hao vijana wa alshababi kuua watu wasio na hatia hata kidogo, kuua watoto wadogo kwa aya zipi za kur ani.

Maelezo ya Nabii Muhammad (S.A.W) alishasema jihadi ndogo imekwisha duniani na kwa sasa imebaki jihadi kubwa, watu wakamuuliza ipi hiyo jihad ndogo na ipi hiyo jihad kubwa? Akajibu jihad ndogo ndio hiyo ya kupigana kwa upanga(vita) na jihad kubwa iliyobaki ni jihad ya nafsi ya mtu dhidi ya maasi ya ulimwengu, vipi mtu atajizuia na yale yaliyokatazwa Eg, ulevi, uzinzi, uasherati, ushirikina, wizi nk. Sasa leo akina Logo na Makaburi wanatumia elimu zao kuwatetea alshababi, 'wonderful'
 
Mahubiri ya kuua watu sio mazuri kabisa kwenye jamii
 
abubakar shariff(makaburi) na aboud logo walikuwa watu wenye elimu kubwa ya kidini hasa ufasaha katika kur ani, kwa hilo tu Allah awalipe insha allah, lakini jambo moja walilonishangaza ni kule kuwatetea kundi la vijana wa alshababi kwa kile walicho kiita eti JIHAD, hakuna jihad inayopiganwa kwa karne hii, hasa hao vijana wa alshababi kuua watu wasio na hatia hata kidogo, kuua watoto wadogo kwa aya zipi za kur ani, maelezo ya Nabii Muhammad (S.A.W) alishasema jihadi ndogo imekwisha duniani na kwa sasa imebaki jihadi kubwa, watu wakamuuliza ipi hiyo jihad ndogo na ipi hiyo jihad kubwa? akajibu jihad ndogo ndio hiyo ya kupigana kwa upanga(vita) na jihad kubwa iliyobaki ni jihad ya nafsi ya mtu dhidi ya maasi ya ulimwengu, vipi mtu atajizuia na yale yaliyokatazwa Eg, ulevi, uzinzi, uasherati, ushirikina, wizi nk, sasa leo akina logo na makaburi wanatumia elimu zao kuwatetea alshababi, 'wonderful "
pole sana ungekuwa na ilim ya diini,inshaallah ungeelewa nini mashekh hawa walichokuwa wanafanya,hata hivyo hueliwi kwamba allah,ametuamrisha tusidhurumu wala tusikubali kudhurumiwa na ametupa amri ya kupigana pale ambapo tumedhurumiwa na tukifa katika kudai haki yetu basi malipo yake tutayakuta kwake yeye allah(.s.w)na muislamu mkakamavu anapendeza zaidi kwa m'mungu kuliko yule goigoi,na hawatohudhunika waliokufa katika njia ya m,mungu(jihad),jihad haiwezi kufa mpaka mwisho wa dunia,kama huelewi uliza ,usitoe fa'twa kwa usilolijua,usije ukawa kafir.
 
kufa kwetu si adhabu ni ahadi ambayo tunajua,tutakufaje kwa bunduki,mabovu au vingine vile we don't know,we don't care, we don't fear,we don't scare.

unashabikia umejificha nyuma ya fakename hapo nyumbani kwako, toka nenda front line kama wewe siyo goigoi! dini zote ni ujinga wa mwanadamu.
 
kufa kwetu si adhabu ni ahadi ambayo tunajua,tutakufaje kwa bunduki,mabovu au vingine vile we don't know,we don't care, we don't fear,we don't scare.

Duh! mmelishwa nn? mbona mnatumia nguvu nyingi kwa ajiri ya dini?
 
pole sana ungekuwa na ilim ya diini,inshaallah ungeelewa nini mashekh hawa walichokuwa wanafanya,hata hivyo hueliwi kwamba allah,ametuamrisha tusidhurumu wala tusikubali kudhurumiwa na ametupa amri ya kupigana pale ambapo tumedhurumiwa na tukifa katika kudai haki yetu basi malipo yake tutayakuta kwake yeye allah(.s.w)na muislamu mkakamavu anapendeza zaidi kwa m'mungu kuliko yule goigoi,na hawatohudhunika waliokufa katika njia ya m,mungu(jihad),jihad haiwezi kufa mpaka mwisho wa dunia,kama huelewi uliza ,usitoe fa'twa kwa usilolijua,usije ukawa kafir.

Mmedhulumiwa nini nyie,ubwabwa?mbona wewe unashawishi wenzako waende mstari wa mbele kwenye Jihad huku ukiwa nyuma keyboard ukichoronga pumba badala ya kwenda hapo Mombasa,Moghadishu au CAR ukawaonyeshe wenzio kwa vitendo. Na huyo Allah wenu ni Allah gani ambae hawezi kujitetea yeye mwenyewe mpaka atetewe na wauaji?
 
Dini ni imani yako don't force everyone kuamini imani yako,ALL IN ALL MUNGU NI MMOJA
 
Siungi Mkono mauaji ya Mtu yoyote bila ya kufuata misingi ya Sheria.

Kama leo tutaunga Mkono mauaji yake kwa kuwa tu ni Mshukiwa wa Ugaidi basi kesho tutakuwa Wanafiki ikitokea Al shabab nao wataua Watu wanaowashuku kuuwa ndugu zao.

Lazima tuepuke Double Standard kwa kukemea Mauaji dhidi ya watu wasio na Hatia wakiwemo wanaushukiwa ni magaidi kwa kuwa bado hawajawa Convicted na Mahakama za Nchi husika.
 
Unawaza kukutana na marehemu kazi kweli kweli. Lakini hata hivyo mwenzio sa hivi yupo anaenjoy na mabikra 70.

Sure mkuu,na kwa taarifa za kiintelijensia ni kua keshawakamua 42 hadi sasa toka jana,inakadiriwa kufikia kesho atakua keshawamaliza kuwatoa bikra.jumapili anaanza kuwarudia,acheni ainjoy shkaji thawabu zake.
 
Siungi Mkono mauaji ya Mtu yoyote bila ya kufuata misingi ya Sheria.

Kama leo tutaunga Mkono mauaji yake kwa kuwa tu ni Mshukiwa wa Ugaidi basi kesho tutakuwa Wanafiki ikitokea Al shabab nao wataua Watu wanaowashuku kuuwa ndugu zao.

Lazima tuepuke Double Standard kwa kukemea Mauaji dhidi ya watu wasio na Hatia wakiwemo wanaushukiwa ni magaidi kwa kuwa bado hawajawa Convicted na Mahakama za Nchi husika.
sisi tushazoea mkuki kwa nguruwe hawajui nafsi zote zina thamani sawa ila itafamika tu iwe kesho au keshokutwa.
 
Mmedhulumiwa nini nyie,ubwabwa?mbona wewe unashawishi wenzako waende mstari wa mbele kwenye Jihad huku ukiwa nyuma keyboard ukichoronga pumba badala ya kwenda hapo Mombasa,Moghadishu au CAR ukawaonyeshe wenzio kwa vitendo. Na huyo Allah wenu ni Allah gani ambae hawezi kujitetea yeye mwenyewe mpaka atetewe na wauaji?
mimi nani mpak nimshawishi mtu?ki kwetu kiislam ukifanya jambo ni kwa ajiri yako kwanza,hata shekh makaburi na wenzie hao wameyafanya kwa maslahi ya nafsi zao,mimi au mwingine nae atafanya kwa ajiri ya nafsi yake.
 
Serikali ya Kenya inakanusha kuwa haihusiki, lakini raia wana akili timamu, kwa matukio kama haya ya mauaji viongozi wa dini ya kiislam, chuki haiwezi kuisha baina ya Serikali na Waislamu
 
kufa kwetu si adhabu ni ahadi ambayo tunajua,tutakufaje kwa bunduki,mabovu au vingine vile we don't know,we don't care, we don't fear,we don't scare.

Nimesikiliza leo hii jioni mawaidha ya sheikh mmoja kwenye TV nikiwa hapa Mwanza. Anasema wanawake wa kiislamu wanaovaa hijabu ni watamu sana kulinganisha na (kwa mujibu wake) wale "wanaoacha vichwa vyao kama nyoka na makwapa wazi"!

Je huu ndio msingi wa maoni yako?
 
Duh! mmelishwa nn? mbona mnatumia nguvu nyingi kwa ajiri ya dini?
hatutumii nguvu nyingi ila sisi hatuogopi kufa kwa ajiri ya mambo ya dini sasa nadini sisi ndo muongozo wetu,hivyo vikifanyika vitendo vya kuidharau au kuidharirisha dini yetu hapo ndipo tunapokuwa wakali na sisi si mnajua hatuogope kufa kwa ajiri ya mambo uadini!?na tumeambiwa tusidhurumu wala tusikubali kudhurumiwa.na tumeruhusiwa pia kulipa kisasi kwa yule aliekuonea.
 
Back
Top Bottom