Wana MMU kwema?
Kuna jambo limenitatiza nikafanya maamuzi ila likanilazimu nililete hapa nione ushauri wenu.
Ni ivi kuna kijana mmoja tunafahamiana kwa mda mrefu ni just a friend ananiheshimu sana kiukweli hatuna lolote ni heshima tu ya mda mrefu (kwanza si type yangu so mnielewe).
Majuzi alinipigia simu yeye na dada yake wanaomba niwe matrion wa mke wake, yaan huyo kijana ndo anaoa.
Niwarudishe nyuma kidogo kwa ufupi nakuaga matron sana marafiki zangu wanapenda niwe matron though sio wote nawakubalia.
Huyo kijana na dada yake hata mama yao wote wanajua kuwa hiyo shughuli naweza ndio maana waliniomba.
Waliponambia nilitaka kukataa lakini nikaona mama yao atanielewaje? Halafu ikifika siku yangu je watanisaidia?
Si mnajua mambo ya sherehe ni watu?
Basi nilikubali akanambia send off in mwezi wa november, so aliniomba mke mtarajiwa aje kwangu nimuone tuongee mambo fulani.
Kweli bi dada alikuja nikampokea ni kampa customer care zote.
Basi aliniomba kuangalia picha ambazo nilishasimamia send off mbalimbali nikampa akaangalia kweli alisifia sana.
Aliniuliza sasa dada mm nitapendeza kwa vazi lip? Nikamwambia tuvae tofauti kidogo na hapa bongo walivo zoea.
Kweli alipenda mavazi ya sendoff za kwetu.
Alikubali akaniomba mambo fulani nikamwambia hakuna shida nitasaidia though nigharama.
Wakati anaangalia picha niliona anaangalia picha huku akinitizama.
Nilichukulia poa, alishukuru sana na akanisisitiza nimsaidie niwezavyo apendeze.
Muda ulifika nikamsindikiza akarudi kwake.
Tatizo lenyewe alipofika kwao huko kwao aliwambia mashoga zake kuwa kapata matron hao mashoga zake walikuwa wanne. Walimwambia tumuone whatsap(si wadada mnajua zetu) kumbe mmoja wapo ni rafiki yangu nakwenye facebook, nilisoma nae advanced so alinijua.
Kwahiyo katika mashoga zake mmoja akaanza wewe(bi harus mtarajiwa) wewe ni mjinga sana utatafutaje matron ambae hamuendani kwani yeye ndo anaolewa?
Ivi nani alimtafuta? Akawambia ni mme wake na dada yake kweli walisema mengi sana mpaka mmoja naomba nisiyaseme.
So yule ambae ni rafiki yangu fb akanitafuta akanambia kila kitu kweli nilijiskia vibaya maana hakunificha lolote
Ukweli ni kwamba bidada na mimi niliona hatuendani kabisa labda tunataka kufanana rangi tu ila pengine sijisifii hatuendani yaani sikustahili niwe matron wake.
Lakini nikasema kama wameridhia poa nisikatae wakasema naringa.
Ikumbukwe kuwa bi dada alipo kuja nilimuhuliza vipi kwenu huwezi pata matron? Akasema sio wazoefu na sherehe itafanyiwa hapa mjini so nitafaa mim.
Baada ya hayo yote walonitukana mashoga zake kumbuka kwenye sherehe watakuwepo nikawaza watakavyokuwa nanyooshewa kidole nikasema hapana isiwe ishu siendi though nitafanya yafuatayo.
1.Mchango natuma
2.Vitu alivoniomba namtumia
3.Sitoi sababu ya kutoenda namwambia atafute mwingine ili nisimsalti yule rafiki yangu facebook aliniambia.
Mama wa kijana juzi alinipigia akanambia nitakuja nikamwambia mungu akijaria huyo mama ananipendaga sana.
Wana mmu maneno walosema lililoniuna ni ili (' au huyo matron alikuwa mchepuko wake?) ndo maana alimtafta?' jamani limeniuma ukizingatia mkaka mwenyewe si type yangu afu ni under age below 30 kwangu hapana coz na mm niko under 30 jamani imeniuma nitaonekana kituko nikienda hasa wale mashoga wa bi harusi.
Jamani familia ya kijana tunaheshimiana sana ila ndo ivo tena.kwanza wamenipunguzia gharama.
Jaman maamuzi haya ni sahihi? Je ikifikazangu yangu mda ukifika wanaweza susia sherehe yangu?
Naomba ushauri.
karibuni wote.
Yaani over 30 alafu bado
wakusumbue hao wengine? think twice if nt tripled, ningekuwa mimi
ningeenda na ningependeza zaidi ili wale watakaonyoosha vidole wasiwe na
la ziada zaidi ya kusifia eeeh Matron hatareee kabisa maana kapendeza,
shughuli ikiisha kila mtu kivyake, usipoende utawa disappoint ambao
hawajui kabisa na hawahusiki ata kidogo na hayo mambo ya ladies, cc the
boss
Afu ujue kuna
uwezekano wa hao mashoga kuwa humu JF...kuna uhusiano wa ma Facebook
addict na addiction na mitandao mingine kama hii...
Watakupa za uso kimya kimya kwa kuwa wanajua unawaongelea wao...(mfano
kuacha substance na kutafuta weakness nyingine za thread yako)
Amini nakuambia, ili
usiwe chanzo cha mkanda wa video na picha kutotazamwa hapo baadae,
achana na habari ya kusimamia hiyo harusi, acha kabisa.
Kama bibi harusi alishaambiwa wewe ulikuwa mchepuko, ataimagine vitu
vingi kiasi kinachoweza hata kuathiri ndoa yake na huyo bwana harusi.
Otherwise, kaa na bibi harusi, mweleze yote uliyoyasikia kinaga ubaga na
mpe msimamo wako, kama akikuelewa basi haina shida simamia. The safe
way ingekuwa kuachana na huo usimamizi.
umeongea la maana mkuu. weekend karibu kwangu.
FUPISHA story kidogo...
Halafu SAY nishaurini SIO nishaulini..
Mmmhhh
Yaani wanawake bwana tuna mambo. ..hivi hapo hao mashost wanaona wivu tu hakuna kingine!
Kwa maoni yangu
Usiache, just do it!ukiacha watafurahi!
Najua utakuwa umemzidi bi harus muonekano mzuri!!!!!
Hahaa haaa
Jus do it
Women's issues.........
Ridiculous stuff zinazoletwa na harusi. Watu badala ya kufocus kwenye ndoa eti 'Not my type'. Kwani wewe malaika na yeye binadamu? The last time I checked wote mnabelong to the same specie...Usiseme huendani na mtu kwa sababu at the end of the day we are all different. Yani kusimama tu na binadamu mwenzio unaona ni issue? Huendani naye kwa unamuoa wewe? Hata ukipita mtaani watu wanakusema and frankly waliyokusema wakati hupo hayakuhusu....
Kiukweli issue yako in utoto too much kiasi kwamba ushauri ni uende ukakue kwanza