Kama nimekosea nishaurini jamani

Kama nimekosea nishaurini jamani

wala siumizwe na maneno ya
wanafki wa pembeni km mwenye shughuli hana shida hao wengine wanakubana
nini?

unenichekesha dia unaweza hawa wanastaili mchambo basi tulisha kua.
 
Wewe kasimamie hiyo sendoff na kuhusu kutokuendana hayo achana nayo maana kila mtu ana uzuri wake
 
Tatizo kina dada mnapenda kushikiwa akili. Likitokea jambo unakimbilia kushauliwa. Mengine tumieni akili zenu. Wahenga walisema ''maji ya moto hayachomi nyumba''.
 
basi usinune nimeuliza tu maana naweza omba uwe matron kwenye sherehe yoyote itakayotokea.

sory ila una matatizo ya akir kwaiyo kuleta uzi ndo ukaona mm nasimamia kila mtu sahau.
 
kila mtu sio type yako...mademu wa hapo bongo mna mbwembwe kweli..
 
Mmh mjini kazi bora mimi harusi yangu ya kijijini sikuwa na matron wala nini mume wangu alikuja kujichukulia mzigo wake watu wakapiga mpunga yakaisha
 
Sasa kila mtu sio type yako,wa type yako wakoje labda?
 
nenda wewe kafanye yako kumbuka washiriki ni ila kombe la m1.fnya u2.ucwackilize watu.utapotewa


Wana MMU kwema?
Kuna jambo limenitatiza nikafanya maamuzi ila likanilazimu nililete hapa nione ushauri wenu.

Ni ivi kuna kijana mmoja tunafahamiana kwa mda mrefu ni just a friend ananiheshimu sana kiukweli hatuna lolote ni heshima tu ya mda mrefu (kwanza si type yangu so mnielewe).

Majuzi alinipigia simu yeye na dada yake wanaomba niwe matrion wa mke wake, yaan huyo kijana ndo anaoa.
Niwarudishe nyuma kidogo kwa ufupi nakuaga matron sana marafiki zangu wanapenda niwe matron though sio wote nawakubalia.

Huyo kijana na dada yake hata mama yao wote wanajua kuwa hiyo shughuli naweza ndio maana waliniomba.

Waliponambia nilitaka kukataa lakini nikaona mama yao atanielewaje? Halafu ikifika siku yangu je watanisaidia?

Si mnajua mambo ya sherehe ni watu?

Basi nilikubali akanambia send off in mwezi wa november, so aliniomba mke mtarajiwa aje kwangu nimuone tuongee mambo fulani.

Kweli bi dada alikuja nikampokea ni kampa customer care zote.

Basi aliniomba kuangalia picha ambazo nilishasimamia send off mbalimbali nikampa akaangalia kweli alisifia sana.

Aliniuliza sasa dada mm nitapendeza kwa vazi lip? Nikamwambia tuvae tofauti kidogo na hapa bongo walivo zoea.

Kweli alipenda mavazi ya sendoff za kwetu.

Alikubali akaniomba mambo fulani nikamwambia hakuna shida nitasaidia though nigharama.

Wakati anaangalia picha niliona anaangalia picha huku akinitizama.

Nilichukulia poa, alishukuru sana na akanisisitiza nimsaidie niwezavyo apendeze.

Muda ulifika nikamsindikiza akarudi kwake.

Tatizo lenyewe alipofika kwao huko kwao aliwambia mashoga zake kuwa kapata matron hao mashoga zake walikuwa wanne. Walimwambia tumuone whatsap(si wadada mnajua zetu) kumbe mmoja wapo ni rafiki yangu nakwenye facebook, nilisoma nae advanced so alinijua.

Kwahiyo katika mashoga zake mmoja akaanza wewe(bi harus mtarajiwa) wewe ni mjinga sana utatafutaje matron ambae hamuendani kwani yeye ndo anaolewa?

Ivi nani alimtafuta? Akawambia ni mme wake na dada yake kweli walisema mengi sana mpaka mmoja naomba nisiyaseme.
So yule ambae ni rafiki yangu fb akanitafuta akanambia kila kitu kweli nilijiskia vibaya maana hakunificha lolote

Ukweli ni kwamba bidada na mimi niliona hatuendani kabisa labda tunataka kufanana rangi tu ila pengine sijisifii hatuendani yaani sikustahili niwe matron wake.

Lakini nikasema kama wameridhia poa nisikatae wakasema naringa.

Ikumbukwe kuwa bi dada alipo kuja nilimuhuliza vipi kwenu huwezi pata matron? Akasema sio wazoefu na sherehe itafanyiwa hapa mjini so nitafaa mim.

Baada ya hayo yote walonitukana mashoga zake kumbuka kwenye sherehe watakuwepo nikawaza watakavyokuwa nanyooshewa kidole nikasema hapana isiwe ishu siendi though nitafanya yafuatayo.

1.Mchango natuma

2.Vitu alivoniomba namtumia

3.Sitoi sababu ya kutoenda namwambia atafute mwingine ili nisimsalti yule rafiki yangu facebook aliniambia.

Mama wa kijana juzi alinipigia akanambia nitakuja nikamwambia mungu akijaria huyo mama ananipendaga sana.

Wana mmu maneno walosema lililoniuna ni ili (' au huyo matron alikuwa mchepuko wake?) ndo maana alimtafta?' jamani limeniuma ukizingatia mkaka mwenyewe si type yangu afu ni under age below 30 kwangu hapana coz na mm niko under 30 jamani imeniuma nitaonekana kituko nikienda hasa wale mashoga wa bi harusi.

Jamani familia ya kijana tunaheshimiana sana ila ndo ivo tena.kwanza wamenipunguzia gharama.

Jaman maamuzi haya ni sahihi? Je ikifikazangu yangu mda ukifika wanaweza susia sherehe yangu?

Naomba ushauri.

karibuni wote.
 
Back
Top Bottom