Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
Kuna baadhi ya nyimbo za bongo fleva huwa nikiziskiliza najihi kama msanii husika aliniimbia mimi, yaani inatokea wimbo unanigusa moja kwa moja! Nyimbo zifuatazo huwa zinarandana na nyakati tofauti tofauti za maisha yangu:
Mwambieni nampenda (baba uko wapi?) by Q-chief
Huu wimbo huwa unanigusa moja kwa moja na hasa katika maneno yanayotengeneza ujumbe ambayo Q chilla aliyatumia hapa! Huwa Nakumbuka namna maisha yangu yasivokuwa na historia chanya kumhusu baba!
Ningekusamehe by 20% & Mama Halima by Linex:
Kipindi fulani, hata sijui ilikuwaje! Ikatokea kumpenda binti mmoja, japo hakuwa mzuri wa kiviile, lakini alikuwa na moyo wa upendo ambao kwa binadamu wa kawaida lazima ange-appreciate! Katika hali ambayo hata sikuelewa, alikuja kubeba mimba ya mtu mwingine nikiwa chuo mji mwingine, akahama na mji, akaenda kuolewa, akapotea jii! 10 years later nikaja kubambana nae FB!
Mkuki moyoni ba Afande sele, Mapito by Lord eyez & Nishike mkono by Darasa:
Hizi kwangu ni bonge la historia! Maisha ya ki-gangstar niliyoishi nikiwa o-level yanafanya nizipende sana hizi ngoma! Kipindi kigumu sana cha utoto kilinipitisha katika nyufa nyingi za hatari. Kuna wakati ukinambia nisimulie namna gani nimefika hapa huwa sina maelezo ya moja kwa moja! Nimeshachomwa sana na mkuki moyoni! Niliitaji sana kushikwa mkono na si tu sikuwa na mtu wa kunishika mkono bali pia nilikuwa sivutii kushikwa mkono!
Kwa kuwa wasanii na sanaa ni mali ya jamii, najua hata wewe kuna ambazo zimekugusa na kama si kwa masika huenda ni kwa kiangazi ama vuli! Tupia zipi na za kina nani!